billtheKID
Member
- May 6, 2017
- 33
- 176
Hii ni tangazo la auction,limeonesha na kiasi cha pesa BOT inazohitaji ukiangalia hapo kwenye competitive na non-competitive then maelezo mengine yanaeleweka.
Sent using Jamii Forums mobile app

Boss ukiuliza humu tutawasaidia na wengine pia tunaweza pata michango ya wazoefu.
Mkuu hisa hutolewa na kampuni, Serikali hutoa T bills na Bonds tu.Lakini hii yote ni uwoga wa kuthubutu tu.
Yaani wataka sema umeshindwa kuinvest mpaka ukanunue hisa Katika taasisi za Serikali????
Yatupasa kuwa na fikra pana zaidi katika kujifunza nidhamu na pesa.
Sent using Jamii Forums mobile app
We uliye invest umefaidika vipi !?Lakini hii yote ni uwoga wa kuthubutu tu.
Yaani wataka sema umeshindwa kuinvest mpaka ukanunue hisa Katika taasisi za Serikali????
Yatupasa kuwa na fikra pana zaidi katika kujifunza nidhamu na pesa.
Sent using Jamii Forums mobile app
Hivi kuinvest ni nini? Maana mi najua ni kuweka pesa/resource yoyote mahali ikazalisha na kununua hisa/bonds ni investment pia.Lakini hii yote ni uwoga wa kuthubutu tu.
Yaani wataka sema umeshindwa kuinvest mpaka ukanunue hisa Katika taasisi za Serikali????
Yatupasa kuwa na fikra pana zaidi katika kujifunza nidhamu na pesa.
Sent using Jamii Forums mobile app
True!Hivi kuinvest ni nini? Maana mi najua ni kuweka pesa/resource yoyote mahali ikazalisha na kununua hisa/bonds ni investment pia.
Noted,& thxUTAJIRI MKUBWA ULIOPO KWENYE UWEKEZAJI WA DHAMANA ZA SERIKALI
Uwekezaji kwenye dhamana za serikali umegawanyika makundi mawili.
i) Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
ii) Dhamana za muda mrefu (treasury bonds)
Kwa nchi yetu ya Tanzania biashara ya dhamana za serikali inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa niaba ya serikali ya Tanzania.
Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
Hizi ni dhamana za muda mfupi ikimaanisha zinaiva ndani ya mwaka mmoja. Lengo kubwa hasa kwa serikali kuweka Treasury bills ni kupata fedha kwa ajili kukabiliana na mapungufu ya fedha katika bajeti na pale inapohitaji fedha kwa haraka.
Dhamana za muda mfupi zipo katika makundi manne kutegemea na mda zitakapoiva: ya siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.
Uwekezaji katika Treasury bill una faida zifuatazo kwa mwekezaji;
i)Hazina hatari yoyote kubwa (risk free) kwa mwekezaji na ni uwekezaji wa uhakika kwa sababu zinatolewa na serikali.
ii)Zaweza kuhamishika kutoka umiliki wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Ikimaanisha pale mwekezaji anapotaka kuuza anaweza akafanya hivo.
iii)Zaweza kutumika kama dhamana za kuombea mikopo kwenye taasisi za fedha bila usumbufu wowote kwa sababu thamani ya treasury bill coupon haibadiliki kwa hiyo ni rahisi kwa taasisi za fedha kuzipa kipaumbele kutumika kwenye dhamana.
iv)Gawio ni kubwa pale unapowekeza kwenye treasury bills zaidi hata ya kuwekeza kwenye taasis yeyote ya fedha kupitia fixed deposits. (namaana ya kwamba riba katika treasury bills ni kubwa maradufu ya riba za benki)
Soko la treasury bills
Biashara na soko la treasury bills zinafanyika kwa njia mbili;
a) Soko la awali (primary market) hapa ni pale banki kuu ya Tanzania inapotoa kwa mara ya kwanza treasury bills kwa wawekezaji.
b) Soko la pili (secondary market) hii inahusisha kuuza na kununua treasury bills na hii inafanyika Dar es salaam stock exchange DSE. Hapa ndipo pale mtu anapotaka kuuza treasury bills anayoimiliki anaweza kwenda kuuza.
Kianzio cha kuwa mwekezaji wa moja kwa moja kwenye treasury bills kwa Tanzania ni sh. 5,000,000. Ina maana kwamba ukiwa na mtaji wa kuanzia milioni tano basi unaruhusiwa moja kwa moja kushiriki kwenye mnada wa treasury bills (treasury bills auction).
Kwa wawekezaji wa mtaji chini ya milioni tano basi wao watashiriki kwenye mnada kupitia primary dealers ambao kwa urahisi ni mabrokers na commercial banks
Primary dealers ambao wamethibitishwa na BOT ni hawa wafuatao (ambao wale wenye mitaji chini ya milioni tano watapitia kwao) Akiba Commercial Bank Ltd, Citibank (T) Ltd, CRDB Bank Ltd, Diamond Trust Bank (T) Ltd, Eurafrican Bank (T) Ltd.Exim Bank (T) Ltd. Habib African Bank Ltd. International Commercial Bank (T) Ltd. Kenya Commercial Bank (T) Ltd.NBC Limited. NMB Ltd. Stanbic Bank (T) Limited Standard Chartered Bank Ltd.Orbit Securities Co. Ltd. Rasilimali Limited Solomoni Securities Ltd. Core securities Ltd. Tanzania securities Ltd. Vertex International Securities.
Unapata vipi pesa kupitia dhamana za muda mfupi?
Serikali kupitia BOT inapotoa treasury bills zinakuwa katika mfumo wa zabuni ikimaanisha kwamba wawekezaji watatakiwa kwa mfano kusema watanunua kila shilingi 100 ya serikali kwa kiasi gani? (hatua hiyo ya kwanza inaitwa bidding)
Ili kupata faida kwa wawekezaji wanatakiwa kutoa bei ambayo ipo katika discout, ikiwa na maana mwekezaji anaweza kununua shilingi 100 ya serikali kwa shilingi 93 hivo mda wa kuiva ukifika atapata faida ya shilingi 7.
Mfano serikali imetoa treasury bills ya siku 365. Kisha mwekezaji akaweka bid ya kununua kila shilingi 100 kwa shilingi 75. Kama mwekezaji atafanikiwa kwenye zabuni hiyo atapata treasury bill yenye (face value) ya Tzs 100,000,000 ingawaje kiasi alichotoa ni Tzs 75,000,000 kwa sababu ndicho kiasi alicho bid katika kabrasha la zabuni yake.
Baada ya treasury bills kuiva yaani kutimia siku 365, mwekezaji atalipwa na BOT kiasi cha TZS 100,000,000 ambayo italeta faida ya (TZS 100,000,000-TZS 75,000,000= TZS 25,000,000). Hivo faida itakuwa ni TZS 25,000,000.
Ukiweka katika asilimia ni kama ifuatavyo;
- Kanuni ya kukokotoa riba katika treasury bills:
Riba=(F-P)/P ×(365×100)/N
F= face value ya treasury bills ambayo ni 100
P= bidding price ambayo ni 75 kama mfano unavosema
N= idadi ya siku treasury bills itapoiva mfano wetu ni siku 365
Riba= (100-75)/75 ×(365×100)/365
=0.3333×100
Riba = 33.33%
Ikiwa na maana kwa pesa ambayo utatoa kununua treasusry bills utapata gawio la asilimia 33.33% ndani ya siku 365 yaani mwaka mmoja tu.
Piga mahesabu kama umewekeza milioni 100 ambazo huna matumizi nazo ina maana baada ya siku 365 utakuwa na faida ya kama milioni 30 ambazo hata kujazitolea jasho.
Nataka pia kuwamegea siri kwamba mabenki ya kibiashara na wafanyabiashara wakubwa ndio wamekuwa wakitajirikia hapa kwani wao wanawekeza kuanzia bilioni na kwenda juu. Kwa hiyo unaweza kufikiri ni pesa kiasi gani wanatengeneza.
Kuna watanzania wengi sana wana mamilioni ya pension benki hizi ndizo fursa za kuchangamkia ambazo huwezi kuzisikia zikitangazwa kwa maana ndipo pesa ilipo.
Kama hujaelewa waweza acha comment yako hapa then ntakujibu..
Yes ni good investment na sababu ina very low risk lakini usisahau kuwaambia JF hiyo faida ina TAX na inflation ya TZ inafanya hii biashara kuwa unpredictable na nimesikia corruption in bidding process is rampant big cats wana insider information ambazo zinawaweka in advantage na minimum bidding amount ni kubwa sana kwa watanzania wengi kuingia kwenye hili soko, ila all in all ni good business kama una enough fund na uombe mungu inflation isile faida yako lakini is not a slam dunkUTAJIRI MKUBWA ULIOPO KWENYE UWEKEZAJI WA DHAMANA ZA SERIKALI
Uwekezaji kwenye dhamana za serikali umegawanyika makundi mawili.
i) Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
ii) Dhamana za muda mrefu (treasury bonds)
Kwa nchi yetu ya Tanzania biashara ya dhamana za serikali inasimamiwa na Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa niaba ya serikali ya Tanzania.
Dhamana za muda mfupi (treasury bills)
Hizi ni dhamana za muda mfupi ikimaanisha zinaiva ndani ya mwaka mmoja. Lengo kubwa hasa kwa serikali kuweka Treasury bills ni kupata fedha kwa ajili kukabiliana na mapungufu ya fedha katika bajeti na pale inapohitaji fedha kwa haraka.
Dhamana za muda mfupi zipo katika makundi manne kutegemea na mda zitakapoiva: ya siku 35, siku 91, siku 182 na siku 364.
Uwekezaji katika Treasury bill una faida zifuatazo kwa mwekezaji;
i)Hazina hatari yoyote kubwa (risk free) kwa mwekezaji na ni uwekezaji wa uhakika kwa sababu zinatolewa na serikali.
ii)Zaweza kuhamishika kutoka umiliki wa mtu mmoja kwenda kwa mwingine. Ikimaanisha pale mwekezaji anapotaka kuuza anaweza akafanya hivo.
iii)Zaweza kutumika kama dhamana za kuombea mikopo kwenye taasisi za fedha bila usumbufu wowote kwa sababu thamani ya treasury bill coupon haibadiliki kwa hiyo ni rahisi kwa taasisi za fedha kuzipa kipaumbele kutumika kwenye dhamana.
iv)Gawio ni kubwa pale unapowekeza kwenye treasury bills zaidi hata ya kuwekeza kwenye taasis yeyote ya fedha kupitia fixed deposits. (namaana ya kwamba riba katika treasury bills ni kubwa maradufu ya riba za benki)
Soko la treasury bills
Biashara na soko la treasury bills zinafanyika kwa njia mbili;
a) Soko la awali (primary market) hapa ni pale banki kuu ya Tanzania inapotoa kwa mara ya kwanza treasury bills kwa wawekezaji.
b) Soko la pili (secondary market) hii inahusisha kuuza na kununua treasury bills na hii inafanyika Dar es salaam stock exchange DSE. Hapa ndipo pale mtu anapotaka kuuza treasury bills anayoimiliki anaweza kwenda kuuza.
Kianzio cha kuwa mwekezaji wa moja kwa moja kwenye treasury bills kwa Tanzania ni sh. 5,000,000. Ina maana kwamba ukiwa na mtaji wa kuanzia milioni tano basi unaruhusiwa moja kwa moja kushiriki kwenye mnada wa treasury bills (treasury bills auction).
Kwa wawekezaji wa mtaji chini ya milioni tano basi wao watashiriki kwenye mnada kupitia primary dealers ambao kwa urahisi ni mabrokers na commercial banks
Primary dealers ambao wamethibitishwa na BOT ni hawa wafuatao (ambao wale wenye mitaji chini ya milioni tano watapitia kwao) Akiba Commercial Bank Ltd, Citibank (T) Ltd, CRDB Bank Ltd, Diamond Trust Bank (T) Ltd, Eurafrican Bank (T) Ltd.Exim Bank (T) Ltd. Habib African Bank Ltd. International Commercial Bank (T) Ltd. Kenya Commercial Bank (T) Ltd.NBC Limited. NMB Ltd. Stanbic Bank (T) Limited Standard Chartered Bank Ltd.Orbit Securities Co. Ltd. Rasilimali Limited Solomoni Securities Ltd. Core securities Ltd. Tanzania securities Ltd. Vertex International Securities.
Unapata vipi pesa kupitia dhamana za muda mfupi?
Serikali kupitia BOT inapotoa treasury bills zinakuwa katika mfumo wa zabuni ikimaanisha kwamba wawekezaji watatakiwa kwa mfano kusema watanunua kila shilingi 100 ya serikali kwa kiasi gani? (hatua hiyo ya kwanza inaitwa bidding)
Ili kupata faida kwa wawekezaji wanatakiwa kutoa bei ambayo ipo katika discout, ikiwa na maana mwekezaji anaweza kununua shilingi 100 ya serikali kwa shilingi 93 hivo mda wa kuiva ukifika atapata faida ya shilingi 7.
Mfano serikali imetoa treasury bills ya siku 365. Kisha mwekezaji akaweka bid ya kununua kila shilingi 100 kwa shilingi 75. Kama mwekezaji atafanikiwa kwenye zabuni hiyo atapata treasury bill yenye (face value) ya Tzs 100,000,000 ingawaje kiasi alichotoa ni Tzs 75,000,000 kwa sababu ndicho kiasi alicho bid katika kabrasha la zabuni yake.
Baada ya treasury bills kuiva yaani kutimia siku 365, mwekezaji atalipwa na BOT kiasi cha TZS 100,000,000 ambayo italeta faida ya (TZS 100,000,000-TZS 75,000,000= TZS 25,000,000). Hivo faida itakuwa ni TZS 25,000,000.
Ukiweka katika asilimia ni kama ifuatavyo;
- Kanuni ya kukokotoa riba katika treasury bills:
Riba=(F-P)/P ×(365×100)/N
F= face value ya treasury bills ambayo ni 100
P= bidding price ambayo ni 75 kama mfano unavosema
N= idadi ya siku treasury bills itapoiva mfano wetu ni siku 365
Riba= (100-75)/75 ×(365×100)/365
=0.3333×100
Riba = 33.33%
Ikiwa na maana kwa pesa ambayo utatoa kununua treasusry bills utapata gawio la asilimia 33.33% ndani ya siku 365 yaani mwaka mmoja tu.
Piga mahesabu kama umewekeza milioni 100 ambazo huna matumizi nazo ina maana baada ya siku 365 utakuwa na faida ya kama milioni 30 ambazo hata kujazitolea jasho.
Nataka pia kuwamegea siri kwamba mabenki ya kibiashara na wafanyabiashara wakubwa ndio wamekuwa wakitajirikia hapa kwani wao wanawekeza kuanzia bilioni na kwenda juu. Kwa hiyo unaweza kufikiri ni pesa kiasi gani wanatengeneza.
Kuna watanzania wengi sana wana mamilioni ya pension benki hizi ndizo fursa za kuchangamkia ambazo huwezi kuzisikia zikitangazwa kwa maana ndipo pesa ilipo.
Kama hujaelewa waweza acha comment yako hapa then ntakujibu..
Huo mfano wako hapo realistiki, Nimehisi Mimi hainihusu kabisa, Ungetoa MTU mwenye laki moja au tano hapo ndipo tupo wengi, M 100 huyo utakuwa unamzungumzia Mengi,Manji n.k
Kuna post ni kama ulisema investment kwenye treasury bond beyond five years haina kodi, je ni sahihi? Na endapo nimeamua kuwekeza kwa miaka 15 je wanaweza kunipa faida kwa mwezi au miezi mitatu nikitaka au nitakuwa nasubiri mpaka mwisho wa mwaka? Nimejaribu kupiga kwa milioni mia mbili ikiwekezwa kwa miaka 15 maana yake kila mwaka itakuwa na faida ya 27,000,000. Sijui kama mahesabu yangu yako sahihi? Na kama yako sahihi swali langu la pili ni kuwa je wanaweza kunipa 2,250,000 kila mwezi kama faida yangu?For those who interested,treasury bond issuance calendar ya mwaka huu wa fedha.
Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu kwa io pesa uko sahihi kwa upande wa interest ila kumbuka kuna faida umeiacha ya discount baada ya bid price yako kuwa successful kwenye mnada,,kwa upande wa malipo sheria znasema utalipwa kila baada ya six months hapo utalipwa half ya 27m six months apart boss!..Kuna post ni kama ulisema investment kwenye treasury bond beyond five years haina kodi, je ni sahihi? Na endapo nimeamua kuwekeza kwa miaka 15 je wanaweza kunipa faida kwa mwezi au miezi mitatu nikitaka au nitakuwa nasubiri mpaka mwisho wa mwaka? Nimejaribu kupiga kwa milioni mia mbili ikiwekezwa kwa miaka 15 maana yake kila mwaka itakuwa na faida ya 27,000,000. Sijui kama mahesabu yangu yako sahihi? Na kama yako sahihi swali langu la pili ni kuwa je wanaweza kunipa 2,250,000 kila mwezi kama faida yangu?
Kafie mbele na dini yako.
Kushiriki T bills na bond kuna soko la kwanza na la upili.
1.Soko la kwanza ni kupitia primary dealers(commercial banks na brokers) hawa kazi yao ni kukufungulia CDS(central depository system) account kukusaidia kuhajaza bid application form ili uweze kushiriki kwenye auction/mnada ambao hufanywa electronically na hapa hakuna bias bid price yako ndo itakufanya ushinde au ushindwe labda ufanye non-competitive bidding.Sasa ikitokea umeshinda hawa dealers utawalipa service charges tu 30000/= na ukishindwa hauwalipi chochote.
2.Soko la upili ni endapo ushafanya uwekezaji then unazitaji pesa zako au kama ulichelewa mnada unaenda DSE kununua au kuuza.
Huu ni uwekezaji ambao ni risk free utegemee faida.Hii ni tofauti na uwekezaji katika hisa ambapo ww unakuwa mmiliki wa kampuni kwa % flani faida na hasara zinakuhusu.
Sent using Jamii Forums mobile app
Yes ni good investment na sababu ina very low risk lakini usisahau kuwaambia JF hiyo faida ina TAX na inflation ya TZ inafanya hii biashara kuwa unpredictable na nimesikia corruption in bidding process is rampant big cats wana insider information ambazo zinawaweka in advantage na minimum bidding amount ni kubwa sana kwa watanzania wengi kuingia kwenye hili soko, ila all in all ni good business kama una enough fund na uombe mungu inflation isile faida yako lakini is not a slam dunk