Matumizi na Faida za Asali katika afya ya binadamu

Naipenda asali na nimekuwa mtumiaji wa muda mrefu na kwa kiwango kikubwa mpaka nakuwa na wasiwasi wa kudhurika. Niliitumia kama kitu nipendacho sikujua kama ni tiba. X-PASTER & MziziMkavu

1: Asali ikikaa muda mrefu huganda kama sukari, je isipofyonzwa mwilini haiwezi kuganda na kuwa jiwe tumboni?
2: Nasikia ukiichanganya na chai au maji ya moto sana vile vitu muhimu hufa na kubaki makapi, je ni kweli?
 
Last edited by a moderator:

Asali haiwezi kuganda hata siku moja Asali hata ukiitia kwenye Jokofu (Friji) haiwezi kuganda Ukiona Asali umeitia kwenye Friji na imeganda hiyo itakuwa ni Asali Feki iliyochanganywa na sukari na zipo Asali Feki nyingi mjini kuwa muangalifu sana Mkuu TaiJike
 
Last edited by a moderator:
Hapa ndo kwenye tiba lakini wengi wetu huwa wana dharau matokeo yake wanabaki kuhangaika.
 
Asali haiwezi kuganda hata siku moja Asali hata ukiitia kwenye Jokofu (Friji) haiwezi kuganda Ukiona Asali umeitia kwenye Friji na imeganda hiyo itakuwa ni Asali Feki iliyochanganywa na sukari na zipo Asali Feki nyingi mjini kuwa muangalifu sana Mkuu TaiJike

Mie ninayo na huwa nanunua kwenye chanzo ambacho ninakiamini yaani nilivyosoma hapa mwili umesisimka maana asali mie nayotumia yaani ni nzito alafu si nyekundu kama niliyozoea those days hasa kwa wale wenyeji wa Mwanza na Tabora wataelewa asali nayoizungumzia, hii asali inaganda na ni nzito alafu inakuwa inaweupe flani hivi yaani ukitaka kumimina inachukua muda mrefu mpaka uiweke kwenye jua, au kuganda huko ni kwa namna gani
 
Hio ni asali mbichi. Inakuwa namna hio. Ni nzuri tu wala haina shaka yoyote nakuhakikishia hilo.
 
Wapendwa salam,

Naomba anayefahamu matumizi ya asali na mdalasini katika kupunguza uzito.

Inatumikaje na muda gani?

Ahsanteni.
 
Changanya katika ratio ambayo itakuwezesha kulamba kwa kijiko...lamba kila siku asubuhi kabla hujapata kifungua kinywa.,asali iwe ya nyuki wadogo....Angalisho ni kwamba sio kila mwenye kitambi kitaisha, mazoezi, tabia ya mlaji na factors nyingine zinahusika..,
 
Habari hiyo imeandikwa kwenye gazeti la Nipashe, Jumamosi Oktoba15, 2016.

Kwa kuwa mimi ni mpenzi na mwumini mwaminifu wa vyakula asilia na matunda, nimeona ni vyema niwashirikishe kujua ubora wa hivi vyakula na matunda kwa afya zetu, vijana na wazee. Hasa vijana acheni kula "junk food" hasa vilivyokaangizwa km chips mayai.

Makala ya NIPASHE kwa ufupi inanukuu ushuhuda wa madaktari kadhaa, kwamba:
1) Maziwa husaidia katika kuimarisha afya ya wanandoa, kwa sababu ya wingi wake wa protini.
2) Asali husaidia kuupa mwili nguvu ambayo ni muhimu kwa tendo la ndoa.

Ili kupata faida ya vyakula hivyo na nitakavyovitaja, ni sharti uwe mlo endelevu. Mtu yabidi ujenge tabia wa kutumia angalau kijiko kimoja cha asali kila asubuhi na jioni na/au glasi moja ya maziwa kila siku.

Kwa asali ni budi iwe ya asili, kwa kuwa ina madini ya chuma ambayo husaidia kutengeneza damu ndani ya mwili. Na kazi ya damu ni kusafirisha hewa ya oxygen kwenye viungo vya mwili (km uume) kwa uhai wake, kufanya kazi vizuri.

Orodha nyingine ya vyakula na matunda, kwa ajili ya kuimarisha uwezo wa tendo la ndoa, ni kama ifuatayo:
1) Mboga za majani: zina vitamini nyingi zinaongeza hisia za kujamiiana
2) Ini: lina wingi wa madini ya zinc ambayo ni muhimu kwa uzalishaji wa homone za kiume (testosterone).
3) Mvinyo mwekundu: husaidia kupunguza uume kukosa nguvu hivyo ni kama kichocheo cha kutahitaji tendo la ndoa.
4) Mayai: yana kiasi kikubwa cha vitamini B5 na B6, ambazo ni muhimu kudhibiti msongo wa mawazo.
5) Ndizi mbivu: japo ina mwonekano wa uume, imesheheni madini ya potassium, magbesium, Vitamini B ambavyo huongeza nguvu za kiume/ tendo la ndoa.
6) Mbegu za matunda kama vile tikiti maji, ubuyu, maboga, alizeti, nk pia karanga. Hizi pia huongeza nguvu za kiume. Na kwa huwa na madini ya zinc, mwili huzalisha mbegu za kiume nyingi.
7) Viazi vitamu: vina vitamini A ambayo husaidia mwanake kulinda umbile la k... na mfuko wa kizazi, na huzalisha homone za kike.
8) Samaki: mafuta yaliyomo kwenye samaki (omega -3) ni muhimu sana kwa nguvu za kiume/ tendo la ndoa.
9) Parachichi: lina umbo la mwili wa kike na lina vitamini B6 na madini ya potassium, muhimu kwa kuongeza nguvu za kiume/ tendo la ndoa.
10) Tikitimaji: pamoja kutumika mbadala wa maji, husaidia kulegeza mishipa ya damu hivyo kurahisisha mzunguko wa damu mwilini na hatimaye nguvu za kiume/tendo la ndoa.
 
Nime-Like hii post, lakini hapo kwenye mvinyo mwekundu mimi sikubaliani napo.
 
Mvinyo mwekundu ni kichocheo cha kupenda tendo la ndoa, na kama mwanaume ana tatizo la urijali unasaidia
 
Mimi nimevitumia hivyo vitu sasa nimegeuka kero kwa wangu darling maanake ni mwendo wa kutaka na kutaka tena,yaani ni kumpa kumpa tena,mpaka nimeamua kupunguza kula maini na mayai lakini wapi!!!
 
Nimeipenda hii kitu nilikua nishaacha pombe ila huo mvinyo haina bahati Dompo kwenda mbele
 
Back
Top Bottom