SoC01 Fahamu umuhimu wa kuwa na ujuzi wa kidijitali

Stories of Change - 2021 Competition

Frank Akile

New Member
Nov 3, 2020
2
3
FAHAMU UMUHIMU WA KUWA NA UJUZI WA KIDIJITALI.

Hatimaye tumeingia katika dunia yenye machaguo mawili pekee ambayo ni 'Nenda dijitali au rudi nyumbani'. Machaguo haya yana maana ya kwamba, dunia ya sasa inaendeshwa kama sio kujiendesha yenyewe katika mifumo ya kikompyuta na au kiintaneti. Dunia ya sasa inapokea chaguo moja tu kwa sasa ili kumfanya mtu kufanikiwa: nalo chaguo hilo ni kutenda na kutembea katika njia za kidijitali. Hivyo kitendo cha mtu kutokubaliana na kutumia ujuzi wa kidijitali kinafananishwa na mtu aliyechagua kubaki nyuma katika maendeleo yoyote (kurudi nyumbani)

Hakuna shaka kua, baadhi yetu tumeshashudia na tunaendelea kushuhudia namna ulimwengu huu uendavyo kasi katika mabadiliko ya kitekinolojia, hususan teknolojia ya kikompyuta na au kiintenet (dijitali) kwa malengo ya kurahisisha shughli ngumu ambazo zisingwezekana kwa urahisi kwa uwezo wa kibinadamu pekee.

Mabadiliko haya ya kiteknolojia hususan, tekinolojia ya kikomyuta na au kiintanet (dijitali), yameweza kuupeleka unafuu katika shughuli mbalimbali za mwanandamu katika nyanja zote za kimaisha kwa maana ya kiuchumi, Kisiasa, Kijamii na hata kiutamaduni. Mabadiliko haya ya kitekinolojia yameweza kurahisisha shughuli za kimawasiliano miongoni mwa wanandamu, Pian mabadiliko haya ya kiteknolojia yameweza kuhamasisha na kurahisisha shughuli za kibiashara na uchumi. Mabadiliko haya pia yamerahisisha mwingiliano wa wanadamu kutoka mataifa tofautiytofauti wenye tija katika kubadilishana fikra chanya (elimu) kuhusiana na mambo mbalimbali ambayo yanapaswa kuigwa na au kuachwa.

Utafiti wa benki ya dunia unafafanua kua, katika miaka kadhaa ijayo, karibu kila shughuli ya mwanadamu itahitaji ujuzi wa kitekinolojia hasa tekinolojia ya kikompyuta na kiintaneti (dijitali), katika ufasiliwaji na au utekelezaji wake. Hii ina maana Kua, hitaji la ujuzi wa kitekinolojia hususani, tekinolojia ya kidijitali kwa kizazi cha sasa na hata kizazi kujacho ni jambo lisilokuwa la hiari tena, bali ni la lazima kwa mwanadamu yeyote mwenye kuhitaji kupiga hatua za kimaendeleo yawayo yote na au kuendelea kukishikilia kile alicho nacho kama sehemu yake ya kuishi, kwa mfano biashara, mawasiliano, afya, elimu, ulinzi na kadhalika.

Dijitali na ujuzi wa kidijitali.

Kwa tafsiri isiyo rasmi sana, neno dijitali linachipukia katika neno dijiti lenye maana ya mfumo wa namba 0,1 mpaka 9 pamoja na maneno, pamoja na alama mbalimbali zilizohifadhiwa katika mifumo ya kikompyuta katika vifaa vyote vya kikompyuta ili kurahisisha shughuli mbalimbali za mwanadamu. Mfumo wa kidijitali pia, umeweza kubeba mifumo ya sauti, picha mnato, picha mjongeo ili kurahisisha shughuli mbalimbali za mwanandamu ambazo zingeshindikana au kumfanya mwanadamu kutumia muda mwingi na gharama kubwa.

Hata hivyo mifumo hii ya kikompyuta imekuwa ikichagizwa sana na maendeleo ya kimtandao na au intaneti kama njia kuu ya kuzisafirishia data za kimawasiliano kwa kutumia vifaa vya mawasiliano vyenye asili ya kikompyuta.

Mifumo hii ya kikompyuta iliyo katika vifaa vya kikompyuta imweza kufungamanishwa katika vifungashio maalumu (Applications) kutokana na aina fulani ya kazi inayohitajika na mtumiaji kwa wakati husika.

Ujuzi wa kidijitali ni nini?

Ni hakika yangu kua, endapo utachukua hatua ya kumuuliza mtu mmoja mmoja na kuwataka wakuambie wanachokifahamu kuhusiana na neno 'ujuzi wa kidijitali', watakupatia majibu tofauti tofauti kutokana na kiwango chao cha uelewa kuhusiana na dhana hii ya ujuzi wa kidijitali. Miongoni mwa watu hao utakaowauliza wataweza kukuambia kua, ujuzi wa kidijitali ni uwezo wa kutumia vifaa ya kimawasiliano vya kikompyuta kama simu na kompyuta, wengine watakuambia ujuzi wa kidijitali ni uwezo wa kutumia vifungashio (applications) sahihi zinazopatikana katika vifaa vya kikompyuta ili kupata faida fulani. Watu hao wote wanaweza kuwa sahihi lakini tofauti yao itakuwa katika ufahamu wa ziada wa mtu mmoja dhidi ya mtu mwingine.

Kwa mujibu wa shirika la umoja wa mataifa la elimu, sayansi na utamaduni (UNESCO) mwaka 2018, wanaufafanua ujuzi wa kidijitali kama kiwango cha uelewa na au uwezo wa mwanadamu katika kuvitumia vifaa vya kikompyuta, vifungashio vya kimawasiliano vya kikompyuta (applications) pamoja na namna ya kuufikia mtandao na kuweza kupata au kutoa taarifa. UNESCO wanaendelea kuifafanua dhana hiyo ya ujuzi wa kidijtali kwa kusema kua uelewa na au ujuzi huo wa matumizi ya vifaa vya kikompyuta, ndio unaowawezesha wanadamu kubuni name kubadilishana mahitaji mbalimbali ya kikompyuta, kuwasiliana na kushirikiana pamoja na kutafuta masuluhisho juu ya changamoto mbalimbali ambazo kwa namna moja au nyingine zinachelewesha maendeleo ya mwanadamu.

Katika maana rahisi, ujuzi wa kidijitali ni kadiri ya uelewa na au uwezo wa mwanadamu katika kuvitumia vifaa vya kikompyuta na mtandao au intaneti pamoja na vifungashio vyake (applications) kulingana na mahitaji ya kibinadamu ya kimawasiliano au mwingiliano wa wanadamu kiuchumi, kisiasa, kijamii na au kiutamaduni kwa njia ya kimtandao na au (intaneti).

Ujuzi wa kidijitali unaweza kupimwa na mtu mwenyewe Kwa kujiuliza maswali yafuatayo.

•Je, ninaweza kuwasha na kuzima vifaa vya kikomyuta Kama simu ya mkononi, tableti na kompyta mpkato?
• Je, ninaweza kutumia vielekezi vya kifaa cha kikompyuta kama keyboard mouse na kadhalika?
• Je, ninaweza kuvitumia vielekezi katika kifaa cha kikompyuta kunirahisishia kazi ninayotaka kuifanya?
• Je, ninaweza kupata mrejesho ninaoutarajia kutoka katika kifaa cha kikompyuta?
• Je, ninafahamu namna ya kuunganisha kifaa cha kikompyuta na mtandao (intaneti) ili kitafuta taarifa nitakayo ihitaji?
• Je, ninaweza kutambua mtandao salama wa kuundanisha na kifaa cha kikompyuta kwa ajili ya matumizi mahususi?
• Je, ninaweza kutafuta taarifa kupitia injini za kiintanet (kwa kutumia browser kuingia katika websites, kwa kutumia injini Kama google, yahuu n.k) kupitia kifaa cha kikompyuta?
•Je ninaweza kupakua taarifa au maudhui kutoka katika mitandao na kupakia maudhui yangu katika mitandao hiyo kwa kutumia kifaa cha kikompyuta?
• Je, ninaweza kuhifadhi taarifa au data zangu kwa kutumia nywira (passwords) au namna yoyote kuhakikisha usalama wa data zangu katika kifaa cha kikompyuta?
• Je, ninaweza kubadilisha taarifa zangu za kiusalama kama nywira na mengine katika kifaa changu cha kikompyuta?

Maswali yote hayo yatamwezesha mtu kuelekea katika kuwa na ufahamu/uelewa wa namna ya kutumia vifaa vya kikompyuta ili kupata faida anayoihitaji kwa wakati fulani, kwani kwa kutafuta majibu ya maswali hayo mtu huyo ataweza kutumia vifaa vya kikompyuta kupata taarifa, kuelewa taarifa na kutoa taarifa kwa njia za kimtandao kwa kutumia kifaa cha kikompyuta. Ataweza kubuni na kuahriri vyema maudhui ya kimtandaoni kwa kupitia kifaa cha kikompyuta. Ataweza kuwasiliana kimtandao mfano kwa kutumia mitandao ya kijamii. Pia ataweza kufanya shughuli za kibiashara (kama kutangaza kuuza na hata kununua bidhaa) kwa njia ya mtandao kwa kutumia kifaa cha kikompyuta na ataweza kuwajibika kwa usalama na kuepukana na usumbufu wa kisheria za kimitandao.

Ujuzi wa kidijitali unapatikana wapi?

Zipo njia kuu mbili za ujifunzaji wa ujuzi huu wa kidijitali. Njia ya kwanza ni kwa kupitia elimu rasmi, elimu itolewayo katika vyuo vinavyofundisha masomo ya tekinolojia, habari na mawasiliani (TEHAMA) na au masomo na au masomo ya tekinolojia ya mawasiliano. Wakati njia ya pili ikiwa ni ile isiyohitaji elimu rasmi, bali elimu ya kujifunza kutoka kwa wengine wanaotuzunguka katika jamii ambao wameshatutangulia kufahamu baadhi ya ujuzi fulani fulani katika vifaa vya kikompyuta pamoja na vifungashio vyake (applications) pamoja na kujifunza kupitia semina za mafunzo ziandaliwazo na watu/taasisi binafsi pia kwa kujifunza kupitia machapisho, ya kimaandishi na sauti na hata video za mafunzo ziwekwazo huko mitandaoni hasa katika mitandao ya kijamii ambayo imweza kufikiwa na watu wengi zaidi wanaomiliki vifaa rahisi vya kikompyuta kama simu janja (smartphones), kompyuta mpakato na kadhalika.

Hata hivyo kutokana na maendeleo ya kisayansi na kitekinolijia ulimwenguni, utafutaji wa ujuzi wa kidijitali umekuwa hautegemei sana elimu ya madarasani pekee. Ujuzi huu wa kitekinolojia umekuwa ukirithishwa kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine kwa namna ya kuelekezana namna ya kutumia kifaa fulani cha kikompyuta sambamba na vifungashio vyake (applications).

Leo hii watu hujifunza kutumia vifaa hivyo vya kikompyuta kutoka kwa wenzao waliowatangulia kufahamu. Mfano mzuri unaweza kuwa ule wa matumizi ya simu mpya za mikononi hususan simu janja (smartphones) zinazotoka kila wakati pamoja na vifungashio vya huduma (applications) vinavyobuniwa kila wakati. Hii ni sawa na kusema kua: ili mtu aongeze ujuzi wake haimlazimu yeye kuhudhuria katika elimu rasmi (shule) bali anaweza kujifunza tu kutoka kwa watu wengine waliomtangulia kufahamu huduma fulani ya kikompyuta na au kupitia mafunzo yatolewayo na watu au taasisi binafsi, pia katika mitandao ya kijamii kama kurasa za facebook, makundi ya whatsap, kurasa za instagram pamoja na mtandao wa video wa YouTube.

Kuna faida gani kwa mtu kuwa na ujuzi wa kidijitali na ni hasara zipi mtu anaweza kuzipata asipokua na ujuzi wa kidijitali?

Kama tulivoona katika aya za awali hapo juu kua, suala la ujuzi wa kidijitali limekuwa sio suala la hiari tena kwa maendeleo ya mwanadamu kwakua limekua ni suala la lazima kwa mwanadamu yeyote mwenye kuhitaji kuendelea katika nyanja yoyote ya kimaisha, iwe ni kiuchumi, kisiasa, kijamii na wakati mwingine hata kitamaduni.

Hii inatokana na mabadiliko ya ufanyaji kazi ya mwandamu ya hapo awali, ambapo kazi nyingi zililazimika kufanyika kwa mikono tofauti na sasa ambapo mifumo ya kiroboti (kikompyuta) imechukua nafasi ya mikono au mwili wa mwanadamu katika kumrahisishia mwanadamu huyo shughuli mbalimbali.Shughuli zote za mwanadamu zimeanza kuahmia katika mifumo hii ya kikompyuta huku mwanadamu mwenyewe akionekana kuepukana na shughuli ngumu (shughuli za mikono).

Leo hii, mtu hataweza kushiriki kikamilifu katika shughuli za kielimu kama hataweza kujifunza namna ya kutumia vifaa vya kikompyuta, kwani malighafi nyingi za kijifunzi pamoja na vielelezo vya kujitisheleza vimekuwa vikihifadhiwa katika mitandao na intaneti.

Leo hii, mtu hataweza kuitangaza biashara yake kwa watu wengi zaidi na kupata wateja wengi zaidi kama hatajifunza namna ya kutangaza kwa njia ya mitandao na intaneti ambako ndiko macho ya watu wengi hutupiwa wakitafuta wanayoyahitaji.

Leo hii, mtu atachelewa kupata masuluhisho ya kiafya kama hataweza kuwa mwenye kujifunza kupitia mitandao na intaneti ambako hata dondoo za kitabibu huhifadhiwa huko.

Leo hii, mtu hatapata burudani mpya kama atajifungia kwenye ujinga dhidi ya ujuzi wa kidigitali, kwani taarifa nyingi za kiburudani huweza kupatikana kwa njia Za kimtandao na intaneti tena katika muonekano picha halisi na picha jongevu (video) hali kadhalika upataji wa burudani au taarifa ya moja kwa moja kutoka katika eneo la tukio (live).

Leo hii pia , mtu asipokuwa na ujuzi wa kidijitali hataweza kuelewa kinachofanywa hata na viongozi wake wa kisiasa hivyo asielewe kama kiongozi wake anatekeleza anachokihitaji au laa.

Kwa kifupi, ujuzi wa kidijitali humuunganisha mtu mmoja na watu wote wa ulimwengu huu kwa kuchangamna nao katika kuwasiliana, ktika kufanya biashara, wakati mwingine hata kuabudu Mungu na kadhalika.

Kwa kuhitimisha

Kabla ya kuhitimisha, yapo mambo mawili ningependa kuyasisitiza kwa nchi kwa maana ya serikali pamoja na mtu mmoja mmoja kwa maana ya jamii.

Mosi, elimu juu ya ujuzi wa kidijitali ni ya muhimu sana:

Elimu ya kidijitali inapaswa kutolowa katika mifumo yote ya elimu katika nchi. Na ili nchi iendelee kitekinolojia na au kidijitali, ujuzi wa kidijitali unapaswa kufundishwa katika elimu rasmi kuanzia elimu ya msingi kabisa ili kumuandaa mtoto/kijana kuweza kuendana na mahitaji ya kidijtali ambayo hayakwepeki. Pia elimu isiyo rasmi ihamasishwe. Elimu kupitia mtu mmoja mmoja na au taasisi zisizo za kiserikali pamoja na uhamasihaji kwa njia za mitandao na intaneti hasa mitandao ya kijamii ni muhimu ili kuchagiza ongezeko la ujuzi wa kidijitali kwa watu wote katika jamii au nchi kwa ujumla.

Pili, Jamii iandaliwe kuwa na mapokeo chanya linapokuja suala la ujuzi wa kidijitali ili kurahisisha maendeleo ya wanajamii wenyewe:

Jamii inapaswa kutolifungamanisha suala la ujuzi wa kidijtali na imani potofu pamoja na masuala ya kijinsia katika jamii husika. Jamii inapaswa kutambua kua ujuzi wa kidijitali ni wa jinsia zote mbili yaani wanaume na wanawake na katika hali ya usawa. Jamii itambue ujuzi wa kidijitali na umiliki wa vifaa vya kikompyita kuwa si wa wanaume pekee na kuwanyima fursa wanawake kumiliki vifaa vya kitekinolojia na kujifunza kupata ujuzi wa kidijitali.

Kwa kufanya hivyo jamii itaweza kuendana na kasi ya mabadiliko ya kitekinolojia duniani, na hatimaye kuhakikisha ukuaji wa kimaendeleo wa jamii yenyewe kiuchumi, kisiasa, Kijamii na hata kiutamaduni.
 
3 Reactions
Reply
Back
Top Bottom