Fahamu masuala mbalimbali kuhusu ugonjwa wa Homa ya ini (Hepatitis B)

Bilionea kid

JF-Expert Member
Oct 19, 2018
581
516
HOMA YA INI (HEPATITIS B)
Kwa tafiti chache zilizofanyika mpaka sasa imegundulika kuwa kati ya watu 117 ni mtu 1 tu anakuwa ameathirika na virusi vya UKIMWI/VVU lakini ni watu 22 wanakuwa wameathirika na HOMA YA INI sawa na asilimia 18.8% lakini pia vifo vinavyosababishwa na homa ya ini kwa report ya dunia mpaka sasa ni mil 1.35 kwa mwaka.

Maambukizi ya HOMA YA INI yameongezeka kutoka milion 1.1 mpaka milion 1.7 kwa mwaka tofauti kabisa na maambukizi ya VVU/ UKIMWI ambayo ni mil 1.3 kwa mwaka hivyo hapa tunaona ni jinsi gani ugonjwa huu unazidi kusambaa kwa kasi zaidi.

Report ya wizara ya afya nchini iliyosomwa na waziri wa afya. July mwaka 2017 kuhusiana na homa ya ini inaonyesha kuwa katika watanzia 100 ni watanzia 8 hupata maambukizi sugu ya ugonjwa huu (chronic hepatitis). Hivyo basi kati ya watanzia million 55 ni watanzania mil 4.2 wanapatwa na ugonjwa sugu wa homa ya ini

Ndugu zangu ugonjwa wa homa ya ini ni ugonjwa hatari saana si tu kwamba unasababisha vifo taratibu au kimya kimya lakini ugonjwa huu unapoupata haujuchukui muda mrefu mpaka kufikia kifo lakini pia njia za ugonjwa huu kusambaa ni rahisi mno ukilinganisha na magonjwa mengine kama virusi vya UKIMWI

Sambamba na hilo kirusi wa homa ya ini ni kirusi ambae ni hatari zaidi kwani anasifa ya pekee ambayo anauwezo wa kukaa nje ya damu kwa muda wa siku zisizo pungua 7 na kusababisha maambukizi ya ugonjwa kwa mtu mwingine hii ina maana kwamba *iwapo ulitumia taulo la mtu aliyeathirika na virusi hivi ndani ya siku saba unakuwa katika mazingira rahisi zaidi ya kuambukizwa* hii ni tofauti kabisa na virusi vya VVU/UKIMWI ambapo kirusi wa VVU/UKIMWI hana uwezo wa kukaa nje ya damu hata dakika 1.

HOMA YA INI
ni ugonjwa ambao mtu anaupata baada ya kuambukizwa na kirusi aina ya HBV au HCV ambavyo hushambulia INI na kusababisha *KANSA YA INI .* Kuna aina 5 ya homa ya ini ambayo ni homa ya ini A, B, C, D, na E. . Watu wengi saana hupata maambukizi ya homa ya ini B na watu wenye virusi vya UKIMWI huambukizwa kwa urahisi zaidi na homa ya ini C . Virusi hivi vinapoingia ndani ya mwili huchukua siku 45 mpaka siku 90 kukomaa . Na ndani ya siku 60 mtu anapopimwa homa ya ini tayari huwa inajionyesha kuwepo ndani ya mwili

Virusi hivi vinapozaliana kwa wingi ndani ya ini hubadilisha mfumo wa kawaida wa ufanyaji kazi wa ini na kupelekea mtu kupata KANSA YA INI. Ambayo hii sasa ndo husababisha kifo kwa watu wengi.

NJIA ZA MAAMBUKIZI
Homa ya ini huambukizwa kwa kugusana na Maji maji / vimiminika Vyovyote vile kutoka kwa mtu aliyeathirika na ugonjwa huu. Vimiminika hivi ni kama
1. Damu
2. Mate
3. Jasho
4. Kuchangia vitu vyenye ncha kali
6. Maji maji ya sehemu za siri
7 kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Watu waliokatika mazingira hatarishi zaidi ambayo ni rahisi zaidi kupata ugonjwa huu ni
1. Wauguzi wa AFYA
2. Watumiaji wa pombe kupita kiasi (ULEVI)
3.Matumizi mabaya ya Dawa ikiwemo DAWA ZA KULEVYA
4. Waathirika wa virusi ya UKIMWI/VVU. Na magojwa yapunguzayo kinga za mwili.
5. kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto

Tafiti zinaonesha kuwa watoto wanaozaliwa na homa ya ini wengi wao hukuwa nayo na kupelekea kufikia hatua za kuwa ugonjwa sugu ndani ya mwili wao na hatimaye kifo

DALILI ZA UGONJWA HUU
HOMA YA INI kwa watu wengi haionyeshi dalili za awali pale tu mtu anapoambukizwa ni watu wachache saana ambao huonyesha dalili za awali za ugonjwa huu ambazo ni Uchovu kila mara, homa wakati wa jioni , kutokwa jasho jingi wakati wa usiku

Ugonjwa huu mara nyingi na kwa watu wengi huonyesha dalili zake unapokuwa umefikia hatua za mwisho yaani unapoona dalili basi ujue KIFO KIPO KARIBU dalili hizo ni
1. Homa
2. Uchovu muda wote
3. Macho kuwa ya njano
4. Maumivi makali yafuatanayo na uvimbe sehemu ya juu kulia kwa tumbo
5. Kutapika damu
6. Ngozi kubadilika
7 kutokwa damu bila kujizuia unapoumia
8. Kutokwa na damu kwenye fizi
 
Jamani naombeni dawa ya homa ya ini....ndugu yngu kaenda kutoa damu kwa baba akakutwa positive
 
Nenda ukachukue ile ya mkuu wa wilaya mama ashumta mshana.

Jaribu huenda ikamsaidia
 
Wahi hospitali,

Ukiwahi huu ugonjwa unatibikaa, ila acha pombe, sigara na michepuko.

Niaminiii
 
Huyo mtu akipewa chanjo na ni tayari +ve anakufa hata siku 3 hazitafika
Atapewaje chanjo wakati amesha ambukizwa na huo ugonjwa wa homa ya ini? Anaye pewa chanjo mtu ambae haja ambukizwa .

Is hepatitis B curable?
There's no cure for hepatitis B, but there are several treatments that can help with managing symptoms and reducing the risk of long-term health problems, such as cirrhosis. ... If you're at risk of being exposed to the virus, your best bet is to get the hepatitis B vaccine if you haven't already
 
Kama ana kinga mwili imara tatizo linaweza kwisha lenyewe bila complications,aepuka factors/ matendo yanayochangia au kepelekea tatizo hilo na yale yanayoshusha kinga mwili.
 
Kama ana kinga mwili imara tatizo linaweza kwisha lenyewe bila complications,aepuka factors/ matendo yanayochangia au kepelekea tatizo hilo na yale yanayoshusha kinga mwili.
Ikiwa amesha ambukizwa na Virusi Vya Homa ya ini kinga za mwili tu peke yake haziwezi kupambana na hao virusi wahoma ya ini pasipo na kutumia dawa za kuweza kuwauwa hao Virus i wa Homa ya ini ka Hepatitis B Virus. Maradhi ya Homa ya ini ni mabya zaidi kuliko hata Ukimwi.
 
Back
Top Bottom