Fahamu upande wa pili wa Dangote

Mondoros

JF-Expert Member
Aug 29, 2015
629
472
Dangote labda abadilike ndio tutaweza kufaidi uwepo wake hapa Tanzania, ila kwa jinsi alivyo na ninavyomfahamu..kwa sasa kuondoka kwake ni nafuu kwa Watanzania na Taifa.

Yule bwana hawezi kufanya biashara bila utapeli hata mfanyakazi wake wa chini kabisa anajua. Jamaa anaingia mahali kwa lugha tamu sana na ahadi kibao, lakini si mtu yule.

Wapo wanaosema kuhusu ajira za watanzania walioko pale, ni hivi wafanyakazi wataalamu walioko pale ni wale waliokuwa kwenye viwanda vingine vya cement vilivyokuwa vinawalipa vizuri ila baada ya kusikia tishio la ujio wa likiwanda kubwa ambalo lingepewa gas, exemption ya kodi n.k likapunguza bei ya cement viwanda hivyo vingekufa kwa kushindwa kujiendesha,

Hatua mojawapo zilizochukuliwa na viwanda bora kama vile Twiga na vingine ni kupunguza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa ambao wengi walienda Dangote kulipwa ujira mdogo sana maana yeye Dangote anatumia management ya Wahindi.

Kule Nigeria alianza biashara zake kwa style ya kuwahonga viongozi wakuu na wakampa excemption ya kodi, matumizi ya barabara hovyo na vitu vingine akashusha bei ya Cement, viwanda vingine vikafa akabaki yeye mwenyewe akishikilia kama 90% ya soko la cement na Lafarge kama chini ya 10% vingine vilikufa baada ya kuhakikisha kwamba ameviua akapandisha bei ikarudi kama zamani.

Hivyo ndivyo alitaka kufanya Tanzania, JK alimpa maeneo makubwa sana, mpaka na eneo la kujenga bandari yake binafsi, jambo ambalo kwa maoni yangu naona ilikuwa hatari hata kwa usalama wa nchi.

Eneo lililojengwa kiwanda na mining lilikuwa la vijiji vitano, ni eneo kubwa ambalo lilikuwa mali ya wananchi, Dangote kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya awamu ya nne waliwatapeli wale wazee kwa kuwapa vitu vidogo vidogo na ziara ya kwenda kuhiji kwa wazee wachache pamoja na laki tano tano na ahadi kibao wakabariki kuiacha ile ardhi na wale wazee wakatumika kuwashawishi wengine wakaingia kingi.

Mara kadhaa nilikuwa nikiwaona hawa wazee wanaojiita wenyeviti wa vijiji vile wakiambaa ambaa pale nje ya kiwanda cha Dangote wakitapeli watu kwa ahadi ya kuwaunganishia vibarua kiwandani wakati hata wao hawana ruhusa ya kuingia ndani ya kiwanda, wazee wamepigika wanajuta tu kimoyo moyo.

Niliwahi kujaribu kuongea na mmoja wao ambaye alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wakati huo nikiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hapo Kiwandani, nilipomuuliza sababu ya wao wazee kugawa ardhi bure kwa Dangote aliniambia kwamba wao waliamini Dangote si mfanyabiashara ni Alhaji kwa hiyo walitoa ardhi kwa Alhaji ili ajenge kiwanda kiwasaidie watu..

Nilishangaa sana, lakini kilichonifurahisha ni kwamba wanajuta maana zaidi ya laki tano na ziara ya Mecca hawajafaidika tena kwa namna walivyotarajia.
Mtindo wa ufanyaji kazi wa Dangote ni wa kitapeli tapeli tu, anatapeliwa kuanzia mfanyakazi wake wa chini mpaka Rais na mawaziri wakiingia kingi wanatapeliwa.

Kule Nigeria, ana kiwanda kikubwa Four kiln lines kwenye state ya Obajana na kingine Ibese, wafanyakazi zaidi ya 60% ni wahindi, wanaishi vizuri kila kitu wanachotumia ni tofauti na weusi, magari, nyumba za kuishi n.k ni tofauti kabisa.

Wahindi wanaletwa wakiwa hawajui kitu kabisa wanafundishwa na weusi (wanigeria) halafu wakishajua wanawasimamia weusi, wanawanyanyasa sana waafrika, pale ndipo nilipojua kwamba Tanzania ni nchi nzuri sana na siku zote nawambia ukitaka kujua uzuri wa nchi yetu Tanzania nenda Nigeria. Hususanu kufanye kazi kwa Dangote.

Wakati Dangote anafungua kiwanda Tanzania, alikuwa anaahidi kuajiri watanzania lakini ukweli ni kwamba alikuwa ameandaa makontena ya wahindi kuja Tanzania kama ilivyo Nigeria, thanks to God Magufuli akaingia Madarakani.

Wale wahindi wachache waliokuwepo walichukia sana wakaanza hata kukuza mambo au kutunga uongo wakiilaumu Serikali ati kwa kuweka vikwazo vingi, wakati mwingine wanamdanganya Dangote kuhusu Serikali yetu na Watanzania ili wao wapate faida. Ninao ushahidi wa mambo baadhi ambayo kwa makusudi kabisa management ya kihindi ilikuwa ikimdanganya Dangote kwa faida yao.

Mojawapo ilikuwa ni ubora wa makaa ya Mawe ya Tanzania, tulikuwa na vijana wetu maabara pale, hata mimi niliposikia kwamba makaa yetu ya mawe yana quality ya chini niliumia sana niliwauliza wahandisi wetu waliokuwa maabara wakasema ni uongo.

Hiyo ilikuwa mbinu ya wahindi kufanya biashara na makampuni ya South Afrika kwa faida yao huku wakichafua bidhaa zetu.

Lingekuwa jambo la ajabu sana kama serikali ingekubali uhuni huo, nawapongeza sana Mawaziri hawa wa awamu ya tano kwa kutumia elimu yao vizuri kuchunguza hilo kwa sababu hata enzi zile tulikuwa tuwaeleza serikali kila tunapopata nafasi lakini enzi ya awamu ya nne ilikuwa enzi ya aina yake. tulionekana wapuuzi au maskini wanoko.

Watanzania tunapopinga au kutetea ni vema tukatafuta ukweli kwanza, Dangote industries ukiisikia kwenye vyombo vya habari utaona ni mkombozi kwa watanzania, lakini kwa namna ilivyo na inavyotaka ifanyiwe ni hatari sana kwa taifa.

Tumshukuru sana Rais na serikali kwa msimamo wake. Dangote hana tofauti na akina Carl peters wa zamani labda abadilike.........

Itaendelea wiki ijayo
 
Dangote labda abadilike ndio tutaweza kufaidi uwepo wake hapa Tanzania, ila kwa jinsi alivyo na ninavyomfahamu..kwa sasa kuondoka kwake ni nafuu kwa Watanzania na Taifa.

Yule bwana hawezi kufanya biashara bila utapeli hata mfanyakazi wake wa chini kabisa anajua. Jamaa anaingia mahali kwa lugha tamu sana na ahadi kibao, lakini si mtu yule.

Wapo wanaosema kuhusu ajira za watanzania walioko pale, ni hivi wafanyakazi wataalamu walioko pale ni wale waliokuwa kwenye viwanda vingine vya cement vilivyokuwa vinawalipa vizuri ila baada ya kusikia tishio la ujio wa likiwanda kubwa ambalo lingepewa gas, exemption ya kodi n.k likapunguza bei ya cement viwanda hivyo vingekufa kwa kushindwa kujiendesha, hatua mojawapo zilizochukuliwa na viwanda bora kama vile Twiga na vingine ni kupunguza wafanyakazi kwa kiasi kikubwa ambao wengi walienda Dangote kulipwa ujira mdogo sana maana yeye Dangote anatumia management ya Wahindi.

Kule Nigeria alianza biashara zake kwa style ya kuwahonga viongozi wakuu na wakampa excemption ya kodi, matumizi ya barabara hovyo na vitu vingine akashusha bei ya Cement, viwanda vingine vikafa akabaki yeye mwenyewe akishikilia kama 90% ya soko la cement na Lafarge kama chini ya 10% vingine vilikufa baada ya kuhakikisha kwamba ameviua akapandisha bei ikarudi kama zamani.

Hivyo ndivyo alitaka kufanya Tanzania, JK alimpa maeneo makubwa sana, mpaka na eneo la kujenga bandari yake binafsi, jambo ambalo kwa maoni yangu naona ilikuwa hatari hata kwa usalama wa nchi.

Eneo lililojengwa kiwanda na mining lilikuwa la vijiji vitano, ni eneo kubwa ambalo lilikuwa mali ya wananchi, Dangote kwa kushirikiana na viongozi wa serikali ya awamu ya nne waliwatapeli wale wazee kwa kuwapa vitu vidogo vidogo na ziara ya kwenda kuhiji kwa wazee wachache pamoja na laki tano tano na ahadi kibao wakabariki kuiacha ile ardhi na wale wazee wakatumika kuwashawishi wengine wakaingia kingi.

Mara kadhaa nilikuwa nikiwaona hawa wazee wanaojiita wenyeviti wa vijiji vile wakiambaa ambaa pale nje ya kiwanda cha Dangote wakitapeli watu kwa ahadi ya kuwaunganishia vibarua kiwandani wakati hata wao hawana ruhusa ya kuingia ndani ya kiwanda, wazee wamepigika wanajuta tu kimoyo moyo. Niliwahi kujaribu kuongea na mmoja wao ambaye alikuwa mwenyekiti wa wenyeviti wakati huo nikiwa kiongozi wa chama cha wafanyakazi hapo Kiwandani, nilipomuuliza sababu ya wao wazee kugawa ardhi bure kwa Dangote aliniambia kwamba wao waliamini Dangote si mfanyabiashara ni Alhaji kwa hiyo walitoa ardhi kwa Alhaji ili ajenge kiwanda kiwasaidie watu..nilishangaa sana, lakini kilichonifurahisha ni kwamba wanajuta maana zaidi ya laki tano na ziara ya Mecca hawajafaidika tena kwa namna walivyotarajia.

Mtindo wa ufanyaji kazi wa Dangote ni wa kitapeli tapeli tu, anatapeliwa kuanzia mfanyakazi wake wa chini mpaka Rais na mawaziri wakiingia kingi wanatapeliwa.

Kule Nigeria, ana kiwanda kikubwa Four kiln lines kwenye state ya Obajana na kingine Ibese, wafanyakazi zaidi ya 60% ni wahindi, wanaishi vizuri kila kitu wanachotumia ni tofauti na weusi, magari, nyumba za kuishi n.k ni tofauti kabisa.
Wahindi wanaletwa wakiwa hawajui kitu kabisa wanafundishwa na weusi (wanigeria) halafu wakishajua wanawasimamia weusi, wanawanyanyasa sana waafrika, pale ndipo nilipojua kwamba Tanzania ni nchi nzuri sana na siku zote nawambia ukitaka kujua uzuri wa nchi yetu Tanzania nenda Nigeria. Hususanu kufanye kazi kwa Dangote.

Wakati Dangote anafungua kiwanda Tanzania, alikuwa anaahidi kuajiri watanzania lakini ukweli ni kwamba alikuwa ameandaa makontena ya wahindi kuja Tanzania kama ilivyo Nigeria, thanks to God Magufuli akaingia Madarakani. Wale wahindi wachache waliokuwepo walichukia sana wakaanza hata kukuza mambo au kutunga uongo wakiilaumu Serikali ati kwa kuweka vikwazo vingi, wakati mwingine wanamdanganya Dangote kuhusu Serikali yetu na Watanzania ili wao wapate faida. Ninao ushahidi wa mambo baadhi ambayo kwa makusudi kabisa management ya kihindi ilikuwa ikimdanganya Dangote kwa faida yao. Mojawapo ilikuwa ni ubora wa makaa ya Mawe ya Tanzania, tulikuwa na vijana wetu maabara pale, hata mimi niliposikia kwamba makaa yetu ya mawe yana quality ya chini niliumia sana niliwauliza wahandisi wetu waliokuwa maabara wakasema ni uongo.
Hiyo ilikuwa mbinu ya wahindi kufanya biashara na makampuni ya South Afrika kwa faida yao huku wakichafua bidhaa zetu.

Lingekuwa jambo la ajabu sana kama serikali ingekubali uhuni huo, nawapongeza sana Mawaziri hawa wa awamu ya tano kwa kutumia elimu yao vizuri kuchunguza hilo kwa sababu hata enzi zile tulikuwa tuwaeleza serikali kila tunapopata nafasi lakini enzi ya awamu ya nne ilikuwa enzi ya aina yake. tulionekana wapuuzi au maskini wanoko.

Watanzania tunapopinga au kutetea ni vema tukatafuta ukweli kwanza, Dangote industries ukiisikia kwenye vyombo vya habari utaona ni mkombozi kwa watanzania, lakini kwa namna ilivyo na inavyotaka ifanyiwe ni hatari sana kwa taifa.

Tumshukuru sana Rais na serikali kwa msimamo wake. Dangote hana tofauti na akina Carl peters wa zamani labda abadilike......... Itaendelea wiki ijayo
mwaga ukweli huo tujue. kajenga kiwanda afanye kazi aache kutaka kupendelewa.
 
Kama unavyomjua sio eeh? wabongo bana, mtu hata kukujua hakujui unajifanya unamfahamu grow up, yeye kama Investor hawezi kuja na kuhonga, yeye lazima apewe ahadi nzuri ili aje kuchoma pesa zake, sasa tatizo aliempa ahadi ni nani ndo wakushtakiwa sio mnalaumu tu upande mmoja
 
We umetumwa na washindani wa Dangote bilashaka
 
Mimi Huyu Dangote habari zake zimekuwa nyingi sana humu, ila sasa inanibidi mimi mwenyewe nitafute habari zake huko Nigeria ili nijue..

Kwa sababu, tunasikia kuwa kuna Hujuma zilikuwa zinafanywa na washindani wake akina Twiga ili kum-provoke Dangote ili ahamishe kiwanda chake, ila kwa hili, naweza kukubali maana, Ile siku Prof. Muhongo alienda na wazalishaji wa Saruji kule Mgodi wa NGAKA ili kuprove au Dis-prove uwepo wa makaa ya mawe, Ubora na wingi wake, Niliona kupitia Television mwakilishi mmoja wa kiwanda cha saruji akishangilia sana pale ambapo Prof. Muhongo alipotamka kuwa...."Tumejiridhisha kuwa makaa ya mawe yapo nchini na ni ya kutosha na ni bora, sasa sitatoa kibali cha kuagiza makaa ya mawe tena kwa mtu yeyote hata kama ni Dangote" huyo mwakilishi alishangilia sana hadi wenzie wakawa wanamzuia...pale nilipata kitu.

Kwa hiyo ili ku-deal na Dangote ni lazima tuangalie mikataba aliyoingia kwanza na hao Awamu ya Nne, inawezekana inatoa relief kwake.

Kuhusu, hilo la Bei ya bidhaa zake kuwa chini ili kuua viwanda vingine, TUME YA USHINDANI Ipo wapi?
 
Ukimaliza stori yako yote wiki ijayo kama ulivyosema, ndiyo nitachangia mkuu.Hata hivyo ahsante kwa kutuonjesha.
 
Baada ya nchi ya Morocco, Tanzania inafuatia kwa kuwa na watu wasiokuwa waaminifu duniani.
 
Mtoa mada nakuunga mkono. Kama management ipo chini ya wahindi bora waondoke tu hawa watu sio kabisa. Watu wa Arusha nadhani wanajua shida za wahindi pale A TO Z kisongo kuna unyanyasaji wa hali ya juu. Pia taasisi zinazokua chini ya wahindi ni shida hizohizo...hao wahindi walitaka wapewe gesi bure ili wapige cha juu na ndo zao. Kam kuna mtu anapinga viongozi wa serikali katika hili maana yake anaunga mkono mikataba ya kinyonyaji ya madini iendelee kutukamua.....Kaza Magufuli. Sikukuchagua lakini naamini utasimamia nidham na usawa, hakuna upendeleo vigezo na masharti kuzingatiwa kama hataki kununua makaa ya mawe ya bongo basi ayalipie kodi bandarini hayo anayotoa south
 
Mengine siyajui ila kuhusu ujira kweli jamaa anawalipa kidogo sana kuna jamaa yangu alitoka kwenye mgodi fulani wa dhahabu akaenda pale kama fundi salary alokutana nayo alifanya kazi mwezi 1 tu akachomoka akawa analalamika kuwa wahindi wanaharibu kile kiwanda na wamekamata positions zote muhimu.
 
Ukiona propaganda za "sizitaki mbichi hizi", zimezidi hivi ktk social media ujue hili saga limemwelemea Mjomba Magu na tujue tayari jamaa anajiandaa kung'oa mitambo ya kiwanda chake kukipeleka Kenya!!

Sasa mwoneni naye huyu, jamaa insha ndeefu na kila mstari umebebwa na na maneno..... jamaa ni tapeli .....tapeli.....tapeli, lakini cha ajabu hata hasemi alimtapeli nani, nini na wapi!!

Possibly, ukweli wa haya waweza kuwa ni the opposite.

Kwamba, inawezekana CCM ndiyo walikuwa wanataka kumtapeli jamaa na kwa kuwa kawashtukia na kama ilivyo asili yao kutapeli sasa wanajaribu kuigeuza picha up side down ili tushindwe kuisoma vyema!!
 
Daah, sasa hv nadhan hta mke akikuzingua inabidi uilaumu serikali ya awamu ya 4. Inasemwa vby na kila mtu aisee...!!

Sifahamu ukweli ni upi katika hili, ila wewe ni MNAFIKI kwa kuendelea kuwepo kwa Dangote wkt unajua sio watu wazuri. Wakati mlipokuwa mnapinga, ungeonesha uzalendo wa hali ya juu kma ungeacha kazi ili usiwe part ya udhalimu huo.

Kama Magufuli asingewakazia Dangote, TUNGEYAJUA YOTE HAYA...??? Au unatueleza ubaya wake huu kwa kuwa tayar uwezekano wa kazi kuwepo ni mdogo?? Mbn yote haya hayakujulikana kabla..??

Ulikuwa unawaeleza serikali. Nani ulimwambia..?? Au ulikuw unadiscuss na mkeo ambaye ni serikali ya nyumban kwako..? Unataka kutuaminisha kwmb serikali ya awamu ya 4 ilikuwa na wajinga wengi kiasi cha kutokukusikiliza hta kma ni kwa maslahi ya taifa..??

Nway, siku zote maskin huwa tunawaona matajiri ni watu wabaya sn. Na ukweli ni kwamba bila kuwa na kaukatili fulani ni ngumu sn kuwa tajiri.
 
Back
Top Bottom