Faida 10 za kula Matango

Status
Not open for further replies.

JamiiTalks

JF Advocacy Team
Aug 7, 2018
625
938
IMG_20210512_024559_269.jpg

Ulaji wa matango na matikiti maji husaidia kuboresha kiwango cha maji ambayo huitajika mwilini, hii ni kutokana na matango kuwa na kiwango kikubwa cha maji ambayo husaidia kuondoa taka mwili pamoja na sumu mbalimbali ambazo miili yetu huzipata kupitia vyakula, madawa na hata vinywaji.

(1)Husaidia kupunguza uzito wa mwili. Kutokana na kuwa na asili ya nyuzi nyuzi au, fibres, humfanya mlaji ajisikie kushiba bila ya kuongeza vitu mwilini ambavyo husababisha mtu aongezeke uzito hivyo kuzuia magonjwa mbalimbali

(2)Hupunguza (hangovers),uchovu, mawengewenge pamoja na hali ya kujisikia vibaya kutokana na unywaji wa kilevi. Hii ni kutokana na kuwa na vitamini B na maji mengi ambapo, baada ya mtu kunywa kilevi na kisha akaja kula matango kabla ya kulala, itamfanya asubuhi asiamke huku akiwa na hangovers

(3)Husaidia katika mmeng’enyo wa chakula, matatizo ya tumbo kama vile kuvimbiwa, tumbo kujaa gesi, vidonda vya tumbo na mengineyo hupungua kutokana na ulaji wa matango, husaidia kuondoa sumu tumboni na kurahisisha ufyonzwaji wa protein mwilini kutokana na uwepo wa kiwezeshaji cha kibaiolojia kinachoitwa, erepsin enzyme.

(4)Husaidia kuondoa msongo wa mawazo kwani yana kiwango kikubwa cha vitamini B ambayo husaidia kuboresha utendaji kazi wa mishipa mbalimbali ya fahamu mwilini na hivyo kuondoa hatari ya mtu kuathirika na msongo wa mawazo unaosababishwa na maisha ya kila siku.

(5)Husaidia kuondoa hatari ya mtu kupata kansa. Yana kiwango kikubwa cha virutubisho vyenye asili ya mimea viitwavyo, lignans, ambavyo pamoja na vitamini c,

(6)husaidia kuondoa sumu mbalimbali na kuiboresha kinga ya mwili na hivyo kuepusha hatari ya mtu kupata kansa.

(7)Husaidia kuondoa harufu mbaya kinywani. Kwa kukiweka kipande cha tango mdomoni kwa dakika kadhaa, huuwa bakteria mbalimbali wasababishao magonjwa mbalimbali ya kinywa na harufu mbaya mdomoni.

(8)Husaidia mtu kupata choo laini na huzuia kukosa choo.

(9)Huzuia kuganda kwa mafuta katika mishipa ya damu ili kuwezesha mzunguko sahihi wa damu kaitika pande zote za mwili sambamba na kurekebisha mapigo ya moyo

(10)Huwepo wa vitamini katika matunda haya husaidia kupunguza kiwango cha sukari mwilini na presha.
 
Kila siju nakula papai tikiti ndizi na parachichi.cha ajabu nikiwekewa tango nawambia watoe haraka sana.kumbe zuri? Naanza leo
 
Tatizo matango yanapigwa dawa sana, ukiwa mtu wa sera za kula matunda yasiyo na makemikali basi hii kitu hautagusa.

Tango linaweza likawa inazidi kabichi kwa upuliziwaji wa madawa

Fikiria

- Tango likipigwa na upepo lazima upulize dawa

- Tango likipigwa na mvua lazima upulize dawa

- Tango likipata minyoo ukanyauka mche mmoj tu basi lazima upulize dawa

- Tango likitoa maua tu lazima upulize dawa

- Tango ili litoke na umbo zuri yaani linyooke lazima upige dawa

Na hapo bado dawa kibao za wadudu na zote hizi ni dawa kali kali bado hujafusa mbolea.

Ukila tango labda ule lililotoka kwenye greenhouse maana huku kwa mtanzania mnyonge ni kikali zakutosha.
 
Inabidi Ule matango pori
 
Hii mada wanaosema ni walaji wa matango ni wadada na wanaume wa dar au hata sisi wanaume wa mikoani tunasema tunakula matango kweli?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom