Faida na hasara za kufanya biashara kwa kutumia Cheki(Check,Cheque)

Masokotz

JF-Expert Member
Nov 26, 2018
3,493
5,528
Wajasiriamali wengi wadogo hufanya biashara kwa kutumia CASH.Akienda kununua mzigo kariakoo anaenda na cash,akaenda kulipa wafanyakazi anaenda na cash.Kila kitu wanatumia Cash.Swali la kujiuliza ni Je ku na faida gani mtu kutumia Check badala ya Cash?

Nianze kwa kueleza kidgo check ni nini.Unapopewa check Book na benki umepewa PESA ambayo wewe utaamua thamani.Umepewa uwezo wa kutengeneza PESA.Inakupa uwezo wa kutoa ahadi na kujenga uaminifu(TRUST).Check zinapoenda benki kwako zinakuwa considered kama Value ambapo huwa katika status ya Cleared na uncleared.Cleared Cheque ni check ambayo tayari pesa yako imepokelewa kwenye akaunti yako na uncleared check ni ile ambayo bado.kupokelewa.Check inaweza kuwa postdated(yaani ukaanidka check ya tarehe ya mbele na kumpatia mtoa huduma kulingana na makubaliano).

Biashara ya kutumia check ni lazima wafanyabiashara muwe na makubaliano maalum mfano.Kama wewe huwa unanunua mzigo Kariako kila mwezi wenye thamni ya Milioni 45 na anayekuuzia ni mtu yuleyule basi wewe unaweza kuingia makubaliano maalum na mtu yule yakufanya biashara kwa Credit.Achana na ile mikopo(Credit za under the Carpet)ambazo mara nyingi inakuwa haiko kisheria.Hii inakuwa ni mikopo ambayo unaweza kuiingiza katika taarifa zako za fedha kama Liabilities.Mkishakuwa na makubaliano maalum ni rahisi sana kuandikiana check na kisha unampatia mlengwa au unaenda kwenye akaunti yake moja kwa moja na kudeposit check hio.

Unapokuwa na mkataba wa kibiashara na mtu ule mkataba unakupa wewe uhakika wa kupata mali na uhakika wa kulipwa na inakuepusha na kuibiwa au kutapeliwa wakati unapeleka pesa benki.Matumizi ya cheki yatakuwezesha pia kuwa na transactional history na benki ambayo inakuongezea wewe credit rating na uwezo wa kupata mkopo mkubwa zaidi kutoka Benki.

Gharma za kutumia cheki ni nafuu zaidi kuliko miamala ya simu na hii ianpunguza pia gharama za withdrawal kwani unatoa pesa kutoka kwenye akaunti na kwenda kwenye akaunti.Kadiri biashara inavokuwa unaweza fika hatua ya kutumia ebanking kuhamisha pesa moja kwa moja ingawa gharama zake zinaweza kutofautiana.

Hata hivo kuna kitu kinaitwa ELECTRONIC CHEQUE.Nimewahi tumia hio nikiwa nje ya nchi ingawa kwa hapa Tanzania sijafahamu kama kuna benki zinatoa huduma hiyo lakini ni kama check zingine ila yenyewe inakuwa electronically generated.

Kuna faida nyingi sana za kufanya biashara kisasa kuliko kienyeji kwani zinaondoa stress na mashaka na hatari ya kufanyiwa uhalifu.

karibuni tujadili uzoefu wenu katika kutumia Check katika biashara
 
Back
Top Bottom