Fahamu tofauti kati Kadinali na Askofu ktk kanisa Katoliki

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
" Canon Laws" ambazo ibara zake hutajwa hivi, Can. 381 nakafhalika zinatosha kumwelewesha yeyote muundo wa Kanisa Katoliki. Zinataja mamlaka ya askofu, askofu-mkuu, kardinali, rais wa baraza la maaskofu na zaidi.

Sheria ya kanisa, Can. 381(1) na Can. 391(1), zinasema kwamba askofu jimboni, ndiye mkuu na mwenye madaraka jimboni.

Ibara hii inatokana agizo la mkutano wa maaskofu uitwao Vatican II, uliotoa hati iitwayo “ Lumen Gentium” ibara ya 27, isemayo kwamba, askofu jimboni ni mwakilishi wa Yesu na si mwakilishi wa Papa au chombo chochote.

Vilevile, hakuna andiko la kanisa linalotaja maneno “Makao makuu”. Badala yake jengo la kanisa liitwalo “ Cathedral ” ndilo lenye mamlaka ya uaskofu.

Kwa wale wanaopenda neno “Makao makuu”, basi afadhali waseme “ Cathedral ” ndiyo “Makao makuu” ya kanisa jimboni.

Pale Roma, “ Cathedral ” ni kanisa liitwalo “St. Lateran’s archbasilica”. Kumbe, makao “makuu ya Kanisa Katoliki duniani”, siyo anakoishi Papa yaani kule Castle Gandolfo au pale Vatican, bali ni hapo “St. Lateran archbasilica”.

Hata kanisa maarufu lililopo Vatican, yaani “St. Peter’s basilica”, lina hadhi ndogo iitwayo “Basilica”, wakati hili la “makao makuu” linaitwa “Arch-basilica”, hadhi kubwa kuliko makanisa yote Katoliki duniani.

Ibara ya 390 na 436(3) ya sheria za kanisa, zinamkataza askofu (bishop ) pamoja na askofu-mkuu ( arch-bishop ) wasiendeshe misa kwenye “ Cathedral ” bila ruhusa ya askofu mahalia, yaani askofu mwenye jimbo.

Hivyo, Polycarp Kardinali Pengo au askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, hawawezi kuendesha misa kwenye “ Cathedral” ya Moshi, yaani kanisa kuu la jimbo la Moshi, bila kwanza kuruhusiwa rasmi na askofu wa Moshi Isaac Aman.

Pia, kwa kutumia sheria, Can. 763, askofu wa jimbo, mfano pale hapa Moshi, amepewa mamlaka na Papa kumpiga marufuku askofu yeyote duniani asihutubie lolote jimboni kwake ikihitajika kufanya hivyo. Yaani zikiwepo sababu za msingi kufanya hivyo.

Mwaka 2004, Joachim Kardinali Meisner, alitumia ibara hii kumkataza askofu Jacques Gaillot asiingie jimboni Cologne, kwani alikwishachokwa kuigawa nchi kwa kauli zake alizoziita “ni maoni yake binafsi”.

Nimechagua ibara hizi chache kuonyesha mamlaka ya askofu, uone kwamba, hakuna askofu hata mmoja nchini aliye juu ya mwingine. Kila mmoja ana mamlaka kamili katika jimbo lake, na ndiye mchungaji wa waumini walio katika jimbo lake.

SASA TUONE UKARDINAL NI NINI?

Mkatoliki akitaka utumishi wake utambulike rasmi kikanisa, lazima atasajiliwa au kusimikwa kwenye kundi linalotambulika. Mara nyingi huwa ni jimboni au kwenye jumuiya ziitwazo “ religious”.

Zamani kila aliyesimikwa hivyo aliitwa “kardinali”. Lakini kuanzia karne ya tisa, neno “kardinali” lilibaki kutumika tu kwa walioitwa na Papa wakahamia na kusimikwa upya Roma.
Padri aliyehamishiwa Roma, huko alisimikwa kwenye kanisa lililoitwa “ titular church”. Hiyo ikawa aina ya kwanza ya makardinali, wakijulikana kama “ cardinal-Priest ”.

Baadaye mashemasi nao wakawa wanahamishiwa Roma, huko wakapewa vituo vilivyoitwa “ deaconia ”. Ikawa aina ya pili ya makardinali waitwao “ Cardinal-Deacon ”.

Kazi za Papa zilipoongezeka, akahitaji msaada wa maaskofu kutoka majimbo jirani yaliyoitwa “ Suburbicarian Diocese”. Hali ya maaskofu hawa kuwa karibu na kuhitajiwa Roma, kukawafanya waitwe “ Cardinal-Bishop ”.

Hizi ndizo aina tatu za makardinali. Zipo hadi leo, yaani “ Cardinal-Deacon ”, “ Cardinal-Priest ” na “ Cardinal-Bishop ”.

Kuanzia mwaka 1150, Papa alianza kuwaita makardinali kwenye vikao vya kumshauri, ambavyo hadi leo vinaitwa “ Consistory” .

Mwaka 1179, haki ya kumchagua Papa mpya, ikaacha kuwa ya wanajimbo wengine wa Roma, bali ikabaki kwa “makardinali” tu kwenye mkutano unaoitwa “ Conclave ”. Mwaka 1975, Papa Paul VI alifupisha umri wa kardinali kuhudhuria “ Conclave ”, yaani chini ya miaka 80.

Tumeona kwamba, kitendo cha kupewa ukardinali na Papa, ni uhamisho wa kwenda Roma. Uhamisho huo unamfanya awe mwanajimbo wa Roma, ambaye kama haishi Roma, basi kokote aliko duniani anafanya umisionari.

Ile aina ya “ Cardinal-Bishops ” bado hupewa lile kanisa liitwalo “ Suburbicarian Diocese”. Siku hizi “ Cardinal-Deacons ” hupewa hata yale makanisa, “ titular church”.

Ile aina ya “ Cardinal-Priest ”, wengi hawaishi Roma kwa sababu ya umisionari wao mbali na Roma. Mmojawapo ni Polycarp Kardinali Pengo, anayeongoza Jimbo la Dar es Salaam, lililo kilomita 6043 kutoka Roma.

Je, mtu anapewa ukardinali baada ya kufikia ngazi ipi ya utumishi? Teodolfo Kardinali Mertel, alipewa ukardinali Machi 15, 1858 akiwa hajapata hata ushemasi. Machi 20, 1556 Reginald Kardinali Pole alikuwa ameshakuwa kardinali kwa miaka 20 na ameshashiriki “ Conclave ” tatu akiwa hajawa padri.

Kuanzia Februari 2, mwaka 1983, Papa John Paul II aliwapa ukardinali mapadri saba, waliobaki na upadri wao bila kuwa maaskofu.

Watano kati yao wameshafariki ambao ni Henri Kardinali de Lubac, Avery Kardinali Dulles, Aloys Kardinali Grillmeier, Joseph Kardinali Congar, Leo Kardinali Scheffczyk. Wawili kati yao wako hai, yaani Roberto Kardinali Tucci na Albert Kardinali Vanhoye.

Papa Benedict XVI, naye ana mapadri wanne aliowapa ukardinali bila kuwa maaskofu. Watatu wamekwishafariki, ambao ni Domenico Kardinali Bartolucci, Urbano Kardinali Navarrete, Umberto Kardinali Bett. Aliye hai ni Josef Kardinali Becker.

“ Roman Curia ” ni jopo linalomsaidia Papa kuendesha kanisa lote duniani. Karibu timu yote “Roman Curia” huripoti shughuli zake kwa “ Secretariet of State”.

Hivyo, “ Secretariet of State ” ana majukumu mazito ndani na nje ya Kanisa, kwani Papa anaweza kusifiwa au kulaumiwa ndani na nje ya kanisa kwa sababu tu ya utendaji wa huyu “ Secretariet of State”.

Nafasi hii ya “ Secretariet of State ” sasa inashikwa na Pietro Kardinali Parolin, aliyeachiwa na Tarcisio Kardinali Bertone.
Wote Kardinali Bertone na huyu Parolin ni maaskofu. Lakini mwaka 1848, nafasi hii ilisimamiwa vizuri na Giacomo Kardinali Antonelli, ambaye alikuwa shemasi tu hadi kifo chake Novemba 06, 1876.

Papa anaweza kumpa mtu ukardinali kwa siri, yaani “ Cardinal in pectore” . Serikali ya China ilipomfunga askofu Ignatius Kung Pin-mei wa Shanghai, haigundua kwamba akiwa humo gerezani alipewa ukardinali kwa siri mnamo Juni 30, 1979.

Kardinali yeyote, kama alivyo Polycarp Pengo, siyo mwakilishi wa nchi kama Tanzania, kwani, hakuna jimbo wala parokia inayoitwa Tanzania.

Tumeona kwamba ukardinali ni kuwa mwanajimbo wa Roma au jirani na Roma (suburbcarian ). Hivyo, hata inavyoelekeza sheria ya kanisa, Can. 357(1), kardinali ni mwakilishi wa parokia yake pale Roma yaani “titular chuch”, ambayo ya Polycarp Pengo pale inaitwa Nostra Signora de La Salette.

Lakini ibara hiyo 357(1), bado inamdhibiti kardinali kwamba, hata hiyo parokia yake pale Roma, haruhusiwi kuiingilia kiutawala, kiuendeshaji au kinidhamu.

Hivyo, eneo pekee duniani ambako Polycarp Pengo ana mamlaka ya uchungaji, utawala, uendeshaji au nidhamu, ni ndani ya mipaka ya Dar es Salaam tu (rejea, Can. 381(1).

Wakati mabaraza ya maaskofu yanashamiri duniani, baadhi ya maaskofu waliitaadharisha Vatican kwamba, ama baraza zima au rais wa baraza hilo, ataweza kujikuta anaingilia ukuu wao jimboni na kugeuka kuwa mkuu nchini.

Hivyo, Papa aliiweka ibara ya 455(4) makusudi kulinda huo ukuu wa askofu wa jimboni, ili asiingiliwe kwa namna yoyote na baraza zima au rais wa baraza la maaskofu.

Hivyo, ibara hii inatosha kukuthibitishia kwamba, rais wa baraza la maaskofu, si kiongozi wa Kanisa Katoliki nchini, wala si mkuu wa maaskofu nchini.

Hivyo, Rais wa TEC, Askofu Tarcicius Ngalalekumtwa, naye eneo pekee la ukuu wake, ni mipaka ya Jimbo la Iringa tu. Nafadi yake kama Rais wa TEC inaheshimiwa na maaskofu wote pale tu anapotoa tamko kwa niaba yao. Yaani anaposimama kwa niaba ya kauli ya maaskofu wote, au anapotoa taarifa fulani kwa kuzingatia mipaka yake halali kiuongozi.

Mkutano wa makardinali wote duniani na Papa yaani “ consistory”, hauna mamlaka ya kutoa tamko kisha liitwe kuwa ni la Kanisa Katoliki duniani. Huo ni mkutano wa askofu wa Roma na wanajimbo wake.

Wakati mkutano wa maaskofu wote duniani na Papa, ndicho chombo kikuu kupita vyote kiitwacho “ magisterium”, chenye mamlaka ya kuamua lolote ndani ya Kanisa Katoliki.

Ibara ya 1121 ya Katekism ya Kanisa Katoliki inasema, askofu haachi kuwa askofu hadi kifo chake, hata akijiuzulu madaraka.

Lakini ukardinali ni tofauti. Padri Louis Billot alikuwa kardinali kwa miaka 16 ,alipojiuzulu ukardinali Septemba 21, 1927, akaacha kuwa kardinali.

Hivyo, uaskofu ni nafasi ya juu zaidi na nyeti zaidi ndani ya Kanisa Katoliki, kuuzidi ukardinali.

TUMSIFU YESU KRISTO!
 
asante kwa hii elimu mkuu.

naomba unitoe tongotongo zaidi kuhusu nomenclature inayotumika kum-address askofu Pengo:
anakuwa addressed kama Polycarp Kadinali Pengo (kwangu mimi hii naona ni sawa na kum-address rais kama John Pombe Rais Magufuli badala ya Rais John Pombe Magufuli).

sasa kwa Pengo... kwa nini isiwe Kadinali Polycarp Pengo?
 
Inatia uvivu kusoma maana ni ndeeeefu!!! ndio shida ya kucopy na kupest maana huwezi summarize.
 
Hii nilikuwa najua japo niliambiwa nikiwa bado mdogo sana ukiisoma kwamakini utaelewa kuwa tamko lolote la askofu yeyete lisipopitishwa na maaskofu wote kwa ujumla hilo sio la baraza la maaskofu wa nchi husika bali huwa la mtu binafsi kwa kadili yake maana hapa utaelew mipaka ya ukuu wa madaraka
Hongeraaaaa
 
Amina mkuu
 
Jifunze kuheshimu uhuru wa mtu
Uhuru wa kucopy & paste? Ukiulizwa maswali hapa, unayo majibu? Si ndio mwanzo wa kutoa taarifa au majibu yasiyo ya kweli? Mambo mengine yaishie huko huko kwenye magroup ya whatsapp, watu mtaulizana na kujiuma huko huko. Hapa naamini ukiulizwa swali kuna mawili; either utakimbia au utajibu uongo!
 
Back
Top Bottom