Faida kubwa za serikali tatu na maoni ya tume ya Warioba.

NJUGHU

JF-Expert Member
Aug 16, 2013
381
261
UWAJIBIKAJI(Responsibility) Uwepo wa dola yenye fedha,Tanganyika au Zanzibar na dola yenye Jeshi Tanzania kutatoa ukiritimba wa ufisadi ambao hutokea na hamna paka wa kumfunga mwenzie kengele.mf.Rais wa muungano anaweza toa msimamo kwa serikali kuwajibika hasa inapotokea mambo kama ya ufisadi,uvunjaji wa haki za binadamu.Na upande wa pili wa serikali shirikisho zina uwezo wa kuhoji mambo ambayo serikali kuu imeenda kinyume na katiba.

UWAZI(Transparence)
Hamna uficho utakaofanyika ndani ya hizi serikali bila moja kuafiki hasa ktk matumizi ya fedha,maamuzi ya kiitikadi au ambayo hayana nia nzuri na nchii hii.

KUTENGANISHA SIASA NA SERIKALI.
Pendekezo la watendaji kutokuwa wanasisa hasa mawaziri kutokuwa mawaziri kutaweka uwajibikaji na usimamizi mzuri wa shughuli za maendeleo na kututoa ktk umaskini.

Zipo faida nyingi wana JF wenzangu tuongezee ili tuongee kwa hoja na kwa manufaa ya nchi zetu.
 
Back
Top Bottom