Faida kugeuza gari yangu binafsi kuwa UBER

stephen4440

JF-Expert Member
Apr 12, 2018
817
1,000
Wakuu habari,

Leo nimekutana na mtu amenishawishi kuigeuza gari yangu binafsi kuwa uber, Naomba kufahamu je inalipa?

Gari yangu ni mpya sio kwamba nina shida sana na pesa bali amenishauri kwamba kwa muda ambao silitumii gari basi liwe barabarani kama uber.

Binafsi sitoweza kuendesha kama dereva wa uber hivyo lazima nitamkabidhi dereva kwa mkataba.

Je, vipi kuhusu usalama wa chombo changu? Naomba wenye uzoefu na hii biashara mnishauri.

Nawasilisha.
 
Consultant

JF-Expert Member
Jun 15, 2008
10,555
2,000
Huyo rafiki yako aliyekushawishi yeye ana gari? Kama analo, analitumia kama uber? Yeye ni driver wa uber? Alishawahi kuwa driver wa uber au alishafanya biashara hiyo?

Kama jibu la swali mojawapo hapo juu ni hapana, achana na hilo wazo. Usipende kupokeapokea ushauri kutoka kwa watu wasio na uzoefu wowote na jambo wanalolizungumzia.
 
Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,353

Ushauri unaweza kuuchukua ama kuuacha!!

Na ukipewa ushauri usiuache upotee, pata muda wa kuufuatilia kwa mapana kama alivyofanya hapa ikiwa ni sehemu ya kupata maoni mbalimbali.
 
DIKASHWA

JF-Expert Member
Aug 2, 2016
278
1,000
Kwenye haya maisha kuwa na malengo, je hili gari ulilinua kwa malengo gani? Kama ilikuwa biashara sawa kama ilikuwa la kutembelea komaa na lengo lako, sio kwamba ukilifanyia biashara ni vibaya ila kwenye biashara kuna kupata na kukosa unaweza ukaletewa hadithi nzuri za uba ila kwenye uhalisia sio gari litachakaa na litatembezwa km nyingi na faida kiduchu.
 
Trubarg

JF-Expert Member
Jan 8, 2020
1,958
2,000
Labda hiyo uber uendeshe mwenyewe..otherwise hilo gari kitakua kopo soon..maana ww uendeshe Dereva aendeshe...likiharibika hapo Kati humtajua aliyeliharibu
 
kamituga

JF-Expert Member
May 31, 2019
1,070
2,000
Ambae anashida na pesa awezi ata kuwaza km iyo ni biashara sahisha kwanza af tukushauri.
 
Maulaga59

Senior Member
Feb 1, 2021
197
250
Wakuu habari
Leo nimekutana na mtu amenishawishi kuigeuza gari yangu binafsi kuwa uber, Naomba kufahamu je inalipa? Gari yangu ni mpya sio kwamba nina shida sana na pesa bali amenishauri kwamba kwa muda ambao silitumii gari basi liwe barabarani kama uber. Binafsi sitoweza kuendesha kama dereva wa uber hivyo lazima nitamkabidhi dereva kwa mkataba, Je, vipi kuhusu usalama wa chombo changu? Naomba wenye uzoefu na hii biashara mnishauri. Nawasilisha

Naomba kuuliza: Hivi UBER ni nini katika haya magari ya kusafirisha abiria?
 
Mad Max

JF-Expert Member
Oct 21, 2010
6,588
2,000
Mkuu, usifanye hiyo biashara. Utaharibu gari lako ndani ya miezi 6 litakua ovyo.

Mi hiyo biashara nilifanya kwa gari langu, lakini enzi izo Uber ulikua unajisajiri na number plate izi za njano haikua na complications sana, hakuna Jiji wala Majembe wa kunibana. Nilikua naweka pesa nzuri sana kwa siku. Ilikua 2017/18.

Ila washkaji zangu sahivi wanajuta. Biashara imekua ngumu. Madereva sio waaminifu. Wateja wachache. Magari mengi. Upinzani mkubwa.
 
Lihove2

JF-Expert Member
Mar 23, 2018
1,865
2,000
Wakuu habari
Leo nimekutana na mtu amenishawishi kuigeuza gari yangu binafsi kuwa uber, Naomba kufahamu je inalipa? Gari yangu ni mpya sio kwamba nina shida sana na pesa bali amenishauri kwamba kwa muda ambao silitumii gari basi liwe barabarani kama uber. Binafsi sitoweza kuendesha kama dereva wa uber hivyo lazima nitamkabidhi dereva kwa mkataba, Je, vipi kuhusu usalama wa chombo changu? Naomba wenye uzoefu na hii biashara mnishauri. Nawasilisha
Kama huna shida sana na hela si uliache gari lipaki tuu.Ya nini kuanza kuuliza uliza risk tena za uber?
 
Ligogoma

JF-Expert Member
Aug 27, 2010
3,353
2,000
Kama huna shida sana na hela si uliache gari lipaki tuu.Ya nini kuanza kuuliza uliza risk tena za uber?

Uelewa unatokea mbali sana!!

Mfano rahisi; Ulishawahi kuona mtu ana eneo limekaa tu, hana mpango wa kujenga wala kuuza!! Akatokea mtu akamshauri ukijenga hotel hapa utapiga biashara sana!! Akaanza kutafuta risk za kuinvest hotel?? Na pengine akainvest kweli na akatoboa!!?

Ni sawa na hili, si kwamba ana pesa ila gari lipo tu kwamba kuliweka kibiashara inawezekana ila mpango huo hakuwa nao!! Na kapata hiyo idea!! Si kwamba kajigamba!!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom