Fahamu zaidi kuhusu Mr Kuku

BRO LEE

JF-Expert Member
Dec 25, 2011
826
600
Habari wana chamvi, nimesoma uzi kuhusu mada tajwa hapo juu nami nataka kushirikishana uzoefu wangu kuhusu huyo 'mwekezaji".

Huyo bwana anaitwa Tariq, mwaka juzi 2018 nilisoma bandiko lake fb kuhusu mradi wa kilimo cha nyanya cha umwagiliaji, ahadi ilikuwa nzuri kuhusu faidi ambapo kiwango cha chini cha hisa ilikuwa 36 na kila hisa 5000/= hivyo unapata 180,000 /=

Baada ya miezi mitatu unapata 360,000/= nilitamani kuwekeza japo nilikuwa na shaka, niliongea nae akanielewesha kwamba uwekezaji ni kupitia vikundi vya watu 15, hivyo akaniunganisha na wadau tukawa na kikundi cha What App tulikuwa mikoa tofauti ila mm niliiona na advantage kwa kuwa mradi ungefanyika jirani.

Tukaanza taratibu za katiba usajili wa kikundi, kabla ya kusajili kikundi akasema tutume fedha ili mradi uanze kuendana na wakati ili kuwahi soko la nyanya.

Baada ya kutoa fedha tulipitia ubabaishaji mwingi sana, mara mradi wa arusha hauwezekani kuna shamba moro, wadau wakataka kwenda moro baada ya muda akasema kule eneo linapitiwa na reli mradi utakuwa Tanga akatutumia vi picha vya eneo na ka tank. Wadau wakalazimisha wakaenda Tanga kufika hakuna kinachendelea.

Tukaanza harakati za kukamilisha katiba na mkataba ili tujipange kwa hatua zaidi. Baada ya muda sana akasema amepata hasara hivyo fedha iliyobaki atawekeza mradi wa kuku uliopa kigamboni. Tukaendelea kupambana na kufuatilia.

Baada ya mwaka baada ya kuwa na maamuzi ya kwenda vgombo vya sheria ndo akaturudishia mitaji yetu na kuahidi faida baada ya muda. Baada tu ya kurudisha mitaji hakuwa anapokea simu wala kujibu hoja za group la What App ambalo tulianzisha. Baada ya kuanza tena harakati za kutaka kufuatilia faida akatoka katika kundi kwa jazba na kusema tufanye tunavyotaka hayupo tayari kuendelea na sisi.

Kama ambavyo mmeona tangazo lake ndivyo alivyo huwa hajibu wala kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu hoja.

Pamoja na kwamba uoga wako ndo umaskini wako ila kwa wawekezaji wa kibongo bora kuwa mwoga. "invest on your own risk"

Nawatakia wakati mwema.
 
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu, nimekutana sana na tangazo lao lakini imani yangu inagoma kuniunga mkono, haya mambo ya weka kiasi fulani upate mara 3 ya kiasi ulichoweka, huwa yananipita kushoto sijui ni uoga ama ni ujinga.!

Mwisho wa siku, yule mwenye maamuzi magumu ndiye atakayekula mema ya nchi.!!
 
Ahsante kwa ufafanuzi mkuu, nimekutana sana na tangazo lao lakini imani yangu inagoma kuniunga mkono, haya mambo ya weka kiasi fulani upate mara 3 ya kiasi ulichoweka, huwa yananipita kushoto sijui ni uoga ama ni ujinga.!

Mwisho wa siku, yule mwenye maamuzi magumu ndiye atakayekula mema ya nchi.!!
Maamuzi magumu yafanyike kwa umakini mkuu la sivyo unaweza jutia
 
Na Joti si ndo Balozi wake. Hivi hawa jamaa wa UHALIFU MITANDAONI WANAHUSIKA NA MATUSI TU? HUU UTAPELI UTAFUTIWE KITENGO KINGINE?

Nakumbuka mwaka 2006 USHIRIKA SACCOSS pale Lumumba walinipiga laki 4, na Mwenyekiti wetu alitupiga chenga mpaka tukanyosha kwapa hela ikakwenda hivyo na tangu siku hiyo aisee siwezi kuwekeza sehemu kirahisi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
65 Reactions
Reply
Back
Top Bottom