Fahamu mambo haya muhimu kuhusu afya ya mama mjamzito

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,495
9,275
=> Wakati wa ujauzito, unaweza kusikia uchovu mkubwa au usingizi. Mara nyingi uchovu huu upo katika miezi mitatu ya awali.

=> Kama mjamzito, jitahidi kupumzika na kuweka miguu juu kila unapoweza na ulale na mito kati ya miguu yako na ulale mapema

=> Kizunguzungu wakati wa ujauzito ni jambo la kawaida na inaweza kusababishwa na msukumo wa damu (presha) kushuka

=> Kizunguzungu wakati wa ujauzito huweza kusababishwa na sukari ktk damu kushuka, upungufu wa madini chuma mwilini, upungufu wa maji mwilini

=> Kusimama ghafla pia huweza kupelekea mama mjamzito akasikia kizunguzungu. Inashauriwa kama mjamzito, usimame taratibu

=> Je wajua mama mjamzito anaweza kupata kisukari kinachosababishwa na ujauzito? Hujitokeza katika miezi ya 4 mpaka 6

=> Kwa akina mama wajawazito maji ni muhimu kuunda kondo ya nyuma na kuboresha mfuko wa uzazi ili mtoto apate virubutisho muhimu

=> Je unajua mstari mweusi upo mwilini mwa mama mjamzito kwenye tumbo katika hali ya kawaida kabla ya ujauzito lakini hauonekani sana? Huitwa Linea NIgra

=> Uvutaji sigara wakati wa ujauzito huweza kupelekea mtoto kuzaliwa kabla ya wakati wake (mtoto njiti) au kuzaliwa na uzito mdogo

=> Uvutaji sigara wakati na baada ya ujauzito pia huweza kupelekea mtoto kufariki ghafla. Sigara ina kemikali zaidi ya 4,000

=> Nini hupelekea mishipa kutuna wakati wa ujauzito? Kadri mtoto anavyokua, presha huongezeka katika mfuko wa uzazi na mishipa

=> Una uwezekano mkubwa zaidi wa mishipa ya damu kuvimba sana kama ni mjamzito na umebeba zaidi ya mtoto mmoja tumboni

=> Ni vyema kupumzika na kuweka miguu juu mara kwa mara wakati wa ujauzito ili kupunguza mishipa kuvimba sana

=> Je wajua kuwa wakati wa ujauzito na hata baada ya kujifungua, akina mama huweza kupata mfadhaiko (postpartum depression)?

=> Ni muhimu kwa familia kuwa makini na kutomwacha mama mjamzito au mwenye mtoto mchanga ambaye ana huzuni au mawazo bila msaada wa kitaalam

=> Takriban 25% ya akina mama hutokwa na damu kidogo uukeni wakati wa mimba katika miezi mitatu ya mwanzo.

=> Ukitokwa na damu nyingi na maumivu ya tumbo wakati wowote wa ujauzito, kamwone mtaalam mara moja!

PIA UNASHAURIWA KUSOMA MADA HIZI:
- Mama mjamzito : mambo ya kufanya na mambo ya kuepuka kufanya - JamiiForums

- Maumivu ya tumbo chini ya kitovu kwa mama mjamzito: Fahamu visababishi, ushauri na tiba - JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom