Fahamu vitu ambayo hutengeneza afya bora ya binadamu

Bwana Matunda

New Member
Jul 16, 2021
4
5
NI VITU GANI UTUMIKA KU-CREATE AFYA BORA KWA BINADAMU?

Ukitaka kupika maandazi basi utahitajika uwe na mahitaji(ingredients) kama unga,chumvi,sukari,baking powder,iriki,maji n.k
Sasa turudi kwenye afya, ukitaka kuwa na afya bora,Je unatakiwa uwe na mahitaji gani?
(What are those ingredients for health?)
.
1. Chakula(food)
Mtu ili awe na afya bora ni lazima apate chakula,tena sio chakula tu bali chakula kilicho fresh,halisi na chenye virutubisho bora. Mtu ukila vyakula ambavyo sio bora matokeo yake maradhi mengi asa yasio ya kuambukiza yatakupata,ivyo ni vyema kuhakikisha unakula chakula bora kulingana na mahitaji ya mwili wako.

2. Mwanga(Light)
Ili mtu uwe na afya bora unahitaji kupata mwanga. Hapa sizungumzii mwanga wa Kibatari,naongelea mwanga wa jua.

3. Hewa(Air)
Ili mtu uwe na afya bora ni lazima upate hewa,tena iliyo safi. Uchafuzi wa mazingira kutokana na shughuli za banadamu umekuwa kikwazo kwa watu wengi kutopata hewa safi na salama. Ila tambua kuwa ni muhimu kupata hewa safi na salama popote pale.

4. Maji(water)
Ili uwe na afya bora basi ni lazima upate maji safi na salama. Kuna msemo unasema "maji ni uhai" ivyo maji ni kitu muhimu kwa mtu yeyote yule.
Kwa siku tunashauriwa kunywa maji angalau glasi 8.

5. Unahitaji Kupata usingizi(kulala)
Bila kupata usingizi wa kutosha unaweza ukajiweka katika mazingira ya kuhatarisha afya yako. Usingizi ni jambo nzuri sana sababu uupa mwili uwezo wa kujitibu na kujiweka sana kutokana na shughuli zake ivyo ni muhimu kwa mtu yeyote yule kuweza kupata usingizi(kulala). Kwa kawaida tunatakiwa kulala angalau kwa masaa 7 hadi 8 kwa siku.

6. Unahitaji mazoezi yatakayo ushughulisha mwili.
Ili uwe na afya ni lazima mwili wako uwe 'active',unaweza fanya mazoezi kama kukimbia(jogging), kuendesha baiskeli,push-ups,kupanda milima na aina nyingine za mazoezi.

7. Unahitaji Ushirikiano na wengine(connection).
Ni lazima ushirikiane na wengine katika jamii unayoishi katika mambo mbalimbali. Ili uwe na afya bora hautakiwi kujitenga kama kisiwa.

8. Unahitaji upate upendo(love)
Ni lazima upate upendo kutoka kwa watu wanaokuzunguka,maana afya bora haiwezi kukamilika bila kupata upendo kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki.

Haya ndio mahitaji(ingredients) 8 ambayo uhitajika kwa mtu yeyote anayetaka kuwa na afya bora.
Ndimi Bwana Matunda
 
1626606958563.png

Haya ndiyo makazi ya 60% ya walipa miamala ya simu.
 
8. Unahitaji upate upendo(love)
Ni lazima upate upendo kutoka kwa watu wanaokuzunguka,maana afya bora haiwezi kukamilika bila kupata upendo kutoka kwa ndugu,jamaa na marafiki.


Hebu hapa ongezea nyama, ni upendo affections au Love ya mapenzi??🤣
 
Back
Top Bottom