Dhana ya "kumbemenda mtoto"

Miss Zomboko

JF-Expert Member
May 18, 2014
4,499
9,279
Kumbemenda mtoto ni mtoto kutokua vizuri ikidhaniwa kutokea kutokana na mama anayenyonyesha mtoto kukutana kimapenzi na mwenzi wake hasa kipindi mtoto bado ni mchanga na ananyonyeshwa.

Hii ni dhana iliyopo katika jamii mbalimbali, na inadhaniwa hutokea kwa sababu mtoto kunyonya maziwa yenye mbegu za kiume zilizoingia kwenye maziwa baada ya kufanya mapenzi.

Je, kuna ukweli wowote?
Hapana. kiukweli na kiutaalamu dhana hii si sahihi kabisa!
kufanya mapenzi na mwenzi wako baada ya kujifungua hakuwezi kusababisha afya ya mtoto kuzorota. mwanamke anapokutana na mwanaume kimapenzi, shahawa huingia kwenye tumbo la uzazi na kubaki huko. haziingii kwenye damu wala haziwezi kufika kwenye maziwa. dhana ya kuwa shahawa huingia kwenye maziwa na kumuathiri mtoto sio sahihi.

Ni baada ya muda gani mwanamke aliyejifungua anaweza kufanya mapenzi?
unaweza kuanza kufanya mapenzi tena baada ya maji maji yenye damu ya uke (lochia) kuacha kutoka ambayo ni kama wiki 3 mpaka 4 baada ya kujifungua, na wewe kujisikia vizuri na kuwa tayari kushiriki katika mapenzi. pia, mnaweza kusubiri mpaka wiki 6 zipite toka ulivyojifungua.

Je, kuna athari yoyote ya kufanya mapenzi baada ya kujifungua?
Kufanya mapenzi baada ya kujifungua hakuwezi kuleta madhara kwa mtoto endapo hamna maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu). ikiwa mwanaume ana vvu anaweza kumuambukiza mama na kisha mtoto kuambukizwa kupitia maziwa ya mama.

Ikiwa mnafanya mapenzi kabla ya damu damu ya ukeni kukata, maambukizi ya bakteria yanaweza kutokea kwenye tumbo la uzazi (endometritis). pia kuna uwezekano wa mama kupata ujauzito miezi 6 ya kwanza ya kunyonyesha.

Nini kinasababisha afya ya mtoto kuzorota?
Kama tulivyoona, kufanya mapenzi hakusababishi mtoto kubemendwa. afya ya mtoto inaweza kuzorota kutokana na sababu mbalimbali zikiwemo;

  • Kukosa maziwa ya mama ya kutosha
  • Mtoto kushindwa kunyonya vizuri
  • Kuanzishiwa vyakula vya ziada mapema, kabla mtoto hajafikisha miezi 6 au vyakula visivyo na viritubisho vya kutosha.
  • Homa, nimonia na maambukizi ya mfumo wa mkojo (uti) za mara kwa mara.
  • Maambukizi ya magonjwa kama virusi vya ukimwi (vvu) au kifua kikuu.
  • Matatizo ya moyo ya kuzaliwa nayo (congenital heart diseases).
Kufanya mapenzi na mwenzi wako hakusababishi mtoto kubemendwa. Baada ya kujifungua mtoto hutegemea kupata lishe bora kutoka kwenye maziwa ya mama, hivyo nyonyesha mtoto wako vizuri. ukiona ukuaji wake unazorota, onana na daktari.
 
Kumbemenda mtoto ni neno linalomaanisha kudhoofika kwa afya ya mtoto wakati akiwa katika miezi ya kwanza ya kunyonya ziwa la mama. Kama msomaji alivyoeleza inahusishwa na mama kutembea nje au kuwa na nyumba ndogo wakati ananyonyesha. Kwa imani za vatu wengi ni kuwa tendo hilo huchafua maziwa ya mama na kumdhuru mtoto anaponyonya. Wakati mwingine humhusisha hata baba wa mtoto kuwa amenaza kujamiiana na mama mapema na huvyo kumdhuru mtoto. Kwa wale tunaofuatilia imani za zamani,kuna imani nzuri ambazo zilikuwa zikilenga kuwakinga vatu na madhara ya kiafya lakini kadri situ zinavyoenda sayansi inaondoa imani hizo hata kama zilikuwa nzuri.

Kumbemenda mtoto kunatokana na ukweli kuwa wazee waliwashauri wazazi kuwa mtoto anapozaliwa basi hakuna kujamiiana mpaka mtoto atimize mwaka mmoja hadi miwili kwa kuwatisha kuwa mtoto atadhurika. Hii ilikuwa inasaidia kumuepusha mama na mimba wakati ananyonyesha na ilisaidia kupanga uzazi. Imani hii ilikuwa na nia nzuri japo ilikuwa inawanyima haki ya kujamiiana vatu walioowana kwa mda mrefu na kuchochea wanaume kuwa na wapenzi wa nje wakati wanasubiri mda ufike. Kwa kipindi hiki cha maradhi ya Ukimwi imani hii ni hatari kwani kama mwanaume atatoka nje ni rahisi kuleta maambukuzi ya virusi kwenye ndoa au mahusiono.

Ukweli ni kwamba hakuna uhusiano wa moja kwa moja wa afya ya mtoto na kujamiiana kwa mama. Hata hivyo zipo sababu za kisayansi na za kijamii zinazohusishwa na kudhoofika kwa afya ya mtoto mama anapojihusisha na mambo yanayochanganya kisaikolojia ikiwamo ngono.

Kwanza, ukiwa unanyonyesha kuna kichiocheo (homone) mwilini kwa ajili ya kumsaidia mama kutoa maziwa ya mtoto na iwapo atakuwa na mpenzi anayemchanganya ni rahisi kukatika kwa homoni hiyo na mtoto kukosa maziwa ya kutosha hivyo kukosa virutubisho. Matokeo yake ni kudhoofika kwa afya ya mtoto.

Pili, iwapo mama atashika mimba wakati ananyonyesha pia atambemenda mtoto. Hii ni kwa sababu mimba inapotunga inahitaji virutubisho vingi kiasi kwamba mwili wa mama hautaweza kutoshereza kwa kiumbe tumboni na kwa ajili ya maziwa ya mtoto.


Hivyo bado mtoto atakosa afya kama vyakula mbadala havitakuwepo ataendelea kudhoofu. Tatu, hata kama mama siyo mpenda ngono lakini akawa mvivu kumnyonyesha mtoto wala kumpa chakula mbadala, mtoto atakuwa na matatizo ya kiafya. Nne, mama anaweza kuwa anatimiza wajibu wake lakina bado mtoto akawa na magonjwa kama malaria, magonjwa ya koo, sikio. Hivyo akawa anaumwa tu na waswahili wakuchulia mama anafanya ngono nje.

Swali la pili linasema: Ni kitu gani mama afanye ili aweze kuinusuru afya ya mwanae? Atumie nini ili aweze kuepusha haya? Na kama mwanamke amefanya ngono na mwanaume mwingine afanyeje ili awe msafi asimdhuru mtoto?

Cha kufanya ni kuhakikisha mama anampa mtoto nafasi ya kunyonya vizuri kwa mda mrefu na akumbuke kuwa kipindi cha miezi sita ya kwanza ni muhimu sana kwa vile maziwa ya mama yanakuwa na virutubisho vya kutosha kujenga mwili na akili ya mtoto. Baada ya miezi sita mtoto anaweza kuendelea kunyonya hadi miezi 24 lakini iwapo mama hana nafasi sana anaweza kuanza kumlisha chakula bora kwa makuzi ya mtoto.

Kuhusu lini unaruhusiwa kuanza kujamiiana na mwezio baada ya kujifungua, ukweli ni vizuri kusuburi angalau siku 40 ili kujiweka sawa halafu mama anaweza kuendelea kujamiiana kwa kuzingatia uzazi wa mpango na maradhi ya ngono ikiwa ni pamoja na Ukimwi.
 
Kumbemenda mtoto inaitwaje kibaiolojia? inasababishwa na nini kikubwa? na muathirika anaweza kupata tiba hospital?

Epuka majibu ya hisia na mizaha....nawasilisha
 
Unamaanisha kumtoboa mtoto masikio? ( kugegeda wakati mtoto akiwa ana 3 month below)
 
Kumbemenda mtoto inaitwaje kibaiolojia? inasababishwa na nini kikubwa? na muathirika anaweza kupata tiba hospital?

Epuka majibu ya hisia na mizaha....nawasilisha

Hta mie sielew ngoja wataalam waje kutupa elimu mana cye wa uzaz wa kwanza vitu ving hatuvijui
 
Kubemenda mtt nijuavyo mm ni pale mama unapokua unanyonyesha,ukawa na mahusiano na mwanaume tofauti na mmeo au baba mtt,hiyo hupelekea mtt afya yke kutetereka,kama amefikia kutembea utasubiri sana,mtt ataishia kukaa tu,hapigi hatua yoyote zaidi ya afya kudhoofu!huko ndio kumbemenda mtt!
 
Kubemenda mtt nijuavyo mm ni pale mama unapokua unanyonyesha,ukawa na mahusiano na mwanaume tofauti na mmeo au baba mtt,hiyo hupelekea mtt afya yke kutetereka,kama amefikia kutembea utasubiri sana,mtt ataishia kukaa tu,hapigi hatua yoyote zaidi ya afya kudhoofu!huko ndio kumbemenda mtt!

Sawa, kwhy mama anaenyonyesha anaweza akaendelea kukutana na mumewe bila kipingamiz chochote! na mtoto asiathirike?
 
Nahisi kama upo sahihi, je kwa wale wanaume ambao wanawake wengi haswa waislam inakuwaje hapo? Maana lazima afanye mzunguko na hata huyu mama mzazi apite alale kwake je hawezi kumbemenda?

Kubemenda mtt nijuavyo mm ni pale mama unapokua unanyonyesha,ukawa na mahusiano na mwanaume tofauti na mmeo au baba mtt,hiyo hupelekea mtt afya yke kutetereka,kama amefikia kutembea utasubiri sana,mtt ataishia kukaa tu,hapigi hatua yoyote zaidi ya afya kudhoofu!huko ndio kumbemenda mtt!
 
Sawa, kwhy mama anaenyonyesha anaweza akaendelea kukutana na mumewe bila kipingamiz chochote! na mtoto asiathirike?

Sawia kabisa. Imajin umelipa jibaba utamu, likawa linanyonya hoteli ya mwanao, linakushika na mikono yake michafu kwenye nyonyo.... afu waenda mnyonyesha mwanao unategemea atakuwa anakula nini huyo baby?
 
Sawia kabisa. Imajin umelipa jibaba utamu, likawa linanyonya hoteli ya mwanao, linakushika na mikono yake michafu kwenye nyonyo.... afu waenda mnyonyesha mwanao unategemea atakuwa anakula nini huyo baby?
babu umezungumza vyema sana,
kikubwa ni usafikwa mama na baba pia, mama anatakiwa akitoka kukutana na mume anapaswa kujisafisha na kufanya joto la mwili kupungua baada ya mihemko yake, kisha ndio aendelee kumshika na kumhudumia mtoto.
Baba nae pia sio anatoka kupiga cha fasta huko chocho akirurudi home anashika mtoto na mijasho yake....
 
ukijua mume sio muaminifu,akirudi asimguse mtt kabla hajaoga
pia baada ya kukutana nae hakikisha unajiswafi thn endelea
na mtt,ila kwa mwanaume muelewa akijua katoka kwny uchafu wake
hatothubutu kumgusa mtt!!
 
Kumbemenda mtoto inaitwaje kibaiolojia? inasababishwa na nini kikubwa? na muathirika anaweza kupata tiba hospital?

Epuka majibu ya hisia na mizaha....nawasilisha

naomba nitumie lugha hiyohiyo"kubemenda". Hapa suala la usafi linahusika sana hata mama na baba wa mtoto wanaweza kuchangia ubemendaji wa mtoto, nikiwa na maana kwamba baba au mama ametoka kwenye shughuli za jasho vumbi bado kwenye daladala ugusane na jasho la watu wa kila aina alafu mkifika hom bila hata kuoga mnafanya kale kamchezo kakikubwa mara mtoto nae anataka chakula yake toka kwa mama, mama nae anamnyonyesha mtoto hivyohivyo,sasa lile jasho na ule uchafu wa kutwa mzima mtoto anabukia kupitia mama yake,hapo ni lazima afya ya mtoto idhoofu...cha kuzingatia ni USAFI tu!
 
Back
Top Bottom