Zifahamu faida kuu 17 za majani ya mpera kiafya

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,589
20,898
FAIDA ZA KUTUMIA MAJANI YA MPERA KWA AJILI YA AFYA YAKO
  1. Chai ya majani ya mpera inasaidia mwili kuwa stadi, inasaidia madini ya carbohydrates yasigeuzwe kuwa sukari ndani ya mwili hivyo kupunguza hamu ya kula.
  2. Chai ya majani ya mpera pia inashusha kiwango cha sukari mwilini na kuzuia mwili kuondoa 'insulin'. Kwa sababu hii wagonjwa wa sukari wanashauriwa kuitumia mara kwa mara.
  3. Chai ya majani ya mpera pia hupunguza lehemu mbaya (bad cholestrol) bila kudhuru lehemu nzuri.
  4. Chai hii ina nguvu za kudhibiti vijidudu vya magonjwa mwilini hasa kuzuia magonjwa ya kuharisha na kipindupindu.
  5. Chai hii inalinda mchafuko wa tumbo na pia inasaidia kukabili madhara yaletwayo na chakula chenye sumu.
  6. Chai hii hutibu kukohoa na kupumua kwa tabu.
  7. Upatapo uvimbe wa fizi na maumivu mdomoni kama jino kuuma, tafuna majani ya mpera.
  8. Kwa matatizo ya homa ya dengue, chemsha glasi mbili na nusu na majani ya mpera (kadiria majani 9) mpaka maji yabakie nusu ya ujazo wa awali.
  9. Chai ya majani ya mpera imefahamika kutibu kansa na 'prostate' kwa wanaume.
  10. Chai hii inasaidia kwa wanaume wenye tatizo la kuzalisha (Infertility).
  11. Ponda majani ya mpera na kuweka sehemu ya kidonda au iliyokatika kuondoa maambukizi. Kwa maumivu nje ya sikio tumia chai ya majani ya mpera. Tia matone ya chai hii iliyopoa kwenye sehemu iliyoathirika.
  12. Majani ya mpera hupondwa na kupakwa eneo lenye muwasho uletwao na allergy.
  13. Unapoumwa na wadudu majani yaliyopondwa ni tiba sahihi.
  14. Majani ya mpera yana saidia kupigana na mba na chunusi kutokana na wingi wake wa vitamini C.
  15. Kuondoa madoa meusi kwenye ngozi ponda majani ya mpera changanya na maji kiasi na upake badala ya dawa za kawaida.
  16. Fanya kama namba 15, kwa tatizo la ngozi kuzeeka mapema.
  17. Majani ya mpera yanaondoa tatizo la kukatika kwa nywele. Chemsha majani kisha wacha yapoe na ukande kwenye paji na eneo la ngozi taratibu kwa dakika 15. Wacha kwa dakika 30 kisha osha na maji safi bila shampoo au sabuni. Fanya hivyo mara 3 kila wiki.
Wengi wananiuliza namna ya kuitengeza chai ya majani ya mpera. Kuna namna mbili. Aidha chemsha maji kama glasi nne mpaka itokote sana, chukua majani kama 10 ya mpera, weka ndani ya yale maji moto kisha funika kwa dakika 10 - 15 koroga, chuja, chai yako tayari.

Aina ya pili ni chemsha maji hayo pamoja na majani yakiwa ndani. Ikitokota ondoa kwenye moto, wacha kwa dakika 10 -15 chuja, chai tayari. Waweza ukatumia majani yaliyo kauka pia. Zingatia ukichanganya na asali badala ya sukari ndio bora zaidi.



PIA SOMA
MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI.
1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua na
kikohozi.
2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri
yanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio
(allergy).
3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwa
kama chai yanaondoa cholesterol iliyozidi
mwilini.
4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwango
cha tatizo la sukari mwilini.
5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenye
matatizo ya nguvu za kiume.
6. Pia inatumika kama scrub ya uso.
Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasi
na inasaidia kuondoa uchafu usoni.
7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawa
ya kuponyesha tumbo la kuhara.
8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumia
majani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizuri
kwa kupunguza maumivu na kukulinda na
maambukizi ya bakteria.
9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuri
yanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa na
mdudu na kupunguza maumivu.
10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa ina
uwezo wa kutibu tezi dume.
11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingi
majani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibu
chunusi.
12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguza
uzito mwilini na kuzuia uharibifu sukari ndani ya
mwilini.
13. Majani ya mpera yanajaza nywele na
kurefusha nywele kwa watu wenye tatizo la
kukatika kwa nywele, unasaga na kuchemsha
kisha acha yapoe ndio upake kichwani kutoka
chini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha ya
nywele zako.
14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi,
maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mpera
na utaona maajabu ya majani haya.
15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpaka
yawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kisha
tumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngozi
inayoanza kuzeeka mapema.
16. Chai ya mpera inasaidia kwa kutibu
mvurugiko wa tumbo.
Pamoja na majani hayo kuwa msaada wa kutibu
maradhi mbalimbali , halikadhalika juisi ya
mapera nayo husaidia sana kutibu mgolo au
bawasiri, figo na hata kuondoa mafuta katika
moyo.
Kimsingi mti wa mpera karibu kila sehemu yake
ni tiba kwani hata mizizi yake inapochemshwa na
kutumia kwa kunywa huenda kuwasaidia
wanawake wenye matatizo ya hedhi au wenye
matatizo ya kutokwa na maji yenye harufu
mbaya sehemu zao za siri.
AHSANTENI SANA……………
Usiache ku-SHARE na wengine wapate elimu hii
+255653216061/call/WhatsApp/text
 
MAJANI YA MPERA NA FAIDA ZAKE MWILINI.
1. Chai ya majani ya mpera inaponyesha kifua nakikohozi.

2. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuriyanatumika kutibu muwasho uliotokana na mzio(allergy).

3. Pia majani haya ya mpera yakichemshwakama chai yanaondoa cholesterol iliyozidimwilini.

4. Chai ya majani ya mpera inapunguza kiwangocha tatizo la sukari mwilini.

5. Chai ya mpera ni dawa nzuri kwa wenyematatizo ya nguvu za kiume.

6. Pia inatumika kama scrub ya uso.Chukua majani ya mpera saga kisha tia maji kiasina inasaidia kuondoa uchafu usoni.

7. Pia majani ya mpera yakichemshwa ni dawaya kuponyesha tumbo la kuhara.

8. Kama umejikata kidogo unaweza kutumiamajani ya mpera yalioshwa na kusagwa vizurikwa kupunguza maumivu na kukulinda namaambukizi ya bakteria.

9. Majani ya mpera yaliyosagwa vizuriyanatumika kutibu eneo la mwili lililong'atwa namdudu na kupunguza maumivu.

10. Chai ya majani ya mpera inaaminika kuwa inauwezo wa kutibu tezi dume.

11. Kutokana na kuwa na vitamini C kwa wingimajani ya mpera yana uwezo mkubwa wa kutibuchunusi.

12. Chai ya majani ya mpera inasaidia kupunguzauzito mwilini na kuzuia uharibifu sukari ndani yamwilini.

13. Majani ya mpera yanajaza nywele nakurefusha nywele kwa watu wenye tatizo lakukatika kwa nywele, unasaga na kuchemshakisha acha yapoe ndio upake kichwani kutokachini ya ngozi ya kichwa hadi kwenye ncha yanywele zako.

14. Ukiwa na tatizo la vidonda kwenye ufizi,maumivu ya jino na ufizi tafuna majani ya mperana utaona maajabu ya majani haya.

15. Chukua majani ya mpera saga vizuri mpakayawe laini kabisa ongeza na maji kidogo kishatumia kupaka usoni kama scrub inatibu ngoziinayoanza kuzeeka mapema.

16. Chai ya mpera inasaidia kwa kutibumvurugiko wa tumbo.Pamoja na majani hayo kuwa msaada wa kutibumaradhi mbalimbali , halikadhalika juisi yamapera nayo husaidia sana kutibu mgolo aubawasiri, figo na hata kuondoa mafuta katikamoyo.

Kimsingi mti wa mpera karibu kila sehemu yakeni tiba kwani hata mizizi yake inapochemshwa nakutumia kwa kunywa huenda kuwasaidiawanawake wenye matatizo ya hedhi au wenyematatizo ya kutokwa na maji yenye harufumbaya sehemu zao za siri.

AHSANTENI SANA.Usiache ku-SHARE na wengine wapate elimu hii+255653216061/call/WhatsApp/text
 
Haha hata kwa wale wanawakw wenye kuwashwa ukeni wanashauriwa kuchemsha majani ya mpera waache yapoe kisha wanawia huko na hayo maji hata U.T.I una blend majan ya mpera na maji kisha unakunywa juice yake
 
Sasa waenda chumvini tunaweza hisi kis.imi ni tunda za pera kwa harufu ya pera pera ....
Haha hata kwa wale wanawakw wenye kuwashwa ukeni wanashauriwa kuchemsha majani ya mpera waache yapoe kisha wanawia huko na hayo maji hata u.t.i una blend majan ya mpera na maji kisha unakunywa juice yake
 
Ni vyema muwe Mnatoa na maelekezo ya dozi ya hizi miti shamba, mtu anywe kiasi gani kwa siku na kwa mda gani,. La sivyo mtakuja kusababishia watu matatizo
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom