Faida kwenye biashara ya Guest House...

Fernando sucre

JF-Expert Member
Jul 14, 2018
295
500
Wakuu naomba kuuliza hivi mmiliki wa guest house anapataje faida kwenye biashara yake? Je, huwa anampa msimamizi target ya hela kila siku au weekly? Kwasababu msimamizi anaweza kodisha vyumba 10 akasema pungufu.

Msaada wenu kwenye uelewa wa hili.
 

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
3,588
2,000
Kaa mwenyewe kwa muda wa mwaka.., utajua peak times na slow times na utajua average ya mapato kwa siku, mwezi na mwaka..., ukimuachia mtu ikiwa pungufu ni either hajui kazi (customer care) au ni mwizi..., hivyo vyote ni vigezo vya kutafuta mwingine
 

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
4,874
2,000
Funga Camera kila chumba

show tiime zikapigiwe choooni

ila mteja akitumia tu kitanda DAI PESA yako ukja kufata hesabu

Bila camera Utalizwa mpk ukione,labda ukae mwenyewe
 

CONTROLA

JF-Expert Member
Sep 15, 2019
4,874
2,000
Kamera zinapaswa kufungwa kwenye korridor na siyo kila chumba, kwani wateja ni binadamu wenye kuhitaji faragha zao ziheshimiwe na kutunzwa, na hukifanya hiyo jua biashara yako unaichimbia kaburi mwenyewe.
natumaini umenielewa
 

Sky Eclat

JF-Expert Member
Oct 17, 2012
46,461
2,000
Mleta mada uaminifu kwanza unahitajika sana kwa pande zote mbili. Msimamizi ajue kuwa mwenye mali akipata hasara biashara itakufa na mwenye mali amlipe msamamizi mshahara anaostahili.

Changamoto kubwa ya guest house ni uhakika wa maji. Siku hizi vyumba vingi ni en-suite hapa matumizi ya maji yanaongezeka. Maji ya kufanyia usafi na kufulia shuka kila siku.
 

PTER

JF-Expert Member
Dec 28, 2014
12,415
2,000
Ni ngumu sana kuzuia wizi kwenye biashara yoyote ile.
Nikipata muda nitakupa hints kidogo ambazo mimi nilizitumia
Wakuu naomba kuuliza hivi mmiliki wa guest house anapataje faida kwenye biashara yake? Je, huwa anampa msimamizi target ya hela kila siku au weekly? Kwasababu msimamizi anaweza kodisha vyumba 10 akasema pungufu.

Msaada wenu kwenye uelewa wa hili.
 

Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,539
2,000
Wadau ambao wapo kwenye hii biashara wachoyo kinoma kwenye infos!

Wachangiaji wengi ni wateja zaidi wanaotumia uzoefu wao tu kuliko wamiliki..

GH inahitaji camera au uwe unashtukiza (usitabirike),niliwahi kuongea na kijana mhudumu mmoja wa mahali nilipokuwa nimefikia ambapo tajiri alikuwa mkoa tofauti.

Kitabu cha wageni kipo lakini ana rooms zake 2 or 3 hawaandiki daily na kaanzisha huduma ya kulipisha watu baki (majirani) kuoga hapo kwa malipo na anakunja yeye.

Nataka niweke pesa huku pia.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom