Fahamu utajiri wa kudumu uliojificha kwenye zao la Parachichi Mkoani Njombe

Ahsante kwa kuomba ufafanuzu wa kitaalam @ mkuu Majan. Baada ya mbolea kufika shambani Ni vema ikakaa pembeni kwa muda usiopungua wiki tatu hadi nne ili kuifanya ipoe isije kuunguza Miche ya mazao. Baada ya muda huo kupita Sasa unaweza kuendelea na hatua ya kuchanganya mbolea na udongo Kisha kupanda miche yako kwenye mashimo
Nashukuru kwa jibu murua mkuu AGRIWORTH TZ ubarikiwe sana
 
Ahsante kwa kuomba ufafanuzu wa kitaalam @ mkuu Majan. Baada ya mbolea kufika shambani Ni vema ikakaa pembeni kwa muda usiopungua wiki tatu hadi nne ili kuifanya ipoe isije kuunguza Miche ya mazao. Baada ya muda huo kupita Sasa unaweza kuendelea na hatua ya kuchanganya mbolea na udongo Kisha kupanda miche yako kwenye mashimo
Hujajibu swala la maji na madawa
 
Naona swali langu limekwepwa,

Nauliza kama mnayo mashamba ya kuuza, mnao utaalamu wa kulima na mnalo soko.

Why msilime nyinyi hayo mashamba mkapata mavuno muuze kwenye hayo masoko?
 
Habari janvini
Kama Bado hujasajiri kampuni.
Karibu ntakusajiria kwa chapu. Bei nzuri kabisa.
Pia huduma ya
- kuandaa mahesabu ya kodi
-mchanganuo wa Biashara
- kusaidia kupata leseni ya biashara
Ushauri bure
Karibuni nyote


FB_IMG_1577116568496.jpeg
 
Mimi sijaelewa hapa,
Nyinyi mnatuambia tukitaka kununua Shamba ni 150,000/-.

Nyinyi mnao utaalamu wa kulima hayo Maparachichi,

Nyinyi mnalo soko la Maparachichi.

Sasa kwanini hayo mashamba msilime wenyewe mkapata hayo Maparachichi mkauza kwenye hilo soko la nje mlilonalo? Na hiki kilimo mnakijua vilivyo nje ndani.


Habari yako mkuu @ Shark. Ni kweli mashamba yapo, wataalam tunao na soko tunalo.
Katika ufanyaji wa majukumu Kuna kitu kinaitwa 'Division of labour'. Sisi majukumu yetu
Ni hayo Kama kampuni.
 
hujajibu swala la maji na madawa


Karibu Tena mkuu @ Danpol. Ufafanuzi kuhusu matumizi ya maji kwenye zao la parachichi
Ni kitu ambacho hakiepukiki. . Ndio maana tunatoa ushauri kuwa upandaji wake ufanyike
msimu wa mvua ili kupunguza gharama na muda wa kumwagilia. Pia madawa ya kuzuia uharibifu
wa miche na matunda yake hupatikana kwenye maduka ya madawa ya kilimo. Gharama juu ya maji na madawa
hutegemea ukubwa wa Shamba, aina ya ugonjwa ambao umeshambulia Miche na Matunda yake, teknolojia itumikayo( ya kisasa au zamani) katika umwagiliaji Pamoja na umbali kilipo chanzo Cha maji na shamba lilipo.
 
Pia katika parachichi nimesikia kuwa kuna hawa nyuki wadogo ambao hawana madhara mara nyingi inashauriwa wafugwe katika miparachichi.
 
Habari ya majukumu wakuu. Niende moja kwa moja kwenye mada tajwa hapo juu.

Maparachichi ni matunda bustanini na mashambani. Maparachichi yana matumizi mengi yenye faida kubwa kwa wakulima na wadau wengine.

Maparachichi ni chakula chenye viini lishe bora kama vitamini {A, B2, C, D, E, K} na madini {P, K,Mn, S} ambavyolinda mwili , mafuta kwa wingi asilimia 5 mpaka 30ambayo huleta joto mwilini, protin asilimia 1 mpaka 5ambayo hujenga mwili na kiasi cha colories 250 ambayo huleta nguvu mwilini.

Tofauti na matunda mengine, maparachichi ni malighafi ya viwandani kutengenezea madawa ya ngozi pamoja na vipodozi mfano mafuta ya nywele, shampoo na sabuni. Vilevile majani yake na mbegu hutumika kama dawa.

Aina bora za parachichi ambazo zimefanyiwa utafditi na kukubalika kwa wakulima na walaji ni pamoja na HASS, FUERTE, WEISAL IKULU, MWAIKOKESYA, EX TENGERU NA NABALI. Aina hizi zinazaa matunda mengi na bora pia huchukua muda mfupi kukomaa . kiasi chs matunda kwa mti ni klati ya 300 hadi 800 kutegemeana na matunda

Njia bora ya kuzalisha miche ya maparachichini kwa njia ya vikonyo. Faida zinazotokaana na njia hii ni

Miti kuchukua muda mfupi kukomaa na kuzaa matunda {miaka 3}
Miti huwa na umbo na urefu wa wastani
Kuepusha magonjwa hasa virus
Miche mingi kuzalishwa kwa wakati mmoja

HATUA ZA KUFUATA KABLA YA KUZALISHA MICHE KWA NJIA YA VIKONYO
1. Kuzalisha miche ya kubebeshea vikonyo kutokana na mbegu
2. Kubebesha vikonyo kwenye miche. Vifaa vinavyohitajika ni mifuko ya plastiki yenye kipenyo cha 5 -6 na urefu wa 5-6, udongo safi usio na magonjwa hasa wa msituni, samadi, mchanga/pumba za mchele kwa uwiano wa 3;1;1, mbolea ya TSP
3. Andaa kitalu sehemu wazi na tengeneza kichanja ili kuzuia jua na mvua
4. Changanya udongo na jaza kwenye viliba
5. Panda mbegu kwenye viliba
6. Uwagilia maji
7. Baada ya wiki 2-3 mbegu zitaanza kuota
8. Tunza miche hadi kufikia umri wa kubebeshwa miezi 3-4 au unene wa penseli. ZINGATIA ukuaji wa miche hutegemea hali ya hewa

JINSI YA KUBEBESHA VIKONYO
Ni muhimu kuchagua tawi zuri kwenye mti uliokomaa na kuzaa matunda ili kuharakisha kukomaana kuzaa matunda kwa mti uliobebeshwa, usichsgue kikonyo chenye maua, kikonyo kikianza kuchipua hakifai kwa kubebesha kwa sababu ni kichanga.
miche inayobebeshwa itoke kwenye jamii moja
  • Urefu wa kikonyo uwe sm 15-20 na chonga kikonyo bapa sm 2-3
  • Mche wa kubebeshea kikonyo ukatwe juu kwenye shina sm 20-25kutoka usawa wa udongo na kata kipenyo cha sm 2-3
  • Urefu wa kikonyo ulingane na urefu wa bapa la kikonyo
  • Sehemu ya mmea yenye mirija ya kupitisha chakula na maji zihakikishwe zinaungana
  • Fungia vizuri kikonyo kwenye shina na mkanda [strip] wa nailoni nyeupe. Tendo hili lifanyike kwenye mazingirea safina haraka ili utomvu kwenye bapa na kipenyo usikauke
  • Funika mche na mfuko wa nailoni nyeupe inayopitisha mwanga mradi isiwe nyeusi
Baada ya wiki 2-3 vikonyo vilivyopona vitaanza kuchipua. Tunza miche ya kitaluni kwa kumwagilia maji na kuondoa machipukizi'

UCHIMBAJI WA MASHIMO
Pima nafasi za kupanda ambazo ni 6m kwa 5m, 6m kwa 6m au 6m kwa 8m. Tenganisha udongo wa wa chini na wa juu. Changanya udongo wa juu na samadi. Rudisha udongon wa juu kwenye shimo. Weka kijiti katikati ya shimo. Rudisha udongo wa chini. Panda miche wakati wa masika. Chagua miche yenye afya nzuri. Fungua mikanda ya nailoni iliyounganisha shimo nsa kikonyo wiki 2-3 baada ya kupanda mche

SHUGHULI NYINGINE MUHIMU NI:
Palizi, kumwagilia maji, kuondoa machipukizi na kuzuia magonjwa na wadudu

MAVUNO YA PARACHICHI NA FAIDA YAKE
Mche mmoja wa parachichi aina ya HASS huanza kwa kutoa kg 40 mpaka kg 60 kwa mavuno yake kwa msimu wa kwanza. Bei ya soko kwa sasa KAMPUNI YA AGRIWORTH TANZANIA tununua kutoka kwa mkulima shambani tsh 1500 KWA KG 1. Hivyo 1500 zidisha kwa kg 40 =60000 kwa mche mmoja kwa kadirio la chini

Ekari moja hupandwa miche 70. MICHE 70 zidisha kwa 60000= 4200000.
Soko la parachini ni kubwa sana duniani kwa sasa.

Miche hii hudumu zaidi ya miaka 50 ya mavuno yake shambani

KWA MAHITAJI YA SHAMBA ZA KILIMO CHA PARACHICHI MKOA WA NJOMBE
Bei ya shamba ni tsh 150,000= kwa ekari moja mkoano Njombe. Ofisi zetu zipo mkoani Njombe. Pia tunatoa huduma ya usimamizi wa shamba mpaka kipindi cha mavuno kwa walio tayari kusimamiwa shughuli zao na kampuni
Mkuu weka namba za simu tufanye mawasiliano.
 

Similar Discussions

22 Reactions
Reply
Back
Top Bottom