Fahamu Matatizo kwa mjamzito kukosa choo

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
KUKOSA CHOO WAKATI WA UJAUZITO.

Kukosa choo ni moja ya matatizo ambayo yamekuwa yakiwasumbua wajawazito wengi hususani katika miezi ya awali ya ujauzito na miezi ya mwisho ya ujauzito ,kukosa choo huleta wasiwasi kwasababu hali iyo siyo ya kawaida kwa mtu ambaye anakula na kunywa Kila siku ,pia kutokujua athari za kiafya ambazo zaweza jitokeza siku za mbele kutokana na tatizo hilo.

Kwa wajawazito kukosa choo ni hali ya kawaida Sana ambayo huchangiwa na uwepo wa mimba,katika kipindi hiki Kuna mabadiliko mengi ambayo hutokea sehemu mbalimbali za mwili,mabadiliko hayo ndiyo huleta vitu ambavyo havijazoeleka katika miili yetu.

Je nini husababisha mjamzito kukosa choo?

Kuna Mambo mbalimbali ambayo hutajwa kusababisha mjamzito kukosa choo,Mambo hayo ni:

.Mabadiliko ya homoni hususani progesterone,kichocheo hiki huzalishwa kwa wingi wakati wa ujauzito kwa kazi mbalimbali katika mwili wa Mama,licha ya kichocheo Cha progesterone kufanya kazi hizo kwa upande mwingine kichocheo hiki hulegeza misuli ya tumbo la chakula hivyo kusababisha mabaki ya chakula kukaa kwa muda mrefu tumboni bila ya kutolewa nje Kama taka,kadiri mabaki hayo yanavyo zidi kubaki tumboni maji yaliyokuwa katika mabaki hayo huendelea kufyonzwa na utumbo hivyo kusababisha kukosa choo kwa muda pia kupata choo kigumu.

.Kuongezeka kwa ukubwa wa tumbo la uzazi,hii hutokea zaidi katika miezi ya mwisho ya ujauzito,ukubwa wa tumbo la uzazi kutokana na kuongezeka kwa ukubwa wa mtoto tumboni husababisha mkandamizo mkubwa kwenye tumbo la chakula,hivyo kupunguza kasi ya usafirishwaji wa mabaki ya chakula nje ya tumbo,hivyo kusababisha mwili kufyonza maji katika mabaki hayo na kuleta choo kigumu.

.Utumiaji wa vidonge vya kuongeza madini ya chuma mwilini,licha ya dawa hizi kuongeza madini ya chuma mwilini ambayo ni muhimu kwa ukuwaji wa mtoto, dawa hizi huelezwa kuchangia kwa kiwango kikubwa mjamzito kukosa choo, pia choo kuwa nyeusi zaidi.

.Kutokufanya mazoezi,ufanyaji wa mazoezi huchochea misuli ya tumbo kufanya kazi yake ya kutoa taka nje ya mwili,kwaiyo mjamzito anavyo kuwa hafanyi mazoezi misuli yatumbo nayo hushindwa fanya kazi yake vizuri.

.Pia kutokula matunda nako hutajwa kuwa ni miongoni mwasababu ambazo huchangia kukosekana kwa choo wakati wa ujauzito.

.Kutokunywa maji pia huchangia kwa kiwango katika ukosekanaji wa choo.


Ushauri
Ili kuondokana na tatizo la kukosa choo wakati wa mimba fanya yafuatayo.

- Hakikisha unakunywa maji mengi kwa wingi Kila siku ili kulainisha choo.

- Pia hakikisha usibane haja kwa muda mrefu kwani kwa kufanya ivyo una sababisha choo kiwe kigumu.

- Hakikisha unafanya mazoezi mepesi Mara kwa Mara ili kuchochea ufanyaji kazi wa misuli tumboni mfano kutembelea.

- Inaelezwa pia Ulaji wa matunda huchangia kupata choo kwa kiwango kikubwa mfano maembe,mapapai n.k.

.Punguza Matumizi ya dawa za kuongeza madini ya chuma Kama unatatizo badala yake tumia vyakula ambavyo vina madini ya chuma mfano matunda na mboga mboga.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom