Fahamu njia zitumikazo Tanzania kupambana na janga la Corona

COARTEM

JF-Expert Member
Nov 26, 2013
3,526
2,000
Kumekuwa na upotoshwaji mwingi sana wa namna nchi yetu inavyopambana na janga hili la virusi vya corona. Upotoshwaji huu ni wa makusudi au ni wakutokufahamu nini kinaendelea ndani ya mfumo mzima wa sekta ya Afya.

Kiujumla Tanzania tunatumia njia zifuatazo.

1. Tiba ya kisayansi (modern medicine)
2. Tiba asilia (Traditional medicine)
3. Sayansi ya kujikinga na Magonjwa (Preventive medicine)
4. Maombi (Prayers) kwa wenye imani na MUNGU

TIBA YA KISAYANSI ( MODERN MEDICINE)
Ukienda kwenye hospitali zetu zote za serikali na binafsi, matibabu ya wagonjwa wa CORONA (COVID-19) yanatolewa kwa kutumia dawa za kitabibu.
Mfano.
Kwa mtu ambaye anadalili za kawaida anapewa.
1. Azithromycin
2. Artemether Lumefantrine (ALU)
3. Dexamethasone
4. Vitamin C
5. Zinc sulfate
6. Junior aspirin

Kwa mtu mwenye dalili mbaya
(Severe cases of covid-19)
1. Ceftriaxone salbactam
2. Ivermectin
3. Colchicine
4. Dexamethasone
5. Amoxiclav inj
6. Aminophylline
7. Vitamin C
8. Vitamin D
9. Zinc
Kwa mgonjwa mwenye dalili mbaya sana na anahitaji Oxygen atawekewa oxygen na dawa zake zinazotumika ICU.

TIBA ASILIA (TRADITIONAL MEDICINE)

Hii watu wengi hudhani ni tiba ya uchawi au ulozi.
Mtu mwenye CORONA anatumia tiba hizi asilia jumlisha na dawa za Hospitalini.

Ieleweke mpaka sasa mahospitalini kinachofanyika ni kutibu dalili na kuondoka CYTOKINES STORMS ambazo zimesababishwa na hawa virusi wa corona.

Tiba mbadala kwa vile haijulikani na wengi basi watu wanaibeza.

Pitia hapa kujifunza njia za Kujifukiza.

1. 7 natural ways to cleanse your lungs

2. Steam Inhalation: Cold, Sinuses, Procedure, Benefits, Cough, and

3. Warm Steam Inhalation before Bedtime Improved Sleep Quality in Adult Men

KINGA (PREVENTIVE MEDICINE)

1. Vaa barakoa kwenye mikusanyiko yote mikubwa ikiwemo misiba, mazishini, kwenye mabasi na daladala, mikutano nk nk.
2. Nawa mikono yako mara kwa mara kwa maji safi tirilika na sabuni.
3. Tumia sanitizer (vipukusi vya asilimia 60 na zaidi) mara kwa mara.
4. Usiguse macho, pua, mdomo kwa mikono ambayo ni michafu.
5. Acha kabisa tabia ya KUSALIMIANA KWA MIKONO.
6. Ukipata dalili za CORONA wahi haraka HOSPITALI ukapate matibabu, acha kabisa tabia ya kujisikilizia.

MAOMBI (PRAYERS)
Hili ni kwa wale watu ambao wanaamini MUNGU yupo.

Kwahiyo kwavile adui tuliyenaye ni msumbufu,kila silaha inabidi itumike kupambana naye.

Tuache upotoshaji
 

Mlenge

Verified Member
Oct 31, 2006
1,926
2,000
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom