Fahamu namna yakupambana na Adui kabla hajakudhuru

Showio

JF-Expert Member
May 16, 2019
255
481
SOMO : SHAMBULIA KAMBI YA ADUI KABLA HAJAKUSHAMBULIA.

"Mwe na kiasi na kukesha;kwa kuwa mshtaki wenu Ibilisi, kama simba angurumaye, huzunguka -zunguka, akitafuta mtu ammeze " 1Petro 5:8

"Maana yeye atakuokoa na na mtego wa mwindaji " Zaburi 91:3

■Kama una amani na hauombi basi usifikiri upo salama, Maana, Simba anayekutafuta akumeze bado hajakupata ,bado anaendelea kuzunguka huku na huku atakapo kupata atakumeza. Kama hauombi basi ujue mbele yako kuna mtego upo mbele yako,umetegwa ni kwamba bado tu kidogo utakunasa ndiyo Maana hamu ya kuomba haipo na unayo amani.

■Watu wengi wanakuwa na maombi hadi pale wanapokutana na mambo magumu maishani mwao. Na wakivuka hawana tena habari na maombi. Ila wakikutana tena na maombi hapo hutafuta namba za watumishi na wachungaji na hata wasio na dini utasikia "NIOMBEE NINAPITIA MAMBO MAGUMU " AU SHETANI AMEJIINUA.

■Shida ni kuwa unafikiri shetani hakutafuti wala hana habari na wewe, shetani ni kama anakulisha kama kuku mwisho wa siku umzalie matunda ya uovu anapokutenga na Mungu hadi ukashindwa kuomba na mwisho kabisa kwa kuwa umekula vyake ni kukuchinja kama kuku.

●Usione shetani kakaa kimya maishani mwako au haupitii vipindi vigumu, ujue haujaingia kwenye mitego yake. Kama usipojifunza kuitegua mitego yake anayoipanga na kuitega gizani na kwenye ulimwengu wa roho ipo siku utanaswa. Siyo kila amani ni njema. Ukiona hauombi na una amani basi hiyo amani ni ya adui.

●Wapo Watu wengi sana Leo wamedumbukia kwenye mitego ambayo wanajaribu kujinasua lakini wameshindwa na kila wakitaka kusonga mbele wanashindwa Wapo pale pale Maana wamenaswa Tayari.
Wengine mitego yao walitegwa kwenye ndoa, Wengine biashara, Wengine madeni, Wengine kwenye masomo, wengine kwenye uchumba, Wengine kazini kwao. N.k

NB:USISUBIRI MABAYA NA MAGUMU NDIPO UOMBE BALI INGIA KWENYE MAOMBI BOMOA, SAMBARATISHA KILA MTEGO WA ADUI NA MAWAZO YAKE JUU YAKO, TEGUA KILA MTEGO. UTAKUWA SALAMA.
 
Back
Top Bottom