Fahamu Sababu za Maumivu ya korodani na nini ufanye upatapo tatizo hili

JanguKamaJangu

JF-Expert Member
Feb 7, 2022
2,308
5,460
Wiki iliyopita tulieleza kwa urefu tatizo la kuvimba korodani, leo tunaendelea kufafanua tatizo hili na tutaeleza nini ufanye upatapo tatizo hili.

Ni kwamba ugonjwa unaoathiri korodani na kuifanya ivimbe, inaweza kusababishwa na bakteria au virusi.

Kutokana na maambukizi ya vimelea hivi bakteria na virusi huweza kusababisha kuathirika kwa korodani moja au zote mbili kwa wakati mmoja.

Lakini kabla ya kwenda mbali zaidi ni vizuri kukumbuka kwamba korodani kazi yake kubwa ni kuzalisha mbegu za kiume.

CHANZO CHA TATIZO
Chanzo kikubwa cha ugonjwa huu ni aina ya virusi vijulikanvyo kama ‘mups virus,’ kwa hiyo virusi hawa endapo watashambulia korodani husababisha korodani kuvimba na kupunguza utendaji kazi wake.

Maambukizi yanayotokana na vimelea (bacteria) inawezekana ni vimelea wanaosababisha tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) na magonjwa mengine ya zinaa kama Kaswende na Kisonono.

Kuumia kwa korodani, pengine inaweza kuwa chanzo ni ajali au michezo ya hatari, hali kama hiyo pia huweza kuchangia korodani kuvimba.

Maambukizi ya ‘epididymis’ ni chanzo kingine cha tatizo hili, ambapo ‘epididymis’ ni mrija ambao kazi yake ni kutunza mbegu za kiume baada ya kuzalishwa kutoka kwenye korodani.

Watu walio katika hatari ya kupata ugonjwa huu ni kama mtu hakupata chanjo ya kuzuia virusi aina ya ‘mumps’ basi mtu huyo atakuwa katika hatari kubwa ya kupata ugonjwa huu.
Kupata tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) mara kwa mara ni moja ya dalili za kuambukizwa bakteria hao.
Watu ambao hufanya mapenzi na watu tofauti tofauti mara kwa mara nao huwa katika hatari ya kupata tatizo hili.

Pia kufanya mapenzi na mtu mwenye magonjwa ya zinaa na kama mtu alishawahi kupata magonjwa ya zinaa pia yuko kwenye hatari ya kupata tatizo hili.

DALILI ZA KUATHIRIKA KWA UGONJWA HUU
Dalili za tatizo hilo ni pamoja na kuvimba kwa korodani moja au zote mbili, maumivu makali ya korodani, homa kali, kichefuchefu na hata kutapika na maumivu sehemu za mitoki.

MATIBABU YA TATIZO HILI
Matibabu ya ugonjwa huu hutegema na chanzo cha maambukizi kati ya bacteria au virusi kwa hiyo baada ya uchunguzi kubaini nini chanzo matibabu ndipo hufuatia na yanaweza kuanzia kwa kuua vimelea vilivyosababisha tatizo hilo kwa kutumia dawa.

Athari ambazo hujitokeza endapo mgonjwa atachelewa kupata matibabu
Kunywea kwa korodani moja au zote mbili pia kuwa na jipu au vijipu kwenye korodani ambalo limeathirika na maambukizi ya bakteria.

Mwanaume kupata utasa, hii ni kutokana na kuzalishwa ‘testosterone hormone’ kwa kiwango kidogo ambayo inasaidia uzalishaji wa mbegu za kiume

Pia mtu anaweza jkukumbwa na tatizo la upungufu wa nguvu za kiume.

NAMNA YA KUEPUKA UGONJWA HUU
·Wapenzi wawe na utaratibu wa kupima afya zao hususan magonjwa ya zinaa hasa kabla ya kushiriki tendo la ndoa.
Wapenzi ni muhimu kuzingatia matumizi ya kondomu wakati wa tendo la ndoa hususan kwa wale ambao hawajapima afya zao.

Pia kupata matibabu ya uhakika pale unapogundulika una tatizo la mkojo mchafu (U.T.I) au magonjwa ya zinaa.

Endapo utakuwa na miongoni mwa dalili hapo juu ni vizuri ukawahi hospitali kupata matibabu mapema baada ya kuchunguzwa na daktari.

Chanzo: Global Publishers
 
Back
Top Bottom