Fahamu namna nzuri ya Mama Mjamzito kulala ili kulinda uhai wa Mtoto

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,500
9,279
Ujauzito ni mtihani mgumu maana anayoyapitia mwanamke ni mazito. Anashindwa wakati mwingine kula, kulala, kutembea yani kwa ujumla kuishi maisha yake ya kawaida kabla ya ujauzito wake ni changamoto na mtihani mkubwa.

Kikubwa sasa huwa atalalaje,hasa anapokuwa kileleni mwa ujauzito wake.Namna ya kulala pia huwa ni mtihani mkubwa. Yaani unapata uchovu ambao hata unatamani ujifungue tu wakati mwana bado.

Mojawapo ya mambo muhimu licha ya hali unayopambana nayo kama mjamzito ni ambavyo unalala hasa katika miezi mitatu ya mwisho ya ujauzito. Unaweza kulala kwa upande wako wa kulia na kushoto lakini chali?…hapana na hata usidhubutu.

Wataalamu wanafananisha kulala chali kwa mwanamke mjamzito na mtu ambaye amevuta sigara kumi kwa siku. Wanasema ni hatari kwa mtoto.

sleeping-mum-1024x536.jpg
Mwanamke anayelala chali humnyima mtoto wake Oxygen ya kutosha
Bila shaka taarifa hii ni ya kushangaza na imewagusa wengi.

Je mtu anayevuta sigara kumi kwa siku anakabiliwa na hatari gani?

Uvutaji sigara wakati una ujauziti sio tisho kubwa tu kwa mama bali pia kwa mtoto wake aliye tumboni. Madhara hayo humwathiri mtoto hata baada ya kuzaliwa.

‘Nicotine’ sumu inayomfanya mtu kuwa mraibu wa sigara, ‘Carbon Monoxide‘ na sumu nyinginezo zinazotokana na uvutaji wa sigara humfikia mtoto akiwa tumboni kupitia kwa mishipa ya damu.

Nicotine, hupunguza kiwango cha gesi ya Oxygen inayomfikia mama na mtoto wake.

Pia huongeza uwezekano wa mimba kutoka , mtoto kufia tumboni, uzani mdogo wa mtoto anapozaliwa na pia kupunguza kasi ya ukuwaji wa mtoto tumboni pamoja na kusababisha matatizo ya kupumua.

Je namna unavyolala kama mama mjamzito kunamwathiri vipi mtoto wako aliye tumboni kiasi cha kulinganshwa na uvutaji sigara?

Mama mjamzito anayekaribia kujifungua anapolala chali, hupunguza kiwango cha damu inayomfikia mtoto sawa na sigara inavyomwathiri mama mjamzito.

Pregnant-woman-asleep-on-her-side-474.jpg



Mwanamke anashauriwa kulala kwa upande wake wa kushoto au kulia
Hata hivyo, kulala chali kunasababisha mshipa mkubwa wa damu ulioko tumboni mwa mama kufinywa kutokana na tumbo kubwa ya ujauzito.

Wanasayansi wametangaza taarifa hii baada ya kufanya utafiti uliowahusisha wanawake wajawazito 1,760 kutoka Uingereza ,New Zealand na Australia.

Wanawake ambao mimba yao ipo Zaidi ya wiki 28, walihojiwa kuhusu namna ambavyo wao hulala.

Watafiti wakagundua kuwa jumla ya uzani wa Watoto waliozaliwa na wanawake ambao hulala chali ilikuwa kilo 3.4.

Uzani wa Watoto waliozaliwa na wanawake wajawazito wanaolala kwa upande wao ni kilo 3.55…..ukiwa juu kwa gramu 144 ikilinganishwa na Watoto wa wanwake wanaolala chali wanapokuwa wajawazito.

anti-smoking-during-pregnancy-message-smoking-belly-small-13759.jpg



Mwanamke anayelala chali yuko sawa tu na mwanamke anayevuta sigara wakati ni mjamzito

Hii ni sawa na hali inayotokea kwa wamwake wanaovuta sigara wakiwa wajawazito. Kwa kila Watoto watanao wanaozaliwa na wanawake wanaovuta sigara wakiwa wajawazito, mmoja wa Watoto hao huzaliwa akiwa na uzani mdogo sana.

Profesa Lesley McCowan, kinara wa idara ya afya ya uzazi katika chou kikuu cha Auckland,Australia amesema kuwa, wanawake hawapaswi kuwa na hofu kwani wanaweza kubadili namna wanavyolala nyakati za usiku.

Aliongeza kwamba utafiti huu ni kumbusho tu kwa wanawake kwamba waangalie namna wanavyolala kwa ajili ya afya ya watoto wao na ili kupunguza idadi ya vifo vya Watoto wakiwa tumboni.
 
Aiseee hamna changamoto kubwa kama ya kulala hasa siku za mwisho. Mungu atubariki kina mama wote
 
Back
Top Bottom