Fahamu njia watumiazo wanawake waliosonga umri kuwapata wachumba kanisani

Habari JF mapenzi.

Wadada wengi waliosonga umri hupenda kutafuta attention kwenye mikusanyiko ikiwa ni pamoja na kanisani ili waonwe na wakaka au wababa wasioa. Njia hizi ni:

1. Kuchelewa kwenda kutoa sadaka, anaenda mwishoni huku watu wote wamemaliza ili kila mtu amwone.

2. Kuchelewa kushiriki Ekaristi takakatifu kwa wale wa Rc kwa minajili ileile anakuwa wa mwisho kabisa, akichelewa kidogo anaweza kukuta padri au sister anajiandaa kurudisha ekaristi iliyobaki.

3. Kuvaa nadhifu kabisa kama binti wa heshima na ikiwezekana nguo zibane mwili kama kaumbika, kama hajaumbika atavaa kadri ya mwili wake.

4. Amalizapo kutoa sadaka au kula ekaristi huja pole pole ktk kiti chake kwa mwendo wa madaha huku akiangaza macho kwa watu wa pande zote kanisani.

5. Huvaa miwani japo sio wote kuimarisha muonekano.

6. Humsalimia kila aliye jirani yake kanisani kwa sauti ya chini haswa vijana wa kiume kama ibada haijaanza

7. Aghalabu/Mara nyingi viatu vyao hutoa mshindo au kelele atembeapo.

8.Endelea.........

Na watumishi wa Mungu amnbao huwa wanapata nafasi ya kusimama madhabahuni unapokuwa kanisani kwenye Ibada nao unawajua vizuri pia kama unavyowajua akina mama hawa? Je ni mtumishi wa aina gani anapokuwa amesimama madhabahuni huwa unaondoka Kanisani ukiwa umebarikiwa to the maximum, yaani unabubujika upako? Nashauri uhangaike na kuwaona watumishi wa Mungu zaidi kanisani kama huwa unakwenda Kanisani kwa ajili ya Ibada, achana na milio ya viatu vya akina mama!
 
Mbinu kubwa nayowashauri mabinti kupata wenzi tena nyepesi kabisa ni kuhakikisha mama wa yule kijana unayempenda anafurahi fulls top.
 
Back
Top Bottom