Fahamu utofauti wa maumivu ayapatao mwanaume na mwanamke pale wanapogundua kuwa wanasalitiwa

LIKUD

JF-Expert Member
Dec 26, 2012
8,151
2,000
Wivu na maumivu anayoyasikia mwanamke pale anapohisi au kugundua kuwa mpenzi wake wa kiume anatembea nje ya mahusiano yao uko katika kiwango cha hisia "emotional level" wakati maumivu anayoyapata mwanaume kwa kusikia au kugundua kuwa mpenzi wake wa kike anamtu mwingine uko katika kiwango cha himaya "territorial level".

Wakati mwanamke anaumia kwa wivu akijiuliza kwanini mwanaume wangu achukuliwe na mwanamke mwingine, huku akiwa na kiu ya kumjua huyo mwanamke anafananaje? Ananini? Anauwezo gani kimvuto na kimuonekano? Maswali haya moyoni mwake huongeza maumivu katika hisia za mwanamke huyu, kwa upande wa pili mwanaume haumii hihisia lakini huumia na kupata machungu zaidi ya mwanamke huku moyoni mwake akihisi kushindwa kuimiliki himaya yake vema hadi mwanaume mwingine kuweza kuivamia, hujihisi kama askari aliye na silaha dhaifu au aliyeshindwa kutumia silaha zake vema hadi askari wa kambi nyingine akapata urahisi wa kumvamia tena kwenye kitovu cha kambi yake.

Katika hali hizi, mwanamke humtazama mwanaume wake kama mpenzi wakati mwanaume akimtazama mwanamke wake kama himaya. Ni ngumu sana mwanaume kustahimili maumivu ya jinsi hii, na ndio maana kwa wanaume wengine huwa rahisi hata kuwaza kujitoa uhai au kuutoa uhai wa huyo mwanaume mwingine aliyetembea na mpenzi wake, wapo pia wanaume ambao huishiwa nguvu za kufanya tendo la ndoa kwa muda fulani "temporary impotency"mara tu wanapogundua kusalitiwa, na nimeshuhudia mwanaume aliyeamua kuzikata sehemu zake zote za siri kwasababu ya kuona hazina tena umuhimu, ingawa hakuweza kuishi tena baadae.

Maumivu na matendo haya hayafanyiki sana kwa jinsia ya kike, wao huishia zaidi kulia, kupiga kelele sana, kutukana, na juhudi za kumsaka huyo mwanamke mwingine zikifanikiwa basi wanaweza kupigana kidogo na kuwekeana uadui wa kawaida, ambao sikumoja unaweza ukaisha - Chris Mauki.
 

Blue G

JF-Expert Member
Jun 20, 2012
5,213
2,000
labda ndio maana sio rahisi kwa wanaume kuwasamehe wapenzi wao wanapowasaliti eeeehhh?
 

Asnam

JF-Expert Member
Jan 18, 2012
4,258
1,225
timbwili la nn wakati muda wako umeisha,jikusanye ubebe vinavyokuhusu usepe,muda wa kumtafuta mke mwenza nautoa wapi maisha yenyewe mafupi haya.
 

miss chagga

JF-Expert Member
Jun 7, 2013
57,917
2,000
kumganda mtu alikuona hufai ya nini ... step out do other thing... world is full of enjoyment and a lot to do and to think about aiii
 

millcent5

Member
Dec 8, 2013
58
95
timbwili la nn wakati muda wako umeisha,jikusanye ubebe vinavyokuhusu usepe,muda wa kumtafuta mke mwenza nautoa wapi maisha yenyewe mafupi haya.

Mama utafungasha kila siku,c utamaliza mitaa,we ukizinguana tu unafungasha
 

MankaM

JF-Expert Member
Apr 20, 2013
9,456
1,500
timbwili la nn wakati muda wako umeisha,jikusanye ubebe vinavyokuhusu usepe,muda wa kumtafuta mke mwenza nautoa wapi maisha yenyewe mafupi haya.

hahahaaaaa afu unakuta mke mwenza kakuzidi parefu tu unabaki umetoa macho ya hatar
 

Ndege Tausi

JF-Expert Member
Nov 12, 2013
962
500
hahahaaaaa afu unakuta mke mwenza kakuzidi parefu tu unabaki umetoa macho ya hatar

Unadhani wanaume wanaangalia hicho unachofikiria wewe eti cha kukuzidi parefu, walaaa. Wanchoongalia wanaume wala wanawake hawawezi kukijua hata siku moja. Ndo maana unaweza kuta mchepuko wa mumeo ni polygon hata kukuzidi wewe, lkn mumeo ndo kafia hapo!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom