Faida hasara na unyanyasaji raia wa kitochi cha usalama barabarani

kmbwembwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2012
7,270
2,000
Sheria ya usalama barabarani licha ya lengo lake kutakiwa kusababisha usalama wa usafiri barabarani imekua ikitumika vibaya na wasimamizi wake wote kuwapatia ulaji.

Ndivyo ilivyo pia kwa uanzishaji wa tochi au kamera za kudhibiti mwendo barabarani. Wakati raia wakitarajia kupungua ajali askari wanazifurahia kama kitendea kazi kujiongezea mapato kwa njia ya rushwa. Kutokana na hivyo wanabughudhi madereva kwa kuwachomekea makosa kwa kutumia vibaya teknologia ya tochi ya mwendo na simu za mikononi.

Tukiwa wazee wawili wastaafu wote madereva tangu ujana na kijana wenu akiendesha tumeshuhudia usumbufu wa askari tukitokea kwenye msiba moshi tarehe 29/12/2020.

Katika safari kwenda na kurudi tumejikuta dereva akiandikiwa makosa mara tatu ya kuzidi mwendo sehemu ya mwisho ikiwa ni kituo mbele ya chekereni operator wa mashine akiwa E 6545 athuman.

Hapo askari mmoja mwanamama sisi wazee tukihoji na kuonesha mashaka ya kielelezo kwenye simu ya askari alitutolea maneno ya kifedhuli na kututishia kutuchenchia na kututia pingu.

Wataalam wa usafiri wanajua ongezeko la ajali nchini ni udhaifu wa usimamizi wa utoaji leseni za kuendesha vyombo vya moto.

Barabara nzuri zinapunguzwa faida yake ya kuwezesha mwendo mkubwa kuokoa muda kutokana na kiwango hafifu cha madereva wanaopewa leseni bila kua na kiwango bora.

Badala yake zinawekwa taratibu za kuzuia mwendo kwa magari nyingi kuliko inavyohitajika na kuwaongezea askari wenye lengo la kujinufaisha binafsi vyanzo vya mapato haramu.
 
Mpuretamu

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
420
1,000
Sheria ya usalama barabarani licha ya lengo lake kutakiwa kusababisha usalama wa usafiri barabarani imekua ikitumika vibaya na wasimamizi wake wote kuwapatia ulaji.
Ndivyo ilivyo pia kwa uanzishaji wa tochi au kamera za kudhibiti mwendo barabarani. Wakati raia wakitarajia kupungua ajali askari wanazifurahia kama kitendea kazi kujiongezea mapato kwa njia ya rushwa. Kutokana na hivyo wanabughudhi madereva kwa kuwachomekea makosa kwa kutumia vibaya teknologia ya tochi ya mwendo na simu za mikononi.
Tukiwa wazee wawili wastaafu wote madereva tangu ujana na kijana wenu akiendesha tumeshuhudia usumbufu wa askari tukitokea kwenye msiba moshi tarehe 29/12/2020.
Katika safari kwenda na kurudi tumejikuta dereva akiandikiwa makosa mara tatu ya kuzidi mwendo sehemu ya mwisho ikiwa ni kituo mbele ya chekereni operator wa mashine akiwa E 6545 athuman. Hapo askari mmoja mwanamama sisi wazee tukihoji na kuonesha mashaka ya kielelezo kwenye simu ya askari alitutolea maneno ya kifedhuli na kututishia kutuchenchia na kututia pingu.
Wataalam wa usafiri wanajua ongezeko la ajali nchini ni udhaifu wa usimamizi wa utoaji leseni za kuendesha vyombo vya moto. Barabara nzuri zinapunguzwa faida yake ya kuwezesha mwendo mkubwa kuokoa muda kutokana na kiwango hafifu cha madereva wanaopewa leseni bila kua na kiwango bora. Badala yake zinawekwa taratibu za kuzuia mwendo kwa magari nyingi kuliko inavyohitajika na kuwaongezea askari wenye lengo la kujinufaisha binafsi vyanzo vya mapato.
Juzi kati nlipigwa tochi katikati ya pori la monduli. Jamaa walitega eneo ambalo kwa jiografia yake huwezi jua 50 imeishia wapi..kweli walikuwa wanazikusanya..haya maendeleo ya teknolojia haya..mmmhhh
 
Masasaa

JF-Expert Member
Oct 23, 2015
458
500
Juzi saa 12 kamili asubuhi nimewakuta mzani wa vigwaza, yaani wao kazi tao ni kuwategea raia
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom