Fahamu utofauti uliopo Kati ya CCTV camera aina ya IP CCTV na Analogy CCTV

naomba brief kidogo ya gharama ya both,nahitaji kufunga moja wapo kwenye biashara yangu
VIFAA VINAVYOHITAJIKA

1. IP Camera(aka IP CCTV Cameras, Network Cameras, Digital Cameras, Security Cameras & Web Cameras)
  • IP Camera
  • NVR(Network Video Recorder)
  • Cat6 UTP Cable
  • Cat6 RJ Connectors
  • Surveillance HDD(Hard Disk Drive)
  • LED/LCD Monitor/Screen
2. Analog Camera
  • Analog Camera
  • DVR(Digital Video Recorder)
  • PSU(Power Supply Unit)
  • BNC Crimp Connectors
  • RG59+2C Cable
  • Surveillance HDD(Hard Disk Drive)
  • LED/LCD Monitor/Screen
FAIDA YA IP CAMERAS UKILINGANISHA NA ANALOG CAMERAS
  • Gharama za kuuhudumia mfumo zipo chini, hii ni kwasababu mfumo wa IP Camera hauna vifaa vingi ukilinganisha na mfumo wa analog, mfano, ukingalia hapo juu utaona idadi ya vifaa vinayotakiwa na mfumo wa IP Cameara ni chache.
  • Mfumo wa IP Camera hauhitaji waya nyingi ukilinganisha na mfumo wa analog, kwanini? kwenye mfumo wa IP, waya(cable) i.e in Cat5e/Cat6, unaotumika kuunganisha camera na NVR ni huohuo utakaobeba signal za video na power kwasababu NVR in mfumo wa switch uitwao PoE(Power over Ethernet) yaani camera inapata umeme kutoka kwenye switch moja kwa moja bila kuhitaji chanzo kingine cha umeme kama ilivyo kwenye mfumo wa analog, ambao utahitaji PSU na cable mbili kwa ajili ya signal ya video na power.
  • IP Camera zina ubora wa juu wa video
  • Unaweza kutumia IP Cameras pekee kwenye nyumba/au sehemu ya biashara kuliko bila kuwa na NVR, kwasababu zipo IP Camera ambazo zina uwezo wa kuhifadhi recorded footage kweye built-in microSD card slot hadi 256GB, hii ni tofauti na mfumo wa analog ambao ni lazima uwe au utumie DVR.
Faida za IP ni nyingi sana, hizo ni baadhi tu.

GHARAMA

  1. IP Camera System - Makadirio ya kamera nne za 2MP ni TZS 1,200,00 hadi 1,500,000
  2. Analog Camera System - Makadirio ya kamera nne za 2MP ni TZS 1,100,000 hadi 1,300,000
Gharama hutegemea na Idadi ya camera pamoja resolution/Megapixels za kamera zitakazotumika kwenye mfumo.
Kwasasa kuna IP camera zenye hadi 30megapixels, ila kwa soko letu nimeona za hadi 12MP.

Ni hayo tu kwa uchache.
 
TOFAUTI KATI YA IP CAMERA NA ANALOGY CAMERA

ANALOGY CCTV CAMERA

CCTV kirefu chake ni Closed-Circuit Television,Ni mfumo wa kukusanya taarifa za picha za video katika eneo Fulani kwa kutumia camera za video katika Idadi flani.

View attachment 1688940

Kwa kawaida taarifa hizi za picha za CCTV ambayo Ni analogy huenda kuhifadhi katika kifaa kinacho itwa Digital Video Recorders (DVRs).

Muda wa kuhifadhi na size ya taarifa kukusanywa itategemeana na size ya storage iliyopo.

CCTV camera kwa ujumla zile za analogy na digital kwa Sasa zimeongezewa teknolojia ya kutambua kitu kinacho jongea (motion detector),na pia zimepewa uwezo wa kupiga alarm au kutuma ujumbe katika email au ujumbe mfupi (sms),pale zinapo hisi Kuna kitu kinajongea au kusogelea eneo husika.

CCTV camera za analogy,techolojia yake ni ya muda kidogo,camera hizi huweza kuona picha za rangi kwa mchana na huona picha ya black and white usiku,ila zipo za bei rahisi zaidi ambazo huweza kuonesha picha ambazo Ni black and white muda wote yaani usiku na mchana.

JINSI CCTV CAMERA AMBAYO NI ANALOGY INAVYOFANYA KAZI

CCTV camera ya analogy,hurecord taarifa za video katika mfumo wa analogy,nakuzipeleka taarifa hizo katika kifaa kinachoitwa (DRV),kwa ajili ya kugeuzwa kuwa katika mfumo wa kidigitali ili DVR iweze kuitunza taarifa hiyo kwa matumizi zaidi.

View attachment 1688941

FAIDA ZA ANALOGY CCTV CAMERA

1.Ni bei rahisi kuinunua
2.Inasaidia kupata taarifa ya matukio kwa mfumo wa video
3.Unaweza kufatilia matukio yanayotokea eneo lako ukiwa,popote Duniani.
4.Rahisi kuunganisha

HASARA ZA CCTV ANALOG CAMERA

1.Inachukua video eneo dogo KULINGANISHA na IP camera.
2.Inatumia DVR,hivyo inatakiwa uunge Idadi ya camera kulingana na Idadi ya port za camera katika DVR.
3.Inatumia cable na vifaa vingi kuunganisha.
4.Picha yake Ni ya pixel ndogo ukilinganisha na IP camera.

DIGITAL CCTV CANERA/ IP CAMERAs

Internet Protocal Camera (IP Camera),Ni camera za mfumo wa kidigitali katika teknolojia ya CCTV,Ni kamera ambazo hutumika katika ulinzi na usalama,au ukusanyaji wa taarifa za video.

View attachment 1688946

Lakini tofauti na CCTV za analogy, camera hizi hupokea taarifa na kuzitafsiri katika mfumo wa kidigitali zenyewe na kuzituma moja kwa moja katika IP network,hii ikiwa na maana haitegemei local recordingdevice(DVRs),kugeuza taarifa yake kwenda digitali.

Camera za IP huhitaji uwepo wa Local Network au internet katika eneo husika kwa ajili ya usafirishaji wa taarifa hizo,katika vifaa vya kutunzia au kutizamia picha,iwe computer,TV,au Smartphone,pia network hii husaidia katika kuzifikia taarifa za camera katika kuweza kuiratibu.

Kuna IP camera ambazo huhitaji pia msaada wa kifaa kinachoitwa Network Video Recorder (NVR),kuweza kusimamia utunzaji wa kumbukumbu za picha za video na kuratibu alarm.

Ila nyingine hazihitaji NVR,sababu zinaweza kurecord zenyewe kwa storage zake au kuweza kutuma taarifa ya video za picha katika storage iliyo mbali.

IP CAMERA INAVYOFANYA KAZI.

IP camera hukamata picha,na kuzipunguza ukubwa wake bila kuharibu ubora na kuzisafirisha taarifa hizo katika mifumo ya network iliyoungwa nayo Kama vile Wi-Fi router, Ethernet,au broadband modem.

View attachment 1688947

FAIDA YA IP CAMERA KULINGANISHA NA CCTV CAMERA.

1.Zina picha yenye mwonekano mzuri zaidi,yaani Ina pixel kubwa,ambayo inakuwezesha kuona details ndogo ndogo,mfano plate namba za gari n.k

2.Haihitaji waya nyingi katika kuunganisha (installation),inaungwa kwa kutumia Ethernet cable,ambyo pia huipa nishati moja kwa moja,hivyo haihitaji waya ya power supply.

3.Unaweza kuifunga kwa muda au moja kwa moja

4.Inaruhusu mfumo wa kutanua picha (zooming bila kuharibu ubora wa picha).

5.Nirahisi kuziratibu ukiwa popote Duniani,ilimradi kuwe na uwepo wa internet.

6.Haihitaji vifaa vingi kuifunga.

7.Inachukua picha katika eneo kubwa Mara Tatu ya analogy camera.

8.Unaweza kuzifunga nyingi bila kizuizi Cha ports,ambacho kipo katika analogy CCTV camera.

HASARA ZA IP CAMERA

1.Ni gharama kuinunua
Ip Camera zipo poa👍
 
Linda Ofisi yako, Nyumba yako na Hata mifugo yako kwa Teknolojia za kisasa.

Kwa Tsh. 22,000/ unapata complete Electric Fence kwa Meter.

Tsh. 800,000/ unapata Full Set ya 4 CCTV Camera.

Tsh. 1,520,000/ unapata Full Set ya Auto Gate Motor.

Tsh. 500,000/ unapata Full Set ya Door Bell Video Intercom.

Tsh. 1,200,000/ unapata complete Licenced Time & Attendance System.

Tsh. 1,200,000/ unapata complete Door Access Control System.
.
Instagram:: Mr Security System

Mawasiliano:: +255757363601
______________+255657496629
 
16 Reactions
Reply
Back
Top Bottom