Fahamu sababu za ndani kabisa zinazomfanya Zitto ajipendekeze mbele ya Lissu

Ndata

JF-Expert Member
Mar 2, 2017
226
321
ZITTO KAAMUA KUKITUMIA KIFARANGA KUIVURUGA CHADEMA.

Mwaka 2014 moja kati ya hotuba zinazoishi ni ile ya Zitto kumfananisha Lissu na kifaranga mbele ya vyombo vya habari.

Mwaka 2018, Zitto alimfananisha Lissu na Zwazwa kwenye majibizano huko bunge la Twitter.

Mwaka 2019, Zitto anahaha kumtafuta Lissu ili aungane nae. Zitto anataka kuungana na kifaranga? huu unyonge Zitto kautoa wapi? Twende pamoja..

Moja, Zitto hajawahi kuwa mnyonge mbele ya mtu, huwa mnyonge pale anapoiona nafasi ya upigaji au uvurugaji. Zitto alikuwa tayari kutengana na Chadema kipindi Chadema imeshika kasi na uhakika wa kutwaa dola ukiwa 45% bado hakukubali kuwa mnyonge au kufunika kombe ili historia mpya iandikwe.

Pili, Zitto hajawahi kumkubali Lissu, kwake Zitto watu aina ya Lissu huwaita washamba na vifaranga.

Baada ya kuangalia hayo mawili sasa fahamu sababu za ndani kabisa zinazomfanya Zitto ajipendekeze mbele ya Lissu.

Kisasi cha Zitto kwa Chadema, Wakati Zitto anafukuzwa Chadema aliahidi kuhakikisha Chadema inakufa na alikula kiapo cha kuivuruga. Harakati za kuivuruga zilianza pale alipoanza kuituhumu Chadema ya kuwa ni chama cha kidini na Kikanda, Kuhakikisha anasajili kutoka Chadema zaidi na kuweka nguvu kubwa kwenye majimbo yaliyokuwa chini ya Chadema huku mgombea urais na team yake wakitembea kila sehemu ya nchi hii kuinanga Chadema.

Mtu wa Kigoma huhakikisha kiapo alichokula kinatimia kwa njia halali na zisizo halali. Kwake Zitto njia halali za kufanya siasa Chama Chake kiwe kikubwa kuliko Chadema zimeshindikana sasa kaamua njia zisizo halali kuichonganisha kwa kumtumia Lissu anayeonekana ana nguvu dhidi ya Chama chake.

Kwa lengo hili, ni rahisi kwa Zitto kumsujudia kifaranga na Zwazwa ili lengo lake litimie.

Chadema wanaufahamu mchezo wote ndio maana wanamuangalia tuu anavyojibaraghua mitandaoni huku akiandika makala uchwara na kumpa Ado yote kutaka aingie ndani ya mfumo au kumnasa Lissu iwe pigo kwa Chadema.

Mbaya zaidi, inaaminika harakati zote hizi zinafadhiliwa na baadhi ya vigogo Ccm, hawa ni vigogo wanaoamini Chadema ikianguka kuna baadhi ya majimbo yatakuwa myepesi kwao hivyo kujenga ngome imara ya kupata mgombea urais kupitia Ccm mwaka 2025.

Lissu kuwa macho, usikubali kutumika kama walivyotumika kina Mwigamba, Machali na wengine wengi. Wewe unawaza ukombozi mwenzako anawaza kulipa kisasi na kutimiza kiapo.
 
Kisasi cha Zitto kwa Chadema, Wakati Zitto anafukuzwa Chadema aliahidi kuhakikisha Chadema inakufa na alikula kiapo cha kuivuruga. Harakati za kuivuruga zilianza pale alipoanza kuituhumu Chadema ya kuwa ni chama cha kidini na Kikanda, Kuhakikisha anasajili kutoka Chadema zaidi na kuweka nguvu kubwa kwenye majimbo yaliyokuwa chini ya Chadema huku mgombea urais na team yake wakitembea kila sehemu ya nchi hii kuinanga Chadema.
 
Kisasi cha Zitto kwa Chadema, Wakati Zitto anafukuzwa Chadema aliahidi kuhakikisha Chadema inakufa na alikula kiapo cha kuivuruga. Harakati za kuivuruga zilianza pale alipoanza kuituhumu Chadema ya kuwa ni chama cha kidini na Kikanda, Kuhakikisha anasajili kutoka Chadema zaidi na kuweka nguvu kubwa kwenye majimbo yaliyokuwa chini ya Chadema huku mgombea urais na team yake wakitembea kila sehemu ya nchi hii kuinanga Chadema.
Too late, Lisu ameshasajiliwa ACT wazalendo!
 
Mbona mnaweweseska sana Combo ya TL na Zitto inawatetemesha mno.

Chadema iko imara siku zote.
 
Akili hizi za kipimbi ndio zinatawala kwenye akili zenu?

Kwa kweli ukistaafu msafara wa magoti ikulu utaona ya uvccm walio watetezi wa chadema
 
Tumwamini nani chama mbadala?
Kisasi cha Zitto kwa Chadema, Wakati Zitto anafukuzwa Chadema aliahidi kuhakikisha Chadema inakufa na alikula kiapo cha kuivuruga. Harakati za kuivuruga zilianza pale alipoanza kuituhumu Chadema ya kuwa ni chama cha kidini na Kikanda, Kuhakikisha anasajili kutoka Chadema zaidi na kuweka nguvu kubwa kwenye majimbo yaliyokuwa chini ya Chadema huku mgombea urais na team yake wakitembea kila sehemu ya nchi hii kuinanga Chadema.
 
Kifaranga Lisu maneno ya Zito upande wa pili ni
Zito ni kibaraka tu maneno ya Lisu
Hawa tuwaache wajijenge ila KUAMINIANA kwao itakua mtihani
 
Si dhambi Lissu kukubaiana na philosophy ya Zitto as a person na si dhambi Lissu kufanya kazi na Zitto kama two young and generic politicians, na si dhambi pia Zitto kumtembelea mgonjwa hata akitaka kila wiki; Dhambi ni pale Zitto anaanza kuamua na kuweka hadharani mambo yanayomuhusu Lissu na chama chake ambayo Lissu hana mamlaka nayo.

Nina uhakika 100% kwamba Lissu ni Jembe, Jembe maana ni mwanasiasa MAKINI, MWEREVU na ana simamimia kile anachokiamini - sidhani kama anaweza ku sign mikataba ya kilaghai ili kuihujumu CDM hapana kwani yeye ni CHADEMA.

Mi naona hili jambo wala si kubwa hii bali linakuzwa kwa sababu maalum.
 
Kwani Lisu kuhamia ACT wazalendo ni kuihujumu Chadema?!..... Kivipi?
 
Kwanini Zitto anaonekana kuongelea sana masuala ya Lissu?

Yericko alisema.

1. Labda anataka kushinikiza kuingizwa ndani ya system ya Chadema.

2. Huenda anataka kujijenga ili aonekane ana nguvu kisha Ccm waone umuhimu wa kumtumia mwakani.
 
Kwani Lisu kuhamia ACT wazalendo ni kuihujumu Chadema?!..... Kivipi?
Nimekwambia Lissu atapigania haki na atalikomboa Taifa hili kupitia chama makini cha CHADEMA. Ni rahisi kwa Mwenyekiti wa CCM kuhamia ACT - Wazalendo kuliko kumshawishi Lissu.
 
Ni rahisi kwa Magufuli kujiunga na ACT kuliko Lissu kuwa mwanachama wa ACT.
Nyie vijana mnaomjua Lissu kupitia Facebook na mitandao mingine hamumjui Lissu ni binadamu wa aina gani. Na kabla ya siasa alikuwaje?
Kwani huyo Lisu hajawahi kuhama chama?!..... au siasa alianzia hapo Ufipa?

Lisu ameshasaini usajili wa ACT wazalendo!
 
Back
Top Bottom