Faida na fursa za kusoma nje ya nchi

Liston Cosmas

Liston Cosmas

Member
Joined
Mar 4, 2015
Messages
5
Points
45
Liston Cosmas

Liston Cosmas

Member
Joined Mar 4, 2015
5 45
Habari zenu wadau! Kwa muda sasa, watu wengi wamekuwa wakiniuliza ni namna gani wangeweza kupata fursa ya kusoma nje ya nchi. Kwa hakika kusoma nje ya nchi kuna manufaa makubwa sana zaidi ya kusafiri kwa ndege pamoja na kupata fedha za udhamini wa masomo. Kama kijana alipata bahati ya kusoma nje ya nchi kuanzia A-Level hadi chuo kikuu, nataka kukufahamisha faida chache za kusoma nje ya nchi.

1. Kuongeza uwezo wako wa lugha
Kusoma kwenye nchi nyingine itakulazimu kujifunza lugha ya nchi husika ili uweze kuwasiliana na kuitumia kujifunza mambo mbalimbali.
Kwa mfano watu wengi wanaosoma nchi za ulaya au Marekani huongeza uwezo wao wa kuzungumza kiingereza zaidi.
Hivyo kusoma nchi za kigeni kutakuwezesha kujifunza na kuongeza uwezo wako wa lugha za kigeni kama vile Kichina, Kifaransa, Kijapani, Kiingereza, Kijerumani, n.k.

2. Kujifunza utamaduni mpya
Kila nchi ina utamaduni wake ambao kwa namna moja au nyingine unatofautiana na wa nchi nyingine. Unapokwenda kusoma nje ya nchi, ni wazi kuwa utajifunza utamaduni mwingine tofauti na ule uliouzoea.

3. Kupata marafiki
Marafiki ni muhimu sana kwenye maisha, hasa marafiki sahihi. Kwa njia ya kusoma nje ya nchi utajipatia marafiki toka sehemu mbalimbali duniani; hii ni kutokana na kukutana na watu kutoka nchi mbalimbali mara uwapo chuoni.
Marafiki hawa utakaowapata kutokana na kusoma nje ya nchi wanaweza kukufaa kwenye maisha yako yote. Inawezekana pia ukapata mwenzi wa maisha unaposoma nje ya nchi.

4. Kujifunza mfumo mpya wa elimu
Mifumo ya elimu hutofautiana kati ya taifa moja na jingine. Hivyo kusoma nje ya nchi kutakuwezesha kuufahamu vyema mfumo wa elimu wa nchi nyingine. Kwa njia hii utaongeza maarifa na ujuzi wako zaidi.

5. Kupanua uwezo wako wa kufikiri
Watu wengi wanaposoma nje ya nchi, hujikuta wakipata fikra pana na uzoefu mkubwa kutokana na yale waliyoyaona huko nje.
Nimeshuhudia watu wakirudi kwenye nchi zao na kutekeleza miradi mikubwa ya kushangaza kutokana na mawazo na fikra chanya walizozipata walipokuwa wanasoma nje ya nchi.

6. Kuufahamu ulimwengu
“Kutembea ni kuona mengi.”
Unaposafiri kwenda nchi nyingine kwa ajili ya masomo, ni wazi kuwa utajifunza na kuufahamu ulimwengu zaidi. Uwapo masomoni unaweza kutembelea maeneo mbalimbali ya nchi husika na ukajifunza mambo mbalimbali tofauti na kusoma ndani ya nchi yako.

7. Huongeza uzoefu wa maisha
Unapokuwa nje ya nchi kwa ajili ya masomo utajifunza mengi na kufanya mengi; utatakiwa kujipangia ratiba, kutumia pesa vyema, kujihudumia, n.k. Hivi vitakupa uzoefu mkubwa wa maisha jambo ambalo ni tofauti na kukaa kwenye familia yako ndani ya nchi yako.

8. Hukuwezesha kuthamini vitu
Mara nyingi huwezi kuthamini kitu hadi pale unapokikosa. Unapokuwa nje ya nchi utakosa ndugu uliowazoea, vyakula, nguo, maeneo, au hata vitu vingine unavyovipata kwenye nchi yako.
Hili litakuwezesha kuthamini vitu na kujifunza kutumia vyema vile vitu vichache utakavyokuwa navyo nje ya nchi.

Sasa ushajua umuhimu wakusoma nje ya nje, je utapataje nafasi hiyo?
Mabibi na mabwana, nimeanzisha jukwaa la mtandao ambalo linalenga kutumika kuunganisha vijana wa kitanzania wote, waliopo nchini na nje ya nchi, kushirikiana fursa, kujifunza zaidi kuhusu ulimwengu na kutatua masuala makubwa zaidi ya wakati wetu. Tafadhali tembelea website yetu www.anza.me kisha jisajili. Ukishajiunga, unaweza kuniongeza mimi kama rafiki (jina ni Liston Cosmas) na unaweza kuniuliza swali lolote kuhusiana na kusoma nje ya nchi. Asanteni, na kila la kheri nyote katika jitihada zenu za kulijenga taifa.
 
Tarakwa

Tarakwa

JF-Expert Member
Joined
Apr 19, 2017
Messages
232
Points
250
Tarakwa

Tarakwa

JF-Expert Member
Joined Apr 19, 2017
232 250

Gharama ya kujisajili?!
 
joshua_ok

joshua_ok

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2012
Messages
8,540
Points
2,000
joshua_ok

joshua_ok

JF-Expert Member
Joined Jun 27, 2012
8,540 2,000
India nako ni nje ya nchi? Lugha gani utajifunza India? Ki-Gujarati kitakusaidia nn?
 
Forum statistics

Threads 1,294,041
Members 497,789
Posts 31,163,268
Top