JamiiTalks
JF Advocacy Team
- Aug 7, 2018
- 625
- 938
Kwa mujibu wa Kanuni za Uchaguzi za 2020 Kifungu cha 68 kifungu kidogo cha kwanza; Tume ya Uchaguzi baada ya kupokea matokeo ya awali ya Urais yatayoletwa kwao na wasimamizi wa Uchaguzi, baada ya kuhakiki itatangaza matokeo ya Urais kwa Jimbo husika.
Kifungu kidogo cha pili kinaeleza kuwa Tume kabla ya kupokea matokeo ya awali ya Urais kutoka kwenye majimbo yote inatakiwa kuvitaarifu Vyama vya Siasa au Wagombea wanaohusika juu ya tarehe, muda na sehemu ya kujumlishia kura.
Aidha kifungu kidogo cha tatu kinaeleza kuwa, Tume itajumlisha kura zote za awali za urais za kila mgombea zilizoletwa kwao na wasimamizi wa Uchaguzi.
Kifungu kidogo cha nne kinaeleza kuwa Tume baada ya kujumlisha kura zote za awali itafanya yafuatayo:-
(a) Itarekodi Matokeo hayo kwenye fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Urais ( fomu No. 27) kama ilivyoelezwa katika taratibu
(b) Itaazimia mgombea mwenye kura nyingi kuwa Rais mteule
(c) Itatoa fomu ya matokeo ya uchaguzi wa urais (fomu No. 27) kwa kila mgombea au wakala wake
(d) Itaonesha Nakala ya fomu ya Matokeo ya Uchaguzi wa Urais (fomu no. 27) katika mbao za matangazo za Ofisi za Tume.
Tume mara baada ya kuazimia Matokeo chini ya Kanuni hizi itatoa cheti kwa mgombea aliyechaguliwa kikionesha yafuatayo:
a) Jina kamili la mgombea aliyechaguliwa
b) Tarehe ya Uchaguzi
c) Wadhifa alioupata mgombea huyo, na
d) Sahihi ya Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti wa Tume