Fahamu njia unazoweza kuzitumia ili kupata Mtaji wa Biashara

Big Phil

Member
Nov 20, 2019
50
338
Nifanyeje nipate mtaji? Nina wazo zuri ila sina mtaji? Haya ni maswali ambayo wengi wetu tunajiuliza sana kwenye harakati zetu za kila siku kwenye kutafuta maisha. Kuna njia ambazo tunaweza kuzitumia kupata mitaji ya kuanzisha biashara.

1. Akiba binafsi

Kuna msemo wa kiswahili unasema "Akiba haiozi" hivyo basi unaweza kutunza kiasi cha fedha unachokipa kama mtaji na kumbuka ndondoo si chururu unapoanza na kidogo ndo akili inakuwa na maarifa zaidi, anza na msingi mdogo ili ukue kwenye biashara na utaona mafanikio.

2. Kubadilisha mali na vitu binafsi

Watu wengi tumekuwa tunalalamika hatuna mitaji ila tunatumia simu za gharama sana iPhone, Samsung za mamilioni, laptops, tv na furniture ghali. Hakuna haja ya kuwa na vitu vyote hivyo kama huna mtaji ni heri ukauza na kuweka kwenye uwekezaji. Ni muhimu kuwekeza kuliko kuwa na maisha ya kifahari anasa.

3. Ndugu na marafiki

Kama una mahusiano mazuri na ndugu ama jamaa, kwanini unaona shida kuomba mtaji wa biashara?
Andaa wazo zuri la biashara (a concrete business plan) na waombe wakuwezeshe na jitahidi kurudisha mapema ili wakuamini

4. Taasisi za kuwezesha wajasiriamali

Hivi Leo kuna taasisi na mashirika mbalimbali yanayotoa mitaji na fedha na vifaa kwa wajasiriamali wadogo ili waweze kutekeleza mawazo yao. Halmashauri zina mifuko kwa ajili ya Ujasiriamali kwa vikundi vya vijana.

5. Mikopo ya taasisi za kifedha

Taasisi zinatoa mikopo kwa vijana na wajasiriamali wapya. Hii mikopo ya taasisi za kifedha inaweza kutumika kama mtaji mzuri sana wa biashara. Ila hii njia inapaswa uwe umejipanga na una mikakati mizuri ya biashara ambayo itakufanya uwe unarudisha rejesho hata kama biashara haiko sawa.

Naamini mpaka hapa tumepata mwanga kidogo wa njia gani tunaweza kupata mtaji kwa ajili ya kutekeleza wazo wa miradi wako.
Tunakumbushana tu kwamba mtaji sio kila kitu na wala kiasi cha pesa bali usimamizi na mikakati sahihi kwenye kila unachokifanya vitakuwezesha kukuza mtaji wako na kufikia malengo yako.

Je, wewe unafahamu njia nyingine ya kupata mtaji? Tafadhali andika hapo chini. Kisha washirikishe wengine makala hii ili vijana tuzidi kuinuana.
 
Naomba kujua hizo taasisi tafadhali
 
Kua muwazi wa hizo taasisi je inahitajika bond yoyote?. Mfano mimi nafanya issue ya Viatu Nina order ya pair kama 300 jumatatu lakini sina mtaji nimekwama nimeamua kutulia tu.
1. Akiba binafsi ni ngumu sana hasa graduate
2. Kubadilishana Mali na vitu binafsi, wengine hata sehemu ya kukaa hakuna tunamiliki tecno iliyopasuka kioo so ni ngumu wala hatuna assert yoyote
3. Marafiki na ndugu hawana msaada wowote
4.it sound good lakini hizo taasisi ziko wapi? Au ni zile vijana mnaanzisha kikundi? ...
 
Rahisi sana kuandika but practically ni lazima tupambane tu hamna namna...

KILA KITU KITAPANDA
 
Kua muwazi wa hizo taasisi je inahitajika bond yoyote?. Mfano mimi nafanya issue ya Viatu Nina order ya pair kama 300 jumatatu lakini sina mtaji nimekwama nimeamua kutulia tu.
1. Akiba binafsi ni ngumu sana hasa graduate
2. Kubadilishana Mali na vitu binafsi, wengine hata sehemu ya kukaa hakuna tunamiliki tecno iliyopasuka kioo so ni ngumu wala hatuna assert yoyote
3. Marafiki na ndugu hawana msaada wowote
4.it sound good lakini hizo taasisi ziko wapi? Au ni zile vijana mnaanzisha kikundi? ...
nakazia hapa
 
Nimepata external source lakini inanitaka nifike kule na kurudi tsh11million niwezesheni narudisha ndani ya miezi6
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom