SoC01 Fahamu mambo yanayofanya Wajasiriamali/Wafanyabiashara wadogo wadogo washindwe kufikia malengo

Stories of Change - 2021 Competition

Nzige255

New Member
Sep 12, 2021
2
2
Karibuni tena wapendwa kujifunza tena kupitia JAMIIFORUMS. Na leo tutapata wakati mzuri wa kujifunza juu ya mambo ambayo baadhi ya wajasiriamali/wafanyabiashara wanayakosea na hivo kushindwa kufikia malengo yao.

Mjasiriamali ni nani?
Ni mtu yeyote yule anayujishughulisha na kazi mbalimbali kwa juhudi zake na kujiingizia kipato. Sasa kuna baadhi ya mambo ambayo baadhi ya wafanyabiashara au wajasiriamali wadogowadogo wanashindwa kuyatimiza iwe wao binafsi au kwa watu wao wanaowahudumia mambo hayo ni pamoja na;

1. LUGHA
Wajasiriamali wengi wanashindwa kufahamu lugha sahihi ambayo wataitumia kwa ajili ya kufanikisha shughuli zao. Na kwenye suala la lugha wajasiriamali wengi wanaokumbana na changamoto hii ya lugha hasa wale wanaojishughulisha na biashara.

Wateja wengi huwa na maudhi mengi na hivo kupelekea mfanyabiashara huyu ashindwe kutumia lugha nzuri nahivo kujikuta tayari ametumia lugha ambayo sio nzuri kwa wateja wake.hivo ukiwa kama mjasiriamali lazima ufahamu kua wateja siku zote wanahitaji lugha nzuri itakayowavutia na wanapenda kunyenyekewa pia.

2. UJUZI
Baadhi ya wajasiriamali wanaingia kufanya shughuli za ujasiriamali pasipo kua na ujuzi/ufahamu wa kitu ambacho wanaenda kukifanya. Ujuzi ni muhimu itakupelekea kujua changamoto ambazo unaweza ukaenda kukumbana nazo wakati wa kutekeleza shughuli hiyo na namna gani utatatua. Mfano wajasiriamali wanaojishughulisha na kilimo hawa wanatakiwa wawe na ujuzi kwenye suala hili kupitia maofisa wa kilimo (Agriculture extensions) waliopo kwenye maeneo hayo ili waweze kufanikisha mafanikio yao waliojiwekea.

3. UZEMBE/UPUUZAJI
Wengi wa wajasiriamali/wafanyabiashara wanakosea katika suala la ulindaji wa mipango waliojiwekea na kuendekeza uzembe pamoja na upuuzaji na hivo kupelekea kuanguka kwenye malengo yao hivo ukiwa kama mjasiriamali inatakiwa uhakikishe unaondoa uzembe wa namna yeyote ule ambao unaweza kukupelekea kuanguka kufikia malengo yako.

4. MUDA
Katika jambo lolote lile ili uweze kufikia malengo inakupasa uwe mlindaji na mtu unayeheshimu muda. Wajasiriamali/wafanyabiashara wengi wamekua wakisahau suala la muda na kujikuta wakianguka kwenye shughuli zao. Ulindaji wa muda ukiwa kama mjasiriamali ni muhimu sana kufikia malengo yako.

5. UVUMILIVU
shughuli nyingi za ujasiriamali zinahitaji muda kuweza kuleta matokeo chanya. Ambazo ukiwa kama mfanyabiashara/mjasiriamali unatakiwa kua mvumilivu kuweza kufikia mafanikio yako. Kuna muda biashara inaweza kukuingizia hasara na ukakata tamaa kabisa lakini jambo la muhimu unatakiwa uzidi kua mvumilivu ili uweze kutimiza ndoto ulizojiwekea.

6. MSIMAMO
Wengi wa wafanyabiashara na wajasiriamali wanashindwa kua na msimamo kwenye shughuli zao. Na kupelekea kuyumbishwa na maneno ya watu wengine na kujikuta wakiona kua chaguzi ya shughuli aliyoichagua sio sahihi. Ukiwa kama mjasiriamali unatakiwa uwe na msimamo kwenye lengo lako hata ikiwa kuna changamoto nyingi zinazokukabili.

Nashukuru kwa kutoa muda wako kujifunza kupitia andiko hili. Natumaini ukiwa kama mjasiriamali/mfanyabiashara umejifunza kitu. Mwisho wa andiko hili ndio mwanzo wa andiko jingine zuri uweze kujifunza nami.

Vote for me please.
 
Back
Top Bottom