Fahamu mbinu za kumrekebisha mtoto mkorofi

MMASSY

JF-Expert Member
Jan 13, 2011
290
193
Na Jerome Mmassy, Arusha

Moja ya changamoto jamii inayokumbana nayo nyakati hizi katika malezi na makuzi ya watoto ni watoto kuwa wakorofi na wasiotii kile wanachoambiwa.Na pengine wazazi ama walezi wamekuwa wakitamani sana watoto wao wawe kama wao walivyokuwa miaka ya 1970/1980.

Ni vyema kutambua kuwa dunia inabidilika kwa kasi sana,ni hatari zaidi kutaka kumela mtoto kama tulivyolelewa sisi miaka ya nyuma.Kuanzia miaka ya 1990 jamii imekuwa ikipambana kuwalelea watoto kata walivyolelewa wazazi wao lakini malezi hayo yameshindikana na sasa hivi tunashuhudia jamii hyenye vijana wakorofi,wanaotumia madawa ya kulevya na wasioambilika.

Hayo yote ni matunda ya kuwalelea watoto kwa kufuata mambo ya jana.Wenzetu katika ulimwengu ulioendelea wanawalelea watoto wao kwa ulimwengu wa kesho sio wa jana.

Hivyo ni vyema nasi kubadili mitazamo yetu kwenye malezi ya watoto ili malezi na mafundisho tunayowapa yaendane na dunia ya leo na kesho.

Maana ya mtoto Mkorofi

Pengine una mtoto unayefikiri ameshindikana. Unamwita mtundu, mtukutu, asiyeambilika, mbishi, mkaidi na wakati mwingine unamwita majina mengine. Ilimradi tu ni tabia yake ya kupenda kushindana na kutotii kile anachoelekezwa. Katika makala hii tunamwita mtoto mkorofi. Huyu ni mtoto anayeweza kukukatalia kitu bila kupepesa macho na ukajikuta ukifedheheka tena mbele ya watu wanaokuheshimu sana katika jamii.

Mtoto wa namna hii unaweza kumwagiza afanye kitu na akabaki akikuangalia. Hajigusi. Wakati mwingine ni mtoto mwepesi kurusha rusha mikono na viungo vingine vya mwili kama namna ya kupinga unachomwelekeza. Anapoamua jambo, anakuwa na msimamo imara. Ukimlazimisha kufanya asichokitaka yeye unaambulia vilio na vurugu.

Mtoto wa namna hii pia huwa mgomvi anapokuwa na wenzake na mara nyingi utapata mashtaka kutoka kwa wenzake. Tabia yake ya kushindana na kila anayekuwa naye inamfanya ajikute kwenye migogoro ya mara kwa mara na wenzake.

Mbali na kusumbuana naye awapo hapo nyumbani, inawezekana pia ni msumbufu hata shuleni,kanisani ama msikitini. Pengine umepokea malalamiko kwa walimu wake kuwa hafanyi kazi anazopewa, hatulii darasani na muda mwingi anautumia kugombana na wenzake bila sababu za msingi. Mara nyingi watoto kama hawa huwa na matokeo mabaya shuleni.

Pia, ukorofi unakwenda sambamba na tabia ya kupenda kujiona ni mtawala anapokuwa na wenzake. Anaweza kuwa mwongeaji au mkimya lakini anafurahia kuona wenzake wakifanya kile anachokitaka yeye. Ni aina fulani ya hulka ya uongozi iliyochanyikana na kutokuelewa wengine wanataka nini. Na hali hii kitaalamu inaitwa Upofu wa hisia.

Ni vizuri kutambua kuwa si kila ubishi ni ukorofi. Kila mtoto kwa wakati fulani hujaribu kupigana na maagizo ya mzazi. Ubishi ni sehemu ya udadisi wa mtoto hasa pale anapofikiri kile anachoambiwa hakiendani na anachotamani. Usichukulie kuulizwa maswali mengi na mwanao kama ubishi au ukorofi. Mtoto mwenye akili nzuri mara nyingi hapokei kirahisi kile anachoambiwa bila kukitafakari.

Ingawa kila mwanadamu anahitaji kiasi fulani cha ukorofi kwa maana ya msimamo wa kile tunachokiamini, tabia hii ya misimamo inayoongozwa na upofu ikiachwa kumea inaweza kuwa kikwazo kwa mafanikio ya mtoto wako.

Ukubwani, ukorofi unahatarisha na hata kuvunja uhusiano baina ya watu. Unapokuwa mtu mkorofi, huwezi kujisikia hatia kumwumiza mwezako. Tena wakati mwingine furaha yako inaweza kuwa kuona wenzako wanaumia. Hakuna mzazi wala jamii inayotamani kukuza mtu wa namna hii.

Mara nyingi ukorofi wa mtoto ni ujumbe. Ni muhimu uuelewe ujumbe huu kabla hujachukua hatua za kuushughulikia. Ukorofi ni lugha ya kusema ndani anajisikia utupu. Ni sawa na mtu aliyeshinda njaa siku kadhaa. Kwa vyovyote vile ni dhahiri atakosa utulivu. Mwili wake unahitaji chakula.

Mtoto mkorofi kimsingi anaamini watu wanaomzunguka hawajatambua nafasi yake ipasavyo. Kuna sauti inatoka ndani yake na anaisikia yeye tu inayomwaminisha kuwa hatambuliki. Imani hiyo potofu huchochea jitihada za kutafuta kutambulika kwa namna isiyofaa.

Ubishi na ukaidi anaoufanya mtoto wakati mwingine bila hata yeye kutambua ni namna ya kujirudishia mamlaka anayoamini hana. Anapobishana na mzazi, anapogombana na wenzake, kimsingi anajaribu kujirejeshea ushawishi ambao anaamini hana.

Mambo mengi yanaweza kuzaa ukorofi. Baadhi ya wanasaikolojia wanaamini mtu huzaliwa na ukorofi na haw ani wale wanaoamini pia katika urithi wa jenetiki. Inawezekana. Lakini kwa sehemu kubwa tafiti zinaonyesha kuwa ukorofi ni zao la malezi.

Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia. Kwanza, inawezekana kwa sababu ya kutamani mtoto ‘anyooke’ umekuwa na unatumia sheria kali mno. Unaamini mtoto hawezi kufanya kitu bila kuamrishwa. Kwa sababu ya kuamini hivyo, umejikuta ukijenga mazingira ya mapambano yasiyo na sababu mtoto. Mtoto mkorofi ni ama anakuiga vile ulivyo au basi anapambana na wewe kwa kuwa wakati mwingi tunaamini tabia yam toto/mtu yaweza kuwa matokeo ya vile anavyoona anatendewa na uoande wa pili.Yaani tabia ya mtu wakati mwingine ni matokeo ya namna aanavyotendewa.

Lakini pili, inawezekana una ukali uliopitiliza. Huwezi kuongea bila kufoka na kupaza sauti. Huna sauti ya upole inayoleta taswira ya mtu mwelewa, anayejali, na mtulivu. Unaamini bila kelele hakuna nidhamu.

Pengine, inawezekana mtoto amekuwa akishuhudia vitendo vya ukorofi katika mazingira ya familia au kwa jirani zako. Kwa kawaida, watoto wananasa kwa haraka sana mambo yanayogusa hisia zao. Wanapoona mtu mzima anafanya jambo fulani na watu anaowaamini wanalichukulia kawaida, wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya kile kile wakati fulani.

Unawezaje kumrekebisha mtoto?

Jambo la kuzingatia ni kuwa ukali na mapambano yanakomaza ukorofi. Badilika na amua kuwekeza katika kujenga urafiki kabla hujatarajia kusikilizwa. Hapa sizungumzii urafiki wa siku mbili au tatu. Hapana. Ninamaanisha urafiki wa kudumu ambao mtoto hatakuwa na sababu ya kuwa na mashaka nao. Kama tulivyoona, mtoto mkorofi kimsingi anahitaji uhusiano wa karibu na wewe mzazi kuliko hata mtu mwingine yeyote yule.

Hata katikati ya urafiki huo, usishangae mwanzoni bado mtoto akaendelea kuwa mkaidi vile vile. Jambo la msingi hapa ni kutokata tamaa. Mpe nafasi ya kukuamini kwa kujenga urafiki imara. Sambamba na urafiki, punguza amri na kelele zisizo za lazima. Kumbuka kuwa amri bila urafiki huchochea uasi.

Jitahidi sana kujenga tabia ya mazungumzo ya utulivu unaposhughulika naye. Badala ya kuagiza, jaribu kushirikiana naye. Mwonyeshe kuwa unajali na kuthamini kile anachokipenda. Huna sababu ya kushindana naye. Katika mazungumzo, mpe nafasi ya kusema. Mwache aongee yaliyoujaza moyo wake na usiwe mwepesi kukosoa hisia zake wala kujitetea. Kumbuka kuwa ukorofi wake unatokana na kujisikia kutokueleweka kama nilivyoeleza hapo awali.

Mpe uzingativu kwa kuacha shughuli unazofanya kwa ajili yake. Ushirikiano wa kiwango hiki utamchangamsha. Ukiweza kufanya hivi bila mara kwa mara mtoto ataanza kukuamini na kidogo kidogo atabadilika.

Kadhalika, mheshimu kama mtu mwingine yeyote unayemheshimu. Heshima ina mambo mengi. Usimdhalilishe mbele ya wenzake kwa maneno au vitendo. Kama kuna sababu ya kumwadhibu, fanya hivyo kwa staha. Kumheshimu mtoto hakukuondolei mamlaka yako kama mzazi.

Jitahidi sana kutengenza mazingira ya kufanya maamuzi shirikishi yanayoheshimu matakwa yake. Kwa sababu tayari ana ukorofi, mweke karibu unapotaka atekeleze jambo. Badala ya kumwambia ‘kafanye,’ badili lugha iwe, ‘tufanye’ hata kama hulazimiki kufanya. Inapobidi, hasa kwenye hatua za mwanzo, shirikiana nae kufanya hicho unachotaka akifanye.

Vile vile, tambua kizuri kipya anachojifunza. Kama, kwa mfano, ameweza kuacha kubishana unapomwagiza kufanya kitu, usikae kimya. Tambua mabadiliko hayo hata kama ni madogo. Fahari ya mtoto ni kuona jitihada zake zinatambuliwa. Kadri unavyomfanya ajisikie kutambuliwa, ataendelea kufanya bidii ya kukupendeza na hatimaye ukorofi aliokuwa nao utapungua.

Jerome Mmassy

Mmassyfm@hotmail.com
 
HATA MAANDIKO YANASEMA USIMNYIME FIMBO TENA ZA KUTOSHA MTOTO MKOROFI NA WAHENGA WALISEMA MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAVYO, KUNA SEHEM ULIKOSEA MWANZONI
 
Hivi ndugu unafaham maana ya "keleb"? Ntakufafanulia. Keleb ni lile kofi la kiafrika ambalo linafungua na kuufunga ukorofi mazima. Trust me hata kawe na kiburi vipi, akikutana na keleb moja mjarabu, huo ukorofi utakimbia kama mbwa aliebana mkia sehem nyeti.
Wat you are saing might be right to some extent, lakini kaa ukijua nadharia hii imetoka kwa wenzetu wazungu, na ni rahisi kwa wao kuipractice kwa sababu wamekua tangu wadogo wakiiona. Kwa sisi wabongo sasa hivi hii ni changamoto kwa sababu moja kuu, mtu aliezaliwa before 2000, amekulia kwenye utii uliokithiri mixer mapigo mbalimbali a.k.a viboko, lakini mtu huyu huyu mtoto anaemzaa lets say mwaka 2022, anakulia kwenye dunia ya utandawazi, so mtazamo ni tofauti. Ujue mzaz analea mtoto subconsciously kuendana na jinsi alivolelewa, so kublend mtazamo wa pre internet era na huu wa utandawazi, lazma kuna sehem ya kukwama.
Psychologically, umri wa 1 to 6 yrs ndo mtoto anajengwa for life time. So mayb kama unataka kuinstill this way of thinking do it kipindi hicho. But kaa ukijua mtoto anafuata unayofanya rather than unachosema.
 
Kumbuka kuwa amri bila urafiki huchochea uasi.
Amri na urafiki ni vitu viwili tofauti,, Mtoto hatakiwi kuwa rafiki yako,, anatakiwa kuwa mtoto wako... Unatakiwa ku act kama mzazi na sio Rafiki... Jua kutofautisha mzazi na rafiki...

Jamii yetu ya kiafrika haijakaa kumpokea mtoto aliyelelewa kama Rafiki na mzazi wake.... huo ulezi wa urafiki ndio unaleta haya unayoona leo.

Kadhalika, mheshimu kama mtu mwingine yeyote unayemheshimu. Heshima ina mambo mengi. Usimdhalilishe mbele ya wenzake kwa maneno au vitendo. Kama kuna sababu ya kumwadhibu, fanya hivyo kwa staha. Kumheshimu mtoto hakukuondolei mamlaka yako kama mzazi.
Hili upo sahihi,, na hata wazazi wetu walilifanya hili ndio maana ilikuwa huwezi kupigwa mbele ya wageni,,kama ni mkubwa basi huwez kula kichapo mbele za wadogo zako,, uliitwa chemba then unachezea unarudi unalia tu..
 
Na Jerome Mmassy, Arusha

Moja ya changamoto jamii inayokumbana nayo nyakati hizi katika malezi na makuzi ya watoto ni watoto kuwa wakorofi na wasiotii kile wanachoambiwa.Na pengine wazazi ama walezi wamekuwa wakitamani sana watoto wao wawe kama wao walivyokuwa miaka ya 1970/1980.

Ni vyema kutambua kuwa dunia inabidilika kwa kasi sana,ni hatari zaidi kutaka kumela mtoto kama tulivyolelewa sisi miaka ya nyuma.Kuanzia miaka ya 1990 jamii imekuwa ikipambana kuwalelea watoto kata walivyolelewa wazazi wao lakini malezi hayo yameshindikana na sasa hivi tunashuhudia jamii hyenye vijana wakorofi,wanaotumia madawa ya kulevya na wasioambilika.

Hayo yote ni matunda ya kuwalelea watoto kwa kufuata mambo ya jana.Wenzetu katika ulimwengu ulioendelea wanawalelea watoto wao kwa ulimwengu wa kesho sio wa jana.

Hivyo ni vyema nasi kubadili mitazamo yetu kwenye malezi ya watoto ili malezi na mafundisho tunayowapa yaendane na dunia ya leo na kesho.

Maana ya mtoto Mkorofi

Pengine una mtoto unayefikiri ameshindikana. Unamwita mtundu, mtukutu, asiyeambilika, mbishi, mkaidi na wakati mwingine unamwita majina mengine. Ilimradi tu ni tabia yake ya kupenda kushindana na kutotii kile anachoelekezwa. Katika makala hii tunamwita mtoto mkorofi. Huyu ni mtoto anayeweza kukukatalia kitu bila kupepesa macho na ukajikuta ukifedheheka tena mbele ya watu wanaokuheshimu sana katika jamii.

Mtoto wa namna hii unaweza kumwagiza afanye kitu na akabaki akikuangalia. Hajigusi. Wakati mwingine ni mtoto mwepesi kurusha rusha mikono na viungo vingine vya mwili kama namna ya kupinga unachomwelekeza. Anapoamua jambo, anakuwa na msimamo imara. Ukimlazimisha kufanya asichokitaka yeye unaambulia vilio na vurugu.

Mtoto wa namna hii pia huwa mgomvi anapokuwa na wenzake na mara nyingi utapata mashtaka kutoka kwa wenzake. Tabia yake ya kushindana na kila anayekuwa naye inamfanya ajikute kwenye migogoro ya mara kwa mara na wenzake.

Mbali na kusumbuana naye awapo hapo nyumbani, inawezekana pia ni msumbufu hata shuleni,kanisani ama msikitini. Pengine umepokea malalamiko kwa walimu wake kuwa hafanyi kazi anazopewa, hatulii darasani na muda mwingi anautumia kugombana na wenzake bila sababu za msingi. Mara nyingi watoto kama hawa huwa na matokeo mabaya shuleni.

Pia, ukorofi unakwenda sambamba na tabia ya kupenda kujiona ni mtawala anapokuwa na wenzake. Anaweza kuwa mwongeaji au mkimya lakini anafurahia kuona wenzake wakifanya kile anachokitaka yeye. Ni aina fulani ya hulka ya uongozi iliyochanyikana na kutokuelewa wengine wanataka nini. Na hali hii kitaalamu inaitwa Upofu wa hisia.

Ni vizuri kutambua kuwa si kila ubishi ni ukorofi. Kila mtoto kwa wakati fulani hujaribu kupigana na maagizo ya mzazi. Ubishi ni sehemu ya udadisi wa mtoto hasa pale anapofikiri kile anachoambiwa hakiendani na anachotamani. Usichukulie kuulizwa maswali mengi na mwanao kama ubishi au ukorofi. Mtoto mwenye akili nzuri mara nyingi hapokei kirahisi kile anachoambiwa bila kukitafakari.

Ingawa kila mwanadamu anahitaji kiasi fulani cha ukorofi kwa maana ya msimamo wa kile tunachokiamini, tabia hii ya misimamo inayoongozwa na upofu ikiachwa kumea inaweza kuwa kikwazo kwa mafanikio ya mtoto wako.

Ukubwani, ukorofi unahatarisha na hata kuvunja uhusiano baina ya watu. Unapokuwa mtu mkorofi, huwezi kujisikia hatia kumwumiza mwezako. Tena wakati mwingine furaha yako inaweza kuwa kuona wenzako wanaumia. Hakuna mzazi wala jamii inayotamani kukuza mtu wa namna hii.

Mara nyingi ukorofi wa mtoto ni ujumbe. Ni muhimu uuelewe ujumbe huu kabla hujachukua hatua za kuushughulikia. Ukorofi ni lugha ya kusema ndani anajisikia utupu. Ni sawa na mtu aliyeshinda njaa siku kadhaa. Kwa vyovyote vile ni dhahiri atakosa utulivu. Mwili wake unahitaji chakula.

Mtoto mkorofi kimsingi anaamini watu wanaomzunguka hawajatambua nafasi yake ipasavyo. Kuna sauti inatoka ndani yake na anaisikia yeye tu inayomwaminisha kuwa hatambuliki. Imani hiyo potofu huchochea jitihada za kutafuta kutambulika kwa namna isiyofaa.

Ubishi na ukaidi anaoufanya mtoto wakati mwingine bila hata yeye kutambua ni namna ya kujirudishia mamlaka anayoamini hana. Anapobishana na mzazi, anapogombana na wenzake, kimsingi anajaribu kujirejeshea ushawishi ambao anaamini hana.

Mambo mengi yanaweza kuzaa ukorofi. Baadhi ya wanasaikolojia wanaamini mtu huzaliwa na ukorofi na haw ani wale wanaoamini pia katika urithi wa jenetiki. Inawezekana. Lakini kwa sehemu kubwa tafiti zinaonyesha kuwa ukorofi ni zao la malezi.

Kuna mambo kadhaa ya kuzingatia. Kwanza, inawezekana kwa sababu ya kutamani mtoto ‘anyooke’ umekuwa na unatumia sheria kali mno. Unaamini mtoto hawezi kufanya kitu bila kuamrishwa. Kwa sababu ya kuamini hivyo, umejikuta ukijenga mazingira ya mapambano yasiyo na sababu mtoto. Mtoto mkorofi ni ama anakuiga vile ulivyo au basi anapambana na wewe kwa kuwa wakati mwingi tunaamini tabia yam toto/mtu yaweza kuwa matokeo ya vile anavyoona anatendewa na uoande wa pili.Yaani tabia ya mtu wakati mwingine ni matokeo ya namna aanavyotendewa.

Lakini pili, inawezekana una ukali uliopitiliza. Huwezi kuongea bila kufoka na kupaza sauti. Huna sauti ya upole inayoleta taswira ya mtu mwelewa, anayejali, na mtulivu. Unaamini bila kelele hakuna nidhamu.

Pengine, inawezekana mtoto amekuwa akishuhudia vitendo vya ukorofi katika mazingira ya familia au kwa jirani zako. Kwa kawaida, watoto wananasa kwa haraka sana mambo yanayogusa hisia zao. Wanapoona mtu mzima anafanya jambo fulani na watu anaowaamini wanalichukulia kawaida, wanakuwa na uwezekano mkubwa wa kufanya kile kile wakati fulani.

Unawezaje kumrekebisha mtoto?

Jambo la kuzingatia ni kuwa ukali na mapambano yanakomaza ukorofi. Badilika na amua kuwekeza katika kujenga urafiki kabla hujatarajia kusikilizwa. Hapa sizungumzii urafiki wa siku mbili au tatu. Hapana. Ninamaanisha urafiki wa kudumu ambao mtoto hatakuwa na sababu ya kuwa na mashaka nao. Kama tulivyoona, mtoto mkorofi kimsingi anahitaji uhusiano wa karibu na wewe mzazi kuliko hata mtu mwingine yeyote yule.

Hata katikati ya urafiki huo, usishangae mwanzoni bado mtoto akaendelea kuwa mkaidi vile vile. Jambo la msingi hapa ni kutokata tamaa. Mpe nafasi ya kukuamini kwa kujenga urafiki imara. Sambamba na urafiki, punguza amri na kelele zisizo za lazima. Kumbuka kuwa amri bila urafiki huchochea uasi.

Jitahidi sana kujenga tabia ya mazungumzo ya utulivu unaposhughulika naye. Badala ya kuagiza, jaribu kushirikiana naye. Mwonyeshe kuwa unajali na kuthamini kile anachokipenda. Huna sababu ya kushindana naye. Katika mazungumzo, mpe nafasi ya kusema. Mwache aongee yaliyoujaza moyo wake na usiwe mwepesi kukosoa hisia zake wala kujitetea. Kumbuka kuwa ukorofi wake unatokana na kujisikia kutokueleweka kama nilivyoeleza hapo awali.

Mpe uzingativu kwa kuacha shughuli unazofanya kwa ajili yake. Ushirikiano wa kiwango hiki utamchangamsha. Ukiweza kufanya hivi bila mara kwa mara mtoto ataanza kukuamini na kidogo kidogo atabadilika.

Kadhalika, mheshimu kama mtu mwingine yeyote unayemheshimu. Heshima ina mambo mengi. Usimdhalilishe mbele ya wenzake kwa maneno au vitendo. Kama kuna sababu ya kumwadhibu, fanya hivyo kwa staha. Kumheshimu mtoto hakukuondolei mamlaka yako kama mzazi.

Jitahidi sana kutengenza mazingira ya kufanya maamuzi shirikishi yanayoheshimu matakwa yake. Kwa sababu tayari ana ukorofi, mweke karibu unapotaka atekeleze jambo. Badala ya kumwambia ‘kafanye,’ badili lugha iwe, ‘tufanye’ hata kama hulazimiki kufanya. Inapobidi, hasa kwenye hatua za mwanzo, shirikiana nae kufanya hicho unachotaka akifanye.

Vile vile, tambua kizuri kipya anachojifunza. Kama, kwa mfano, ameweza kuacha kubishana unapomwagiza kufanya kitu, usikae kimya. Tambua mabadiliko hayo hata kama ni madogo. Fahari ya mtoto ni kuona jitihada zake zinatambuliwa. Kadri unavyomfanya ajisikie kutambuliwa, ataendelea kufanya bidii ya kukupendeza na hatimaye ukorofi aliokuwa nao utapungua.

Jerome Mmassy

Mmassyfm@hotmail.com
Nilivyomwelewa mleta mada Ni kwamba, usiwe mzazi mkorofi.
Mzazi mkorofi always hutengeneza mtoto mkorofi.
Tuongee ukweli, Ni mzazi yupi mkorofi anaeweza kuzingatia kanuni za mleta mada!
 
Back
Top Bottom