Fahamu matumizi na faida za asali katika afya ya binadamu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fahamu matumizi na faida za asali katika afya ya binadamu

Discussion in 'JF Doctor' started by X-PASTER, Nov 16, 2008.

 1. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #1
  Nov 16, 2008
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Habari za muda huu wana-JF!

  ASALI inafahamika kwa muda mrefu kama chakula muhimu ambacho pia kinasaidia sana katika kupambana na magonjwa mbalimbali na matatizo yatokanayo na uzee. Kwa mujibu wa tafiti mpya za wataalamu wa madawa lishe na vifaa tiba, imedhihirika kwamba, uwezo wa asali kutibu unaweza kuongezeka
  maradufu kama itachanganywa na mdalasini.

  Aidha, uchunguzi wa kila wiki unaofanywa na jarida la World News kuhusu tiba unasema, wataalamu wa madawa yatokanayo na mimea,imeonekana kwamba kuna dazani nyingi za umuhimu wa asali na
  mdalasini katika kujenga afya bora.

  Asali ikishachanganywa na mdalasini pamoja na mafuta ya vuguvugu ya mzaituni, hutoa kichocheo maridhawa cha kuotesha nywele kinachotumika katika dawa ya Dork.

  Mchanganyiko huo vuguvugu unapakwa kwa kusugua kichwani na kuachwa kwa dakika 15. Kwa mujibu wa watafiti wa madawa tiba, Dk Alexander Andreyed na Eric Vogelmann, madhara yaletwayo na vyakula vyenye mafuta mwilini yanaweza kudhibitiwa kwa kiasi kikubwa kwa matumizi ya mara kwa mara ya chai iliyoungwa kwa kutumia mchanganyiko wa asali na mdalasini.

  Ugunduzi wao huo, uliyakinishwa vema kwenye jarida mashuhuri linalozungumzia masuala ya tiba la nchini Denmark la Julai 1994. Uchunguzi mwingine pia umeonesha kwamba matumizi ya kila siku ya asali yanapunguza viwango vya lehemu mwilini.

  Asali inatajwa pia kuwa dawa ya jino, inaponya pia ngozi iliyoharibika, ni dawa asilia ya shinikizo la juu la damu ni kiungo muhimu katika utengenezaji wa asilimia kubwa ya madawa mmimiko na asilimia kubwa ya vipodozi na mafuta ya kupaka.

  Ugonjwa wa mafua ambao huwakera na kuwanyima watu wengi raha imegundulika na wataalamu kwamba hupungua na kupotea kabisa ikiwa watatumia kijiko kimoja cha chai cha asali vuguvugu iliyochanganywa na robo kijiko cha chai cha mdalasini. Mtafiti mmoja wa Hispania imethibitisha kwamba, aina ya dawa moja asilia iliyofanikiwa kuharibu vimelea viletavyo mafua ilitengenezwa kwa kiwango kikubwa na asali.

  Mchanganyiko huo pia ni mahususi katika kusaidia kupunguza na kuondoa chafya na kuvimba kwa koo. Asali inaaminika pia huamsha hamu ya tendo la ndoa. Wale ambao mambo katika eneo hilo si mazuri wanashauriwa angalau kunywa vijiko viwili vya mezani kila siku kabla ya muda wa kulala usiku. Kuna wakati asali ilipigwa marufuku kwa makasisi katika baadhi ya dini za Mashariki mwa dunia ili isiwe sababu ya kuwaongezea mihemko.

  Asali inaaminika kuwa dawa ifaayo katika kuondoa mchafuko wa tumbo pamoja na kichefuchefu. Ukiwa katika kadhia hiyo, unashauriwa kuongeza kiasi kidogo cha mdalasini na asali kwenye chai ama maji, itapunguza hali hiyo na maumivu yaletwayo na vidonda vya tumbo.

  Utamaduni wa kula asali pamoja na mdalasini, huweza kuondoa mchafuko wa tumbo na utumbo uletwao na gesi kwa mujibu wa uchunguzi mahsusi uliofanywa huko India na Japani kwa miaka mingi. Unaweza kukinga kupata ugonjwa wa moyo na kuzuia, mkusanyiko wa mtandao wa mafuta kwenye mishipa ya damu kwa kula asali na mdalasini mara kwa mara wakati wa kifungua kinywa.

  Kula mkate uliopakwa asali kijiko kimoja cha mezani kila siku nyuzi nyuzi zake ni muhimu pia kiafya. Tiba hii, iliweza kupunguza kuganda kwa mishipa ya damu kwa asilimia 74 ya wagonjwa waliofanyiwa utafiti. Shinikizo la damu, pamoja na matatizo yaambatanayo na maumivu ya kifua na kizunguzungu yalitoweka kutoka kwa wagonjwa wengi wiki chache tu baada ya watafiti wa Kiitaliano kuwapa dozi za mara kwa mara za asali iliyochanganywa na mdalasini.

  Kinga ya mwili, itaongezeka mara tatu zaidi ikiwa utatumia mara kwa mara asali na mdalasini kwa pamoja, wataalamu wanasema. Utafiti wa kitiba unaonesha kwamba, asali ina hazina kubwa ya virutubisho na madini pamoja na michanganyiko mingine iondoayo magonjwa pamoja na kinga, itolewayo na chembechembe nyeupe za damu, husaidia kuzuia magonjwa pamoja na kuharibu vimelea virusi na bakteria. Vijiko viwili vya asali iliyonyunyiziwa mdalasini kabla ya mlo, huondoa kiungulia pia. Inasemekana kuwa, unaweza kuishi hadi miaka 100 ukifurahia maisha ya afya bora na madhubuti kwa kunywa kila siku kikombe baridi cha chai iliyowekwa mdalasini na asali.

  Kutengeneza kinywaji hiki kitamu, weka vijiko vinne vikubwa vya mdalasini katika vikombe vitatu vya maji na koroga kwa dakika 10, kunywa robo kikombe kutwa mara tatu au nne, watafiti wanasema.

  Asali ni tiba rafiki na asilia kwa watu wenye shida ya chunusi. Ili kutibu tatizo hilo watafiti wanasema changanya vijiko vitatu vya asali pamoja na kijiko kimoja mdalasini na pakaa kwenye chunusi.

  Uwezo wa asali wa kuua bakteria utaufanya uso wako kuwa kawaida katika muda wa wiki mbili pekee. Asali, wanasema inairudisha ngozi iliyoharibiwa na wadudu waharibifu kama dondola, washawasha na hata ngozi iliyopata madhara kutokana na kuungua moto. Pakaa asali na mdalasini moja kwa moja kwenye sehemu zilizoathirika na rudia wakati mwasho unapokuathiri. Rudia tena hadi uvimbe unapotoweka.

  Utafiti uliofanywa karibuni nchini Australia na Japan, umeonesha kuwa, asali ina uwezo mkubwa katika tiba ya mgonjwa kwa mtu anayetumia madawa ya kutibu saratani. Katika utafiti uliofanywa kwa wagonjwa waliokuwa wanaugua kwa kiwango kikubwa saratani ya mifupa na tumbo, wale waliokuwa wakitumia kila siku dozi za asali na mdalasini, walionesha kupata nafuu maradufu kuliko wale waliokuwa wakitumia madawa ya saratani pekee. "Tuliwapa kijiko cha mdalasini na asali kutwa mara tatu kwa mwezi," anasema Dk Hiroki Owatta. Upo ushahidi mpya kwamba, sukari asilia zilizopo kwenye asali, zina uwezo wa kuongeza nishati mwilini. Zikitumika ipasavyo, sukari hizi zinaweza kuwasaidia wazee na wengine wanaosumbuliwa na uchovu.

  Wataalamu wanapendekeza kuchanganya nusu kijiko cha asali katika nusu bilauri ya maji kisha nyunyizia mdalasini na kunywa masaa mawili baada ya kuamka asubuhi. "Kunywa tena saa 9:00 alasiri wakati nishati (nguvu) inapoanza kushuka," anashauri Dk Milton Abbozza ambaye kazi zake kuhusu asali na mdalasini kama kichocheo cha nishati mwilini zinatambulika kimataifa.

  Asali inao uwezo mkubwa wa kupunguza na kuponya miguu iliyopasuka kwenye kisigino. Chua asali na mdalasini vuguvugu katika miguu au nyayo zilizoathirika baada ya siku ndefu na kazi au baada ya mazoezi marefu. Rudia kila siku asubuhi halafu, osha nyayo zako kwenye maji baridi na vaa viatu.

  Baadhi ya watu Marekani ya Kusini, wanasukutua maji ya vuguvugu yaliyowekwa asali na mdalasini kila asubuhi ili kufanya harufu mdomoni kuwa nzuri na safi kiasilia. Katika Asia ya Kusini Mashariki, watu hutumia kijiko cha mdalasini na asali ili kuondoa harufu mbaya mdomoni (halitosis).

  Wataalamu wanaamini kwamba, uwezo wa kuua bakteria uliopo kwenye asali ndiyo unaopigana na harufu mbaya itokayo mdomoni. Dozi za kila siku za asali na mdalasini, hufanya hali ya usikivu murua kwa wanafunzi wawapo darasani au viongozi mkutanoni kama ilivyogunduliwa na Wagiriki wa zamani. Hiyo ndiyo asali. Ni chakula na dawa. Lakini inayozungumzwa hapa ni asali mbichi ambayo inapatikana kwa wingi Tanzania, lakini tatizo kubwa ipo pia feki inayouzwa kama mbichi!

  Kwa hisani ya AFYA.KWANZA

  =============

  Toafauti ya asali ya nyuki wadogo na nyuki wakubwa

  Asali za NYUKI WAKUBWA na WADOGO zina tofautiana katika mambo kadhaa na hvyo ni muhimu kujua tofauti hizo kabla hujanunua ili kua na uhakika.


  NYUKI WADOGO
  1. Ni nyepesi zaidi kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 24​

  2. Ina ladha ya UCHACHU ingawa ni tamu sana.
  3. Mara nyingi ina rangi ya KAHAWIA ILIYOKOLEA inayoenda kwenye WEUSI


  NYUKI WAKUBWA
  1. Ni nzito kuliko ya nyuki wadogo kwani ina kiwango cha maji kuanzia asilimia 17 hadi 20.
  2. Ni tamu moja kwa moja bila kua na ladha ya uchachu kama nyuki wadogo
  3. Ina rangi nyingi kuanzia NYEUPE, NYANO, KAHAWIA ILIYOPOA, KAHAWIA ILIYOKOZA n.k

  Hizo ni tofauti za muhimu kuzijua kwani zitakuwezesha kupata asali unayoitaka na kuepuka usumbufu.
   
 2. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #2
  Nov 16, 2008
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,893
  Likes Received: 66
  Trophy Points: 145
  I am strating to realise that everything GOD gave us is pertinent and for very good reason.

  ======================

  =======================
  Asali na mdalasini
  =======================
  ================
  Asali na Karanga
  ================

  [​IMG]

  Karanga ni mojawapo ya nafaka muhimu kwa afya ya binadamu. Huweza kutumika kama chakula, mafuta, kiungo na hata kwa ajili ya urembo.

  Zao hilo huweza vile vile kufanya maajabu katika ngozi.Bila kubagua jinsia, matumizi ya karanga husaidia katika kuondoa makunyanzi na kulainisha ngozi.

  Kwa kazi hii ya ngozi, karanga zinazohitajika ni zile mbichi. Kitu kinachohitajika ni kuchukua karanga mbichi ambazo hazijakaangwa kiasi kidogo kama kikombe kidogo cha chai.

  Zianike karanga juani kwa muda ili ziweze kumenyeka kwa urahisi bila kukaanga. Saga karanga zako kwa kutumia blenda au kitu chochote kitakachoweza kuzilainisha na kuwa unga laini.

  Chukua unga wako wa karanga na uuchanganye na asali mbichi kiasi kidogo, kisha acha kwa muda wa dakika 10 ili vichanganyike. Chukua mchanganyiko wako, kisha paka usoni hasa zile sehemu unazoziona kuwa na mikunjo zaidi.

  Subiri kwa dakika kama 10, kisha osha uso wako na sabuni isiyo na kemikali baadaya hapo futa uso wako na kitambaa kisafi na kikavu. Subiri tena kwa dakika 5 halafu paka mafuta au losheni.Unashauriwa kufanya hivi mara moja kwa wiki.

  Kiasili njia hii imekuwa ikitumiwa na Wanyamwezi wa Tabora kama kipodozi kwa ajili ya mabinti wadogo pindi wanapokaribia kufanyiwa sherehe maalum.
  Unaweza pia kusugua taratibuuso kwa kutumia mchanganyiko wako ili kuondoa takataka katika mwiliwako ambapo baada ya kumaliza zoezi hilo unaweza kujipodoa kwa kupaka aina nyingine za vipodozi.

  Kwa kuwa hazina madhara, unaweza kufanya hivi kila siku na utafurahia matokeo yake.


  Source: Mwananchi.

  Mpendao ngozi zenu kazi kwenu mshindwe wenyewe tu!
   
 3. s

  sinani Member

  #3
  Feb 15, 2010
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Asante sana maalim.
  Hiii ni dahwa haswa...
  Tuko pamoja.


  ==================
  Asali na Tangawizi
  ==================


  ====================

  Dawa ya kikohozi kwa kuchanganya Asali na yai la Kienyeji

  Asali weka kijiko 1 na changanya na yai la kuku wa kienyeji moja kunywa asubuhi kabla ya kula kitu fanya hivyo kwa muda wa siku 3 kila siku asubuhi na mchana na usiku utapona inshallah.
   
 4. Kimbweka

  Kimbweka JF-Expert Member

  #4
  Feb 15, 2010
  Joined: Jul 16, 2009
  Messages: 8,608
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  Kula 5 mkuu hii safi sana!
   
 5. A

  AHAKU Member

  #5
  Feb 15, 2010
  Joined: Jan 28, 2010
  Messages: 26
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  asante sana ndugu X Pastor ila naomba unisaidie kiswahili cha Cinnamon powder
   
 6. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #6
  Feb 15, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Mdalasini ya unga.
   
 7. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #7
  Feb 16, 2010
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  naongeza 5 zangu ziwe 10 kabisa
   
 8. Kunta Kinte

  Kunta Kinte JF-Expert Member

  #8
  Feb 16, 2010
  Joined: May 18, 2009
  Messages: 3,660
  Likes Received: 215
  Trophy Points: 160
  It is good brother, thanks a lot!
   
 9. kikahe

  kikahe JF-Expert Member

  #9
  Feb 16, 2010
  Joined: May 23, 2009
  Messages: 1,273
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hii imekaa vizuri!!!
   
 10. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #10
  Feb 16, 2010
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Asali inafaa sana kwenye shughuli nzima ya kufanya mapenzi! Its a good lubricant na inaongeza mnato! For smooth sex man can apply honey on his part before penetration especially if the partner has a dry va....kama foreplay cant help go for honey
   
 11. D

  Donrich Senior Member

  #11
  Feb 16, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 106
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Asali kweli kiboko!
   
 12. Mshirazi

  Mshirazi JF-Expert Member

  #12
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 8, 2009
  Messages: 444
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Tunashkuru sana mkuu

  Na jee vipi kuhusu hii habari ya asali ya NYUKI WADOGO na asali ya NYUKI WAKUBWA,,, Jee! kitaalamu inaleta mantiki yoyote? Ni kweli kwamba ile ya nyuki WADOGO ni nzuri zaidi? au ndio usanii wa kupandisha BEI tu?
   
 13. elimumali

  elimumali Senior Member

  #13
  Feb 17, 2010
  Joined: Jan 13, 2010
  Messages: 149
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Asante sana X-Paster. Wana Jamii mi ombi langu ni moja. Anayejua pale inapopatikana asali (ORIGINAL) atuelekeze hapa, maana asali hapa mjini zimejaa fake, zilizopikwa na kuchujuka hata hiyo faida zote hizi zinazoelezwa hapo zinakuwa hazipo tena.
   
 14. L

  Lusyonja Member

  #14
  Feb 17, 2010
  Joined: Jul 21, 2008
  Messages: 15
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Thanx for information on health benefits of HONEY.

  A nutural Honey can be purchased at Ministry of natural resources, department of honey and bee.

  But we are looking availability of PROPOLIS in local market esp.in DAR
  Due to acidity(low PH) of propolis and Honey it is vey good to improve immune system thus can be used for cancer and HIV patients.

  Where some one can purchase propolis in dar es salaam so that we can advice wananchi to go for it?
   
 15. Sinkala

  Sinkala JF-Expert Member

  #15
  Feb 17, 2010
  Joined: Dec 22, 2008
  Messages: 1,505
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Thanks X-P
   
 16. X-PASTER

  X-PASTER Moderator

  #16
  Feb 17, 2010
  Joined: Feb 12, 2007
  Messages: 11,651
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  Aina za nyuki zipo nyingi, habari za nyuki wakubwa na wadogo ni katika biashara tu. Kwani ubora wa asali ni kutokana na maua waliyoyapitia hao nyuki.

  NB:
  Nyuki wakubwa si wenye kuuma kama wale nyuki wadogo, hawa nyuki wadogo ni hatari sana wakikuuma maana wanaweza kusababisha hata kifo, ukilinganisha na nyuki wakubwa ambao inasemekana si wenye kuuma.
   
 17. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #17
  Aug 12, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,616
  Trophy Points: 280
  NAMNA YA KUTUMIA TANGAWIZI KWA TIBA
  Kutibu kutokusagika kwa chakula tumboni, Gesi tumboni, Msokoto wa tumbo (bila kuharisha), Kutapika, Mshtuko/Mkazo wa ghafula (wa msuli),Maumivu ya tumbo na Kibofu cha mkojo ikiambatana na Homa, Mafua, Kukohoa na Pumu.

  TUMIA JAM YA TANGAWIZI.
  JINSI YA KUTENGENEZA JAM YA TANGAWIZI.
  Kamua TANGAWIZI mbichi kisha changanya maji yake (Juice) na Sukari. Chemsha mpaka mchanganyiko huo uwe mzito. Ongeza Zafarani iliyosagwa,Iliki iliyosagwa, Kungumanga zilizosagwa na karafuu iliosagwa. Iweke dawa hii vizuri na tumia inapo hitajika.

  KWA KUVIMBIWA NA KUTAKA HAMU YA KULA.
  Changanya Juice ya TANGAWIZI, Juice ya Limau na Chumvi Mawe kwa vipimo vilivyo sawa. Hakikisha umechanganya vizuri. Kunywa dawa hii kabla ya Chakula.
  Vingineyo changanya vipimo vilivyo sawa sawa vya Juice ya TANGAWIZI na Sukari Mawe. Koroga vizuri, kunywa kabla ya kula chakula. Dawa hii husafisha Ulimi na Koo na hukuongeza hamu ya kula na kukufanya mchangamfu.


  MAUMIVU YA KOO NA KUKAUKA SAUTI
  Tafuna vipande vidogo vya Tangawizi.

  KWA KUHARISHA
  Chua sehemu zinazozunguka kitovu kwa Juice ya Tangawizi.

  KWA KISUKARI
  Kunywa Juice ya Tangawizi iliyochanganywa na Sukari mawe.

  KIUNGULIA, KUKOSA HAMU YA KULA NA BAWASIRI
  Tumia Samasarkara Churna.

  KICHEFUCHEFU NA KUTAPIKA
  Kunywa mchanganyiko wa Juice ya Tangawizi na Juice ya Kitunguu.

  MAUMIVU YA KICHWA CHA WASIWASI
  Changanya Juice ya Tangawizi na Maziwa, kisha kausha. Nusa unga huo kama Tumbaku.

  MAUMIVU MAKALI YA TUMBO
  Changanya kijiko kimoja cha au viwili vya Tangawizi iliyosagwa na kijiko kimoja au viwili vya mafuta ya Kastoroli. Kunywa kijiko kimoja mara mbili kwa siku.

  BARIDI YABISI SUGU
  Changanya kijiko kimoja cha Tangawizi ya unga na vijiko 24 vya maji kunywa mchanganyiko huu ukiwa vuguvugu. Ulale na ujifunike mpaka utoe jasho.

  KUUMWA JINO NA MAUMIVU YA KICHWA
  Chukua Tangawizi ya Unga koroga na maji kidogo iwe nzito kama tope. Jipake na uchue kwenye paji lako la uso kabla ya kulala. Kwa Jino jipake na uchuwe kwenye Shavu.
   
 18. L

  Lady JF-Expert Member

  #18
  Aug 12, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Thanks Mzizi Mkavu!
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  Aug 19, 2010
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Dawa Tosha,sasa mbona hatufugi nyuki kwa wingi,maybe ktk kilimo kwanza wataalam watuhamasishe tulime na kufuga nyuki
   
 20. Gamaha

  Gamaha JF-Expert Member

  #20
  Aug 19, 2010
  Joined: Jul 17, 2008
  Messages: 2,695
  Likes Received: 753
  Trophy Points: 280
  ha ha Rev kumbee! Thanks
   
Loading...