Fahamu mambo mbalimbali kuhusu Kilimo cha Korosho

safiii saana umempa za uso, aina ya watu kama hao wapo wengi saana mtandaoni, wengine ndo haoo wanasema "ZIMEDODA" hahaa hajui watu wanapiga pesa tuu

Hao watoto wa manzese mkuu. Wanakaa darajani pale kushangaa magari huku wapo mitandao kuchat ela za bando wanapiga mizinga kwa ndg zao. Kwa kukosa kazi wanashinda umu kupotosha watu. Kama huyo mwingine akaja na picha ii tujue ni mkulima kumbe tapeli tu.

Aisee hatari sana. Afu MTU kama huyo anaweza sema tuma ela nikufanyie mchakato uku nawe ukaamini kweli ni mkulima
Wadau cha msingi mkisikia fursa sehemu kabla ya yote nenda mwenyewe eneo la tukio ukajionee afu ufanye maamuzi.

Kama zimedoda au zinalipa utajionea uko uko na maamuzi sahihi utayapata eneo la tukio.

Ova
 
Naskia kuna wengine wananunua kidogo kidogo wanakusanya hadi ziwe nyingi afu wanaziuza tena
Sasa hapa ndio sijaelewa

Unakusanya afu ukiuza tena utamuuzia nani? Kuna faida gn pale?!

Yeah wananunua kwa mkulima kwa bei ya chini mfano elf2 kwa kilo. fu anapeleka kuuza ghalani ambako kule utaratibu wa mauzo ni wa mkopo, maana mpaka mnada upigwe bei ifahamike ndo ela inatoka baada ya siku kadhaa.

Huu utaratibu wa kuuza ghalani kwa mkopo ndo unasababisha mkulima auze kwa mnunuzi mdogo kwa bei ya ulanguzi ili tu apate ela ya kujikimu. Maana akipeleka ghalani ela inachelewa Ghalani ela inatoka baada ya mnada kupigwa. Kwa hiyo mkuu ni fursa kwa watu kwenye ela zao.

Ukinunua elf2. Ukauza kwa 3940. Nafikiri hisabati ulisoma darasa la pili
Jibu ngapi hapo?

Mfanyabiashara hapo ndipo anapopunia pesa Maana akitoa makato kidogo ata 600 tu Bado inamlipa 3940-600=??
Kila mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yaken Ila ni biashara haramu mkuu. Serikali ikikufuma mnagawana umasikini,maana wanakataza ulanguzi huu.

Tehtehteh! Nadhani umeelewa mkuu
 
Yeah wananunua kwa mkulima kwa bei ya chini mfano elf2 kwa kilo. Afu anapeleka kuuza ghalani ambako kule utaratibu wa mauzo ni wa mkopo,maana mpaka mnada upigwe bei ifahamike ndo ela inatoka baada ya siku kadhaa.

Huu utaratibu wa kuuza ghalani kwa mkopo ndo unasababisha mkulima auze kwa mnunuzi mdogo kwa bei ya ulanguzi ili tu apate ela ya kujikimu maana akipeleka ghalani ela inachelewa ghalani ela inatoka baada ya mnada kupigwa. Kwa hiyo mkuu ni fursa kwa watu kwenye ela zao. Ukinunua elf2. Ukauza kwa 3940. Nafikiri hisabati ulisoma darasa la pili, Jibu ngapi hapo?

Mfanyabiashara hapo ndipo anapopunia pesa Maana akitoa makato kidogo ata 600 tu Bado inamlipa
3940-600=? Kila mbuzi anakula kulingana na urefu wa kamba yake Ila ni biashara haramu mkuu, serikali ikikufuma mnagawana umasikini, maana wanakataza ulanguzi huu.

Tehtehteh
Nadhani umeelewa mkuu
Nimeelewa na asante kwa ufafanuzi mkuu
 
Habari wana JF. Naomba mwenye uzoefu au utaalamu wa zao la korosho anisaidie kujua mahitaji ya kuanzisha kilimo hiki. Nataka nitafute shamba(virgin land) kwa kilimo hiki, napenda nijue maeneo ambayo zao hili hustawi sana, mbegu bora ya muda mfupi, gharama za kuhudumia hadi kuanza kuvuna ikiwa ni pamoja na madawa, mbolea kama itahitajika na masuala mengineyo.

HABARI,
"Mandison,
Gharama za kuanzisha kilimo cha koroso sio kubwa sana haizidi laki moja kwa heka,Korosho ni zao linalokubali katika mikoa mingi hapa tanzania ukiacha mikoa yenye umaarufu ,MTWARA,LINDI,PWANI,TANGA,iko mikoa mipya kamaTABORA,SINGIDA,DODOMA,SOGWE,RUKWA huko kote zao la korosho linastawi vizuri fanya mawasilianano na kituo cha utafiti wa kilimo cha naliendele.Watakupa maelekezo mengi sana nadhani maswali yako yote utapata majibu pale,
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI)


Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com

LUMUMBA
 
jogi BILA SHAKA KUDODA UNAMAANISHA UZALISHAJI. NI KWELI MWAKA HUU KOROSHO HAZIJAZAA SANA.

WAPO WANAOSEMA HALI YA HEWA HAIKUWA NZURI IKAPUKUTISHA NA KUKAUSHA MAUA

LAKINI WAPO WANAOSEMA CHANZO NI UPATIKANAJI WA DAWA ZENYE UBORA

TUNASUBIRI RIPOTI YA WATAALAMU WA KILIMO
 
jogi BILA SHAKA KUDODA UNAMAANISHA UZALISHAJI. NI KWELI MWAKA HUU KOROSHO HAZIJAZAA SANA.

WAPO WANAOSEMA HALI YA HEWA HAIKUWA NZURI IKAPUKUTISHA NA KUKAUSHA MAUA

LAKINI WAPO WANAOSEMA CHANZO NI UPATIKANAJI WA DAWA ZENYE UBORA

TUNASUBIRI RIPOTI YA WATAALAMU WA KILIMO
Sulphur ilisumbua sana, wakulima baadhi walitegemea wauze choroau mbaazi ndio wanunulie sulphur, mambo hayakuwa mazuri.
 
Mti mmoja wa korosho uliostawi vizuri unatoa kilo ngapi za korosho kwa msimu mmoja? Ekari moja ni miti mingapi?
 
Mti mmoja wa korosho uliostawi vizuri unatoa kilo ngapi za korosho kwa msimu mmoja? Ekari moja ni miti mingapi?

HABARI,
"Revolution,
Kwa kilimo cha kisasa nikimaanisha mbegu bora za kisasa na kwa mpango wa upandaji bila kuchanganya na mazao mengine heka moja inakaa mpaka miti 100 ma mkorosho uliostawi vizuri unatoa kuanzia kilo 10-20.Kwa hiyo unauhakika wa kuvuna kuanzia tani moja ya korosho kila heka ambayao tani moja sio chini ya milioni 3 kwa bei ya sasa,Hapo utapiga hesabu na heka ulizokuwa nazo au unazotegemea kupanda utapata jibu.
Naliendele wana maajibu yote kwa ujumla kama uko tayari nenda pale.
Contact
Zonal Director (South),
Naliendele Agricultural Research Institute (NARI),
10 Newala Road, P. O. Box 509, Mtwara.
Tel.: +255 732 934 035
Fax.: +255 732 934 103
e-mail: utafiti@iwayafrica.com

LUMUMBA
 
Waache waendelee kukaa mjini, njooni mfanye survey cze nauli haizidi 25,000 ila kumbuka kilimo si cha watu lelemama, hivyo kama uko vizuri njoo kipindi hiki uandae mashamba ya choroko, mbaazi, upupu, Karanga huku ukiusoma mchezo taratibu.
 
hab
Waache waendelee kukaa mjini,njooni mfanye survey cze nauli haizidi 25,000.Ila kumbuka kilimo si cha watu lelemama,hivyo kama uko vizuri njoo kipindi hiki uandae mashamba ya choroko,mbaazi,upupu,Karanga huku ukiusoma mchezo taratibu.

HABARI,
"Ricecooker,
Mkuu asante sana (cze) ni chalinze au na heka moja ni shiling ngapi na kuna uwezekano wa kununua 50,

LUMUMBA
 
hab


HABARI,
"Ricecooker,
Mkuu asante sana (cze) ni chalinze au na heka moja ni shiling ngapi na kuna uwezekano wa kununua 50.

LUMUMBA
Wengi wananua mashamba yenye mikorosho then wanaindeleza kwa kupanda niche mipya,ambapo ikianza kuzaa kwa wingi ndipo hukata ya zamani.Ila kipindi hiki kuuziwa shamba la mikorosho ni shughuli cze in sawa na kuuza kitalu cha madini. Leo benki zote hapa masasi haziingiliki foleni ya kuchukua pesa ni ndefu balaa!

Bei zikiendelea hivi mikoa ya kusini hali itabadilika japokuwa ufujaji wa fedha ni mkubwa kwa baadhi ya wakulima.Ukweli ni kwamba vijana wengi hawana mikorosho hivyo wazee ndio madoni kwa kipindi hiki.

Nawasilisha
 
Wengi wananua mashamba yenye mikorosho then wanaindeleza kwa kupanda niche mipya,ambapo ikianza kuzaa kwa wingi ndipo hukata ya zamani.Ila kipindi hiki kuuziwa shamba LA mikorosho ni shughuli cze in sawa na kuuza kitalu cha madini.Leo benki zote hapa masasi haziingiliki foleni ya kuchukua pesa ni ndefu balaa!Bei zikiendelea hivi mikoa ya kusini hali itabadilika japokuwa ufujaji wa fedha ni mkubwa kwa baadhi ya wakulima.Ukweli ni kwamba vijana wengi hawana mikorosho hivyo wazee ndio madoni kwa kipindi hiki,nawasilisha


HABARI,
Ni kweli ni vijana shida kutaka mafanikio ya haraka haowazee walisha panda mikorosho zaidi ya miaka 20 iliyopita sasa baada ya serikali kusimamia kidete na kuwaondoa walanguzi.Ila kama una shamba na ukiweza kupata mbegu bora ndani ya miaka mitatu unaaza kuvuna na jinsi muda unavyokwenda ndio kiwango cha mavuno kinapoongezeka kwa sasa ni habari njema kwamba hata kanda ya kati mikoa ya tabora singida na dodoma kwa sasa zao hilo linakubali vizuri.

LUMUMBA
 
Huu uzi umekuwa wa msaada sana shukrani kwa wote waliochangia hasa waliotoa mawasiliano ya vituo vya utafiti, naliendele ntawatafuta. wenye taarifa msichoke kwa maswali ya member kama mimi ningependa kujua kama huu upande bagamoyo mpaka msata je hili zao la korosho linakubali?
 
huu uzi umekuwa wa msaada sana shukrani kwa wote waliochangia hasa waliotoa mawasiliano ya vituo vya utafiti, naliendele ntawatafuta. wenye taarifa msichoke kwa maswali ya member kama mimi ningependa kujua kama huu upande bagamoyo mpaka msata je hili zao la korosho linakubali?

HABARI,
"zegebovu1,

Kwa ujumala ni kwamba pwani yote ya bahari ya Hindi Kuanzia Mtwara Mpaka Tanga, Fikiria kama Dodoma, Singida zina kubali huko Bagamoyo, Msata ndio maeneo yake.

LUMUMBA
 
HABARI,
"zegebovu1,
Kwa ujumala ni kwamba pwani yote ya bahari ya Hindi Kuanzia Mtwara Mpaka Tanga ,Fikiria kama Dodoma,Singida zina kubali huko Bagamoyo,Msata ndio maeneo yake..

LUMUMBA

Kweli kabisa mkuu nimepita ukanda wa bagamoyo nimeona namna mikorosho ilivyostawi na kubeba korosho nyingi ilihali haina matunzo kabisa ya kusafishiwa kutifuliwa wala haijawahi kupuliziwa dawa kwa ujumla zinakubali sana ukanda wote wa pwani.
 
Safi kabisa..hizi ndio nondo zenye akili..ngoja nijiongeze kwenye korosho nako.

HABARI,
"Mshuza2,
Kweli Kama unadhamira Hiyo usirudi nyuma,Kama ukiweza kupata mikorosho ile ya kubebesha ya Muda mfupi inaanza Kuto Korosho kuanzia miaka mitatu,Huwa wanasema miaka miwili au mmoja ni kweli ila unakuwa haunanguvu unashauriwa Kutoa mau yote ili uwezi kutengeneza matawi na kuwa na nguvu.

Kwa mikorosho ya kubebesha kwa hekari moja unaweza kupanda mpaka miti 120 kama una heka 1o utakuwa na miti 1200.
Makadirio ya kitaaluma mmkorosho wa kubebeshwa wa miaka mitatu unatoa kuanzia k
Safi kabisa..hizi ndio nondo zenye akili..ngoja nijiongeze kwenye korosho nako.

HABARI,
"Mshuza2,
Kama unania hiyo wahi Mkuu ndani ya miaka 3 Kama ukitumia mbegu ya kubebesha na Kama mambo yote yatakwenda safi kwa upande wa ukuaji na kama utaweka lengo la miti Elfu moja na kundelea utakuwa na kipato cha uhakika sana na kikubwa kwa mwaka,Na hata kama ulikuwa na mawazo ya biashara nyingine ukakosa mtaji hapo kila mwaka unakuwa na mtaji tosha Huangaiki na Bank.

Kwa mti mmoja wa miaka 3 unaweza kuanza kuvuna mpaka kilo 2-3 ikifika miaka 5-10 ni zaidi kilo 30 Pale Dodoma kwenye wilaya ya mpwapwa kunagereza wanayo miti walipanda ya kubebesha ya miaka 10 kila mti unatoa kilo 40 kwa mwaka.Sasa kama ukivuna kilo 2 kwa kila mti kwa miti 1000 ni tani 2 na kwabei ya mwisho wa mwaka huu ilifika mpaka elfu 3800 kwa kilo maana ya sh.Milioni 3.8 kwa Tani ukiwa na tani 2 ni milioni 7.6 hiyo ni kwa kilo 2 kwa mti mmoja sasa piga hesabu ukivuna kilo 5-10 kwa mti utapata jibu Mkuu na hata kama bei ikiwa ni sh.2500 kwa kilo bado unahela nyingi.

Wataalam wakubwa wa mambo ya uchumi wanakwambia matajiri wengi wapya watakaokuja kwa sasa ukitoa mambo ya COMPUTER wengi watatokana na shuguli za kilimo hao ni wataalam waliobobea kwenye mambo ya uchumi.
Usirudi nyuma Ndugu ifanyie kazi.

LUMUMBA
 
Back
Top Bottom