Yoda
JF-Expert Member
- Jul 22, 2018
- 37,558
- 46,099
Dunia imegawanyika katika sehemu kuu tatu.
1.Vitu halisi vinavyoweza kuthibitishwa na milango ya fahamu ya binadamu mfano kiti,mlima, nguo,nyumba,mnyama,binadamu mwenzako,nyota,sayari n.k.Pia vitu kama hewa,umeme,radi ambavyo kuna njia za kisayansi kuweza kuvipima.Hivi ni vitu ambavyo ni dhahiri na havitegemei utamaduni au hadithi za binadamu kuwepo kwake.
2.Vitu/hali visivyo halisi ambavyo vimejengwa tu katika akili za watu mfano dini, taifa, utamaduni, uzalendo, Taifa, mifumo ya kifedha.Hizi ni dhana ambazo wanadamu wameziunda kutokana na kuambiana story kwa muda mrefu lkn sio vitu halisi hasa bali vilivyoundwa katika fikra za binadamu tu, nje ya hapo havipo,sio vitu halisi.
Kwa upana zaidi ni kwamba huwezi kuliona Taifa,japo kuna watu wanakufa katika vita kwa sababu ya mataifa yao.Huwezi kuliona kampuni japo kila siku watu wanaenda kufanya kazi kwenye kampuni zao, huwezi kuuona uzalendo japo umekuwa ni wimbo katika kila taifa.Hivi vyote ni vitu ambavyo binadamu wamekubaliana tu viwepo baada ya hadithi nyingi wakati wowote wanapokubalina visiwepo au wakafarana kwa kiwango cha juu huwa vinatoweka.Hivyo ni dhahiri ni vitu vilivyo katika fikira za binadamu tu ila sio vitu dhahiri.
3.Vitu/hali zilizo katikati ya vitu halisi na visivyo halisi mfano hisia za mapenzi, huruma, ndoa, familia, aibu, haya n.k
Vitu vilivyo katika kundi namba mbili na tatu ndivyo vinavyoitwa utaratibu wa ulimwengu(order) na ndivyo vinavyoathiri maisha ya binadamu katika kukaa pamoja.