Fahamu namna kuku anavyotumika kwenye kuroga na kuponya watu

Bujibuji Simba Nyamaume

JF-Expert Member
Feb 4, 2009
74,692
155,120
MAKOROKOCHO MARKET 🇹🇿

FAHAMU JINSI KUKU ANAVYOTUMIKA KATIKA ULIMWENGU WA GIZA MBALI NA KITOWEO.

Wengi wetu tunamtambua kuku ni kama ndege afugwaye na watu wengi na kutumika kama kitoweo, kutoa mayai ukiuza unapata pesa lakini kumbe kuna siri kubwa ambayo ndege huyu Mungu amemuumbia nazo pasipo watu wengi kuzijua zenye faida kibao kwa mwanadamu, kivipi? Hebu nifuate.....

Kuku huyu yupo katika jinsia mbili kama viumbe wengine yaani Jogoo na Koo ila hapa nieleweke kuku ninaemsemea hapa ni kienyeji na si hao wanyama,mayai au aina nyingine mbali na hiyo.

Leo nitakupa faida za jinsia hizi mbili katika maisha ya mwanadamu kiafya kupambana na matatizo mbalimbali yatokanayo na nguvu za Giza pamoja na kujiletea manufaa ya kimaisha.

1.JOGOO;
Hii ni jinsia ya kuku wa kiume ambaye ana mambo mengi ya ajabu, kwanza Jogoo mweupe hutumika kama tulizo la magonjwa yote ya kichawi kwa mtu sababu amebeba nguvu ya uzima ndani yake.
Ukichukua ile nyama yake ya kichwani ambayo ipo kama upanga na kuchanganya na dawa husika basi inauwezo wa kuita kimbunga cha katrina, mbegu zake hutumika kutengeneza dawa kali kabisa ya nguvu za kiume hii ndiyo walikua wakitumia machifu hapo zamani na kuwa na uwezo wa kumiliki wake zaidi ya kumi hivyo ukiwa na dawa hii ni lazima uwe na wanawake wa kutosha.
Nyoya lake hutumika kutibia ugonjwa wa ndimi mbili, ubongo wake hutumika kutoa taarifa kwa njia ya njozi au kujua endapo mbaya wako anakuandama tena ndani ya wakati kama jinsi yeye atambuapo masaa na kuwika.
Mshipa wake wa shingoni hutumika kutibia matatizo ya ganzi mwilini
Jicho lake hutumika kuona chochote kisichoonekana katika hali ya kawaida kama kuona wachawi, misukule au chuma ulete akija kwenye biashara yako.
Pia Jogoo mweusi hutumika katika mazindiko ya kuficha mali, pesa au nyumba na wewe mwenyewe usionekane na mchawi au jambazi.

2.KOO

Huyu hutumika katika kufungua kizazi au mwanamke alie tasa kuzaa ila kwa kulogwa tu husaidia huyo mtu kuzaa,
Pia hutumika kufungia mimba zinazoporomoka au kudondoka
Mayai yake hutumika kumfungua mtu aliyefungwa kichawi yaani nuksi, pia yai lake ambalo ni viza hutumika kusambaratisha ubaya wa adui au kumrudishia ubaya wake.
Lakini pia kuku ndio kafara kubwa itumikayo kama ufunguo wa kufungulia ulimwengu wa Giza yaani kuita mizimu, majini, na kuwatuma utakacho ila hapa itategemea na moyo wako umekusudia kuwatuma kwa ubaya au jambo zuri.

Mambo ni mengi ila kwa leo niishie hapa. Sio kila unachosoma mtandaoni kina ukweli, vingine ni magirini na miyeyusho, unalainishwa ili upigwe.

NAWATAKIA HERI YA NOELI NA MWAKA MPYA.
 
Kuku hutumiwa na waganga wa kienyeji kupigia ramli kwa wateja wao.

Ramli chonganishi husababisha chuki, visasi na hata mauaji kwa ndugu, jamaa na jamii kwa ujumla.
 
Jamani Bujibuji mbona mambo mengi, halafu mwaka mpya tule nini sasa?
 
Huyo kuku ni wa kienyeji au boiler?

Vipi kuhusu dagaa mbona huwa hawahitajiki?
 
MAKOROKOCHO MARKET

FAHAMU JINSI KUKU ANAVYOTUMIKA KATIKA ULIMWENGU WA GIZA MBALI NA KITOWEO.

Wengi wetu tunamtambua kuku ni kama ndege afugwaye na watu wengi na kutumika kama kitoweo, kutoa mayai ukiuza unapata pesa lakini kumbe kuna siri kubwa ambayo ndege huyu Mungu amemuumbia nazo pasipo watu wengi kuzijua zenye faida kibao kwa mwanadamu, kivipi? Hebu nifuate.....

Kuku huyu yupo katika jinsia mbili kama viumbe wengine yaani Jogoo na Koo ila hapa nieleweke kuku ninaemsemea hapa ni kienyeji na si hao wanyama,mayai au aina nyingine mbali na hiyo.

Leo nitakupa faida za jinsia hizi mbili katika maisha ya mwanadamu kiafya kupambana na matatizo mbalimbali yatokanayo na nguvu za Giza pamoja na kujiletea manufaa ya kimaisha.

1.JOGOO;
Hii ni jinsia ya kuku wa kiume ambaye ana mambo mengi ya ajabu, kwanza Jogoo mweupe hutumika kama tulizo la magonjwa yote ya kichawi kwa mtu sababu amebeba nguvu ya uzima ndani yake.
Ukichukua ile nyama yake ya kichwani ambayo ipo kama upanga na kuchanganya na dawa husika basi inauwezo wa kuita kimbunga cha katrina, mbegu zake hutumika kutengeneza dawa kali kabisa ya nguvu za kiume hii ndiyo walikua wakitumia machifu hapo zamani na kuwa na uwezo wa kumiliki wake zaidi ya kumi hivyo ukiwa na dawa hii ni lazima uwe na wanawake wa kutosha.
Nyoya lake hutumika kutibia ugonjwa wa ndimi mbili, ubongo wake hutumika kutoa taarifa kwa njia ya njozi au kujua endapo mbaya wako anakuandama tena ndani ya wakati kama jinsi yeye atambuapo masaa na kuwika.
Mshipa wake wa shingoni hutumika kutibia matatizo ya ganzi mwilini
Jicho lake hutumika kuona chochote kisichoonekana katika hali ya kawaida kama kuona wachawi, misukule au chuma ulete akija kwenye biashara yako.
Pia Jogoo mweusi hutumika katika mazindiko ya kuficha mali, pesa au nyumba na wewe mwenyewe usionekane na mchawi au jambazi.

2.KOO

Huyu hutumika katika kufungua kizazi au mwanamke alie tasa kuzaa ila kwa kulogwa tu husaidia huyo mtu kuzaa,
Pia hutumika kufungia mimba zinazoporomoka au kudondoka
Mayai yake hutumika kumfungua mtu aliyefungwa kichawi yaani nuksi, pia yai lake ambalo ni viza hutumika kusambaratisha ubaya wa adui au kumrudishia ubaya wake.
Lakini pia kuku ndio kafara kubwa itumikayo kama ufunguo wa kufungulia ulimwengu wa Giza yaani kuita mizimu, majini, na kuwatuma utakacho ila hapa itategemea na moyo wako umekusudia kuwatuma kwa ubaya au jambo zuri.

Mambo ni mengi ila kwa leo niishie hapa. Sio kila unachosoma mtandaoni kina ukweli, vingine ni magirini na miyeyusho, unalainishwa ili upigwe.

NAWATAKIA HERI YA NOELI NA MWAKA MPYA.
Wafanya biashara wa kuku wa kienyeji naona mnatafuta kisingizio cha kupandisha bei ya kuku msimu huu wa sikukuu.
 
Elimu ya asili ni pana sana,haya yote sikuyajua hapo mwanzo.
Shukrani kwa elimu.
Buji kama Buji.
 
Unaharibu, si tungepata hata wawili mmoja uniuzie nusu bei.
Tutawapata tu. Si unajua kuku anaongeza sperm count, anarudisha siku za wanawake ambao hawaonagi siku zao, pia kwa wale walio blidi muda mrefu kuku anabalance hormones na kufanya mwanamke apate siku zake kama kawaida.
Pia kwa wale ambao hawajapata watoto, Kuna dawa maalum inasaidia sana kwenye kurutubisha yai la mama
 
Naomba utofauti wa nguvu ya damu na aina ya kiumbe kwenye ulimwengu huu wa giza .

Mfano nguvu ya damu ya kuku against nguvu ya damu ya mbuzi
 
MAKOROKOCHO MARKET

FAHAMU JINSI KUKU ANAVYOTUMIKA KATIKA ULIMWENGU WA GIZA MBALI NA KITOWEO.

Wengi wetu tunamtambua kuku ni kama ndege afugwaye na watu wengi na kutumika kama kitoweo, kutoa mayai ukiuza unapata pesa lakini kumbe kuna siri kubwa ambayo ndege huyu Mungu amemuumbia nazo pasipo watu wengi kuzijua zenye faida kibao kwa mwanadamu, kivipi? Hebu nifuate.....

Kuku huyu yupo katika jinsia mbili kama viumbe wengine yaani Jogoo na Koo ila hapa nieleweke kuku ninaemsemea hapa ni kienyeji na si hao wanyama,mayai au aina nyingine mbali na hiyo.

Leo nitakupa faida za jinsia hizi mbili katika maisha ya mwanadamu kiafya kupambana na matatizo mbalimbali yatokanayo na nguvu za Giza pamoja na kujiletea manufaa ya kimaisha.

1.JOGOO;
Hii ni jinsia ya kuku wa kiume ambaye ana mambo mengi ya ajabu, kwanza Jogoo mweupe hutumika kama tulizo la magonjwa yote ya kichawi kwa mtu sababu amebeba nguvu ya uzima ndani yake.
Ukichukua ile nyama yake ya kichwani ambayo ipo kama upanga na kuchanganya na dawa husika basi inauwezo wa kuita kimbunga cha katrina, mbegu zake hutumika kutengeneza dawa kali kabisa ya nguvu za kiume hii ndiyo walikua wakitumia machifu hapo zamani na kuwa na uwezo wa kumiliki wake zaidi ya kumi hivyo ukiwa na dawa hii ni lazima uwe na wanawake wa kutosha.
Nyoya lake hutumika kutibia ugonjwa wa ndimi mbili, ubongo wake hutumika kutoa taarifa kwa njia ya njozi au kujua endapo mbaya wako anakuandama tena ndani ya wakati kama jinsi yeye atambuapo masaa na kuwika.
Mshipa wake wa shingoni hutumika kutibia matatizo ya ganzi mwilini
Jicho lake hutumika kuona chochote kisichoonekana katika hali ya kawaida kama kuona wachawi, misukule au chuma ulete akija kwenye biashara yako.
Pia Jogoo mweusi hutumika katika mazindiko ya kuficha mali, pesa au nyumba na wewe mwenyewe usionekane na mchawi au jambazi.

2.KOO

Huyu hutumika katika kufungua kizazi au mwanamke alie tasa kuzaa ila kwa kulogwa tu husaidia huyo mtu kuzaa,
Pia hutumika kufungia mimba zinazoporomoka au kudondoka
Mayai yake hutumika kumfungua mtu aliyefungwa kichawi yaani nuksi, pia yai lake ambalo ni viza hutumika kusambaratisha ubaya wa adui au kumrudishia ubaya wake.
Lakini pia kuku ndio kafara kubwa itumikayo kama ufunguo wa kufungulia ulimwengu wa Giza yaani kuita mizimu, majini, na kuwatuma utakacho ila hapa itategemea na moyo wako umekusudia kuwatuma kwa ubaya au jambo zuri.

Mambo ni mengi ila kwa leo niishie hapa. Sio kila unachosoma mtandaoni kina ukweli, vingine ni magirini na miyeyusho, unalainishwa ili upigwe.

NAWATAKIA HERI YA NOELI NA MWAKA MPYA.
We rafiki utasababisha kuku wapande bei....
 
Inawezekana.
Kwa wanaotaka utajiri wa ndagu, huchukuliwa jogoo mweusi asiye na doa hata moja. Kisha anayetaka utajiri hutamkishwa maneno fulani ambayo Ni spil, Kisha huambiwa amchinje huyo kuku, na muda huo akiwa anachinja, kule kwake, Yule mtoto wake anayempenda sana ataanza kulalamika kuwa kichwa kinamuuma, na baada ya siku moja atakufa.
Mi na walokole tunakushukuru Sana kwa maelezo haya
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom