Mchaichai (Lemon Grass) na faida zake kwa matumizi ya mwanadamu

Lusyonja

Member
Jul 21, 2008
15
16
Salaam Wanajanvi,

Tupo katika mapambano na malaria, hasa kuwatokomeza mbu wanaoeneza hayo malaria.

Mwenye kujua hebu tujuze kama mchai chai (Lemon Grass) unaweza kufukuza mbu pamoja na wadudu wengine kama nzi?

Kama ni kweli hufukuza mbu (insect reppellent-citronella), haya majani yanatumikaje? Pamoja na kwamba watu wengi wanatumia kama kinywaji moto badala ya chai.

Kama utafukuza mbu, je unapatikana sehemu gani?

Nawasilisha

1.KUSAFISHA FIGO NA MKOJO

Mchaichai una kazi ya kusafisha figo ambayo kazi yake kubwa ni kusafisha damu katika mwili, kuondoa mafuta mabaya mwilini ambayo mengi yanatengenezwa na kemikali za viwandani na hivyo mwili kushindwa kuziondoa na baadaye kusasababisha magonjwa mbalimbali.Figo inapokuwa safi na imara,hata kazi nyingine kama kusafisha mkojo zinafanyika

kirahisi


2.HUSAIDIA UMENGENYWAJI WA CHAKULA MWILINI

Mchaichai husifika kusaidia urahisishaji wa mmengenyo wa chakula mwilini na kutibu maumivu ya tumbo kama vile hali ya tumbo kujaa gesi.


3.KUZUIA HALI YA KUHARISHA MARA KWA MARA

Mchaichai pia ni dawa nzuri kwa wale wanaosumbuliwa na hali ya kuarisha mara kwa mara,kwani inauwezo wa kupambana na mdudu aina ya protozoa anayesababisha ugonjwa huu.


4.HUSAIDIA KUSAFISHA DAMU

Faida nyingine ya mchaichai ni kusafisha damu mwilini hasa kwa watu ambao wamekuwa na tabia ya kupata magonjwa ya ngozi kama mapele na kutoka majipu.


5.HUUPA MWILI KINGA DHIDI YA UGONJWA WA SARATANI.

Mchaichai umegundulika pia unauwezo wa kuua seli zinazoweza kusababisha ugonjwa wa saratani.Kwani kwenye gila gram 100 ya mchaichai kuna virutumbisho ambayo vinaweza kuondoa na kuukinga mwili dhidi ya sumu ambayo inasababisha ugonjwa wa saratani.


6.KUONDOA MLUNDIKANO WA MAFUTA KATIKA MISHIPA YA DAMU

Mchaichai husaidia kuondoa mafuta katika mishipa ya damu hivyo kuruhusu damu kupita vizuri katika sehemu mbalimbali za mwili na kuifanya mishipa hiyo kuwa na afya njema.Pia kusaidia mapigo ya moyo kuwa katika hali nzuri wakati wote.


JINSI YA KUTUMIA MCHAICHAI

Kupata faida hizi unashauriwa majani ya mchaichai yalowekwe katika maji ya moto kiasi cha vikombe vitatu vya chai, weka majani ya mchaichai kisha kunywa maji hayo kiasi cha kikombe kimoja cha chai kabla ya kula chochote asubuhi, mchana, nusu saa kabla ya mlo, na jioni kabla ya chakula cha jioni.Pia unaweza kutia sukari kwa kiasi kidogo mno. Unaweza fanya jambo hili kuwa endelevu kwa kutumia chai ambayo imepikwa kwa majani ya mchaichai mara kwa mara.

[https://4]


Kumbuka faida zilizo tajwa hapo juu ni chache tu ambazo nimekuletea siku ya leo na ni matumaini yangu utanza kutumia mchaichai kuwa sehemu ya lishe yako ili kupata virutubisho mbalimbali na kujikinga dhidi ya magonjwa mbalimbali.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hizi ni baadhi ya faida za kunywa chai yenye mchai chai katika mwili wa binadamu.

1. Kuzuia kutapika

2. Kutuliza maumivu ya tumbo

3. Kupunguza makali ya homa.

4. Msaada kwa wenye tatizo la baridi yabisi,

5. Husaidia kusafisha figo

6. Huzuia tatizo la tumbo kuunguruma

7. Husaidia uyeyushaji wa chakula

8. Hupunguza uwezekano wa kupatwa na maumivu mbalimbali ya mwilini.

9. Husaidia kupunguza maumivu kwa kinamama wakati wa hedhi
 
Mchaichai una faida nyingi zaidi ya kufukuza wadudu za kutia harufu nzuri ( kwenye vyakula na vipodozi).

Mchaichai ukichumwa na kuchemshwa waweza kunywewa kama tiba ya kuua cells za cancer.

Madaktari hushauri wagonjwa wanaopata tiba ya mionzi kunywa chai hii kwanza kabla ya tiba!

SOMA HAPA CHINI:

Lemongrass is a perennial, aromatic tall grass with a light lemon scent used for culinary and medicinal purposes. For centuries, herbalists have used the herb as an effective digestive tonic and nervous system relaxant.

Lemon grass oil is used to help clear blemishes and maintain balanced skin tone. Lemon grass is also used as an insect and mosquito repellent.

Now, according to Israeli scientists, they can add cancer prevention to the list of attributes associated with lemon grass
 
Ukweli Mchai chai hafukuzi mbu wala nzi nyumba yetu ilikuwa imezungukwa na michai chai kwa ajili ya kufanyia chai na kupikia mchuzi.

Binafsi kwetu ikifika magharibi mbu huwa kama vile nzi wamegunduwa mzoga na maleria yalikuwa yana nisumbuwa kiasi kama kwetu tungekuwa washirikina basi watu wangesema nimerogwa hiyo ilikuwa ni miaka ya 80 hadi 90.

Kwa taarifa yako, mchai chai hauna matibabu badala ya kuwa kiungo wakati wakupika mchuzi na kufanyia chai kama huna majani ya chai chai yake inanukia vizuri pamoja la ladha yake.
 
Hujambo ndugu,

Nimesoma kutoka kwa mtandao ya kuwa ungependa kupata habari kuhusu 'Lemon grass.

Mimi ni mkulima kutoka Kenya na huu ni mojawapo ya mimea ambayo ninakuza.

Kama ungetaka habari zaidi nitakupasha vilivyo.
 
habari za asubuhi wadau, langu ni moja tu naombeni msaada ni wapi nipate mchaichai? ikiwezekana nipate mche kwa ajili kupanda ili niwe nafanya machumo nyumbani kwangu.
 
ooh please this is bull shit mwisho utatuuliza wapi wanauza condoms nzuri, do not lower this jukwaa this low you surely know where to ask for mchai chai wa nyumbani kwako mimi nilikusoma nikidhani unatafuta suppliers umepata soko kwa hiyo unategemea mtu akwambie ninao nyumbani kwangu ama nenda kona ya pili kwa mwajuma ama mama Rhoda?
 
ooh please this is bull shit mwisho utatuuliza wapi wanauza condoms nzuri, do not lower this jukwaa this low you surely know where to ask for mchai chai wa nyumbani kwako mimi nilikusoma nikidhani unatafuta suppliers umepata soko kwa hiyo unategemea mtu akwambie ninao nyumbani kwangu ama nenda kona ya pili kwa mwajuma ama mama Rhoda?

Nndondo, heshima yako,

Jamaa kaomba msaada wa huo mchai chai ambay labda ni tiba ya magonjwa fulani na ndiyo maana akatuma hapa kwenye hili jukwaa. Mimi nilifikiri ungeuliza nini matumizi ya huu mchai chai na kadhalika lakini wewe umeamua kutoa hukumu.

Tukirudi kwa muulizaji, nenda hapo karibu na tangi bovu au kwenye vitalu vya wauza miti na maua utaweza kupata huo mchai chai
 
Mheshimiwa sana nndono punguza JAZBA.. Nitafute ninao nyumbani kwangu..(ni PM please):painkiller:
 
hebu tuelimishane, apart from being kiungo cha chai, matumizi yake mengine ni yapi? japo nakumbuka mama yangu alikuwa akiuchemsha na kuchanganya na majani mengine tunakunnywa sijui unatibu ugonjwa gani hasa.
 
Unanukia vizuri sana kwenye chai..ila inapatikana sehemu nyingi sana mtoa mada zunguka tu utakumbana nayo
 
Tatizo hajaeleza yeye mwenyewe yuko wapi.

JF ni kubwa, wengine wapo Dar, wengine Kyela, wengine China, US nk. Sasa kama upo Mogadishu nikikuambia njoo nyumbani hapa Tunduma mimi ninao mchaichai, si utaona kama ninakukebehi?

Ni vyema ukasema wewe uko wapi ili walio maeneo ya karibu wakusaidie. Hata huyo aliyesema ipo Tangi Bovu amejaribu ku~guess tu kwamba upo Dar.
 
Kwani nini faida ya mchaichai ki-afya ukiondoa suala zima la kuongeza ladha ya chai??
 
asante sana mdau kwa msaada wako na kuwa miongoni mwa walioelewa nini hasa nilikuwanataka. leo leo naenda pale tangi bovu kujipatia mche.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom