Faida 4 Za Kugeuza Bidhaa Au Huduma Unayotoa Kuwa Kampuni Ndogo Na Hatua Rahisi Za Kusajili Kampuni

JAMII BORA

Member
Apr 18, 2017
78
125
Business Digitalization Solution tumekuwa kwa zaidi ya miaka minne tukiwasaidia wajasiriamali wadogo kukua, yaani kutoka hatua ya mjasiriamali mmoja hadi kuwa kampuni ndogo inayotambulika. Kwa kawaida, kama mtaji wako ni kati ya milioni moja mpaka milioni kumi, basi unakuwa na sifa za kuitwa kampuni ndogo daraja la pili.Faida ya kuwa kampuni ndogo unakuwa haujafikia kulipia kodi za kampuni kubwa kama VAT, lakini unakuwa umefikia hatua ya kufaidika na matunda yafuatayo:Moja : Unakuwa umepata sifa ya kuomba Tender

Tazama mfano wa mahitaji ya tender

Company profile should include at least three trade references
(Wasifu wa kampuni yako imeanza lini na inatoa huduma gani wateja watatu uliowahi kuwahudumia)
Certified copy of Certificate of in- cooperation(Cheti cha usajili)
Certified copy of business license (leseni ya biashara)
Certified copy of TIN certificate (Cheti cha namba ya mlipa kodi )

Kwa kukosa document hizo chache, unakuwa umejinyima fursa ya mamilioni. Wastani bajeti inayotengwa kwa tenda mojawapo ya kuandaa application ya taasisi au usafi n.k hufikia milioni 43 walizotenga wateja hawa kwa kazi hii.


Mbili: Kupata fursa ya kuomba pesa za udhamini

Kila mwaka, kuna wadhamini toka nje na ndani wanahitaji kufanya tafiti au mradi na kampuni kadhaa ndogo.mfano wa wadhamini ni pamoja na Viet (partner wa halotel),

Tolly Foundation,U S aid n.k. Wanatumia list ya kampuni ndogo zilosajiliwa, hivyo endapo una bidhaa bora au huduma lakini hauna kampuni ndogo, ni wazi utakuwa umekosa vigezo.

WhatsApp Image 2020-07-31 at 14.38.12.jpeg
Tatu: Kampuni ni rahisi kuendeshwa na familia pale itakapotanuka

Mfano mzuri ni mfanyabiashara Said Salim Bakhresa,alikuwa yeye kama mtu binafsi,hivyo alishindwa kutambulisha wanae aliowaachia waendeshe kampuni hiyo. Lakini aliposajili Bakhresa group of companies, wanae wote kawapa vitengo na wanatambulika ndani na nje ya nchi,kama ifuatavyo:

Yusuph Said Salim Bakhresa:
Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Azam Media Limited na Mkurugenzi wa Group Companies. Anashiriki kila siku kwenye shughuli za Bakhresa Food Products Ltd.

Abubakar Said Salim Bakhresa:
Anasimamia Bakhresa Malawi Limited, Bakhresa Grain Milling (Rwanda), Bakhresa Grain Milling Limitada (Msumbiji) na Bakhresa South Africa (Pty) Limited. Anajihusisha zaidi na biashara za usindikaji ngano katika Group na anasimamia ununuzi wa ngano kwa ajili ya Group.

Mohamed Said Salim Bakhresa:
Ni mkurugenzi Mtendaji wa Bakhresa Grain Milling (Uganda) Limited, kiwanda kikubwa zaidi cha kusindika ngano nchini Uganda.

Salim Ali Salim Bakhresa:
Ni Mkurugenzi Mtendaji wa Verde Hotel. Hoteli Bora ya viwango vya 5 star iliyopo Zanzibar.

Hii ni tofauti na biashara nyingi zinazoyumba na hata kufa mara baada ya muanzilishi wake kuumwa kwa muda mrefu au kufariki kwa sababu hamna mgawanyo mzuri wa majukumu toka mwanzo.


Nne: Kupata maingiliano na wadau wa huduma yako (Connection)

Taasisi nyingi za ndani na nje hutoa mafunzo ya bure kila mwaka kwa kampuni ndogo ili ziendane na mabadiliko ya teknolojia duniani. Mfano wa taasisi hizi ni pamoja na Kuehne Foundation ya Uswizi ambayo huwapa mafunzo wadau jinsi ya kundesha biashara kidigitali , jinsi ya kukabili mabadiliko kwenye biashara ikiwemo kukua kwa technology, au janga la Corona,bure, mingi ya mialiko hupitia kwenye kampuni ndogo.


digital.jpgMwisho ,kutokana na wajasiriamali walioomba tufanye semina kwa vitendo, tumepitia maombi na tumepitisha hilo. Hivyo tumekuandalia group la whatsapp la kukuonesha hatua kwa hatua na kukushika mkono hadi uweze kufanya yafuatayo:

1. Kusajili kampuni

2. Kuandaa tender

3. Kuiweka biashara yako kidigitali ili watumia Internet waweze kukujua

4. Ushauri mbali mbali na kujibu maswali ya changamoto zinazoikabili biashara yako

Piga 0713-039875 kupata ufafanuzi kuunganishwa kwenye group hili kwa ajili ya semina. Jiunge muda huu kabla group kujaa.
 

SHIMBA YA BUYENZE

JF-Expert Member
Dec 22, 2014
134,236
2,000
Wewe jamaa mjanja sana. Mtu anaweza kusoma na asigundue kuwa ni tangazo la biashara mpaka afike mwishoni kabisa
 

JAMII BORA

Member
Apr 18, 2017
78
125
Wewe jamaa mjanja sana. Mtu anaweza kusoma na asigundue kuwa ni tangazo la biashara mpaka afike mwishoni kabisa
Si tangazo .hii ni elimu bure, nimeandika jukwaa hili makala nyingi ,fuatilia. Kuongezeka maombi , ndo kunapelekea tuongeze uangalizi wa karibu kwa wahitaji.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom