Fahamu makosa na adhabu zitolewazo na sheria zinazokataza matumizi ya mifuko ya plastiki Tanzania

BEHOLD

JF-Expert Member
Nov 17, 2013
5,057
10,715
*FAHAMU MAKOSA NA ADHABU ZITOLEWAZO NA SHERIA ZINAZOKATAZA MATUMIZI YA MIFUKO YA PLASTIKI TANZANIA*

*By Omari Kilwanda-Wakili*

Kimsingi kuna *Makosa Makuu Matano* yaliyotajwa na kukatazwa ndani ya Sheria husika. Sheria hiyo Ndogo inajulikana kama *The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019*. Sheria hii Ndogo imetungwa kwa Mujibu wa Kifungu Na. 230 (2) (f) cha Sheria inayojihusisha na Usimamizi wa Mazingira *(The Environmental Management Act, Cap. 191)*.

*A: MAKOSA*
Kwa mujibu wa Kifungu/Kanuni Na. 8 Cha Sheria ya Kuzuia Matumizi ya Mifuko ya Plastiki ambayo ni *The Environmental Management (Prohibition of Plastic Carrier Bags) Regulations, 2019* kuna Makosa Matano ambayo ni;
(A). Kuzalisha na Kuagiza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 a )*;
(B). Kusafirisha nje ya nchi Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 b )*;
(C). Kuhifadhi na Kusambaza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 c )*;
(D). Kuuza Mifuko ya Plastiki, *(Kifungu/Kanuni Na. 8 d )*;
(E). Kumiliki na Kutumia Mifuko ya Plastiki? *(Kifungu/Kanuni Na. 8 e )*.

*B: ADHABU*
Kwa kila kosa tajwa hapo juu, Sheria husika imetaja Adhabu yake. Hivyo basi kuna Adhabu aina tano kama ilivyo kwa Makosa husika. Kifungu/Kanuni Na. 8 cha Sheria tajwa hapo kilichotaja Makosa Matano ndicho hicho kimetaja Adhabu ya kila Kosa kama ifuatavyo;

(A). *Adhabu kwa Wazalishaji na Waagizaji.*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (a) cha Sheria tajwa hapo juu, kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 20 na isiyozidi Billioni 1*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miaka Miwili*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(B). Adhabu kwa Wasafirishaji kwenda nje ya nchi.*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (b) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 5 na isiyozidi Milioni 20*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miaka 2*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(C). Adhabu kwa Wanaohifadhi na Wasambazaji*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (c) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Milioni 5 na isiyozidi Milioni 50*,
ii. Kifungo Kisichozidi Miaka 2,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(D). Adhabu kwa Wauuzaji*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (d) cha Sheria tajwa hapo juu kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Laki 1 na isiyozidi Laki 5*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Miezi 3*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo juu.

*(E). Adhabu kwa Watumiaji na Wanaomiliki*
Kifungu/Kanuni Na. 8 (e) cha Sheria tajwa hapo kinataja Adhabu kwa Mtu au Watu hao kama ifuatavyo;
i. Faini isiyopungua *Elfu 30 na isiyozidi Laki 2*,
ii. Kifungo Kisichozidi *Siku 7*,
iii. Au vyote *Kifungo na Faini* tajwa hapo.
 
Bora hata serikali ingeanza kwanza kufunga viwanda vya mifuko then wazuie mifuko kutoka nje kuliko hii haraka waliyotumia maana muda sio mrefu tutaanza kuona visanga kati ya MIGAMBO na watumiaji wa mifuko
 
True ilikuwa wala haina haja ya kutoa matanko au kudeal na watumiaji moja kwa moja
 
... awali ya yote naomba kuuliza hivi kosa la uvunjaji wa hii sheria linaangukia katika kundi la makosa ya jinai au sio jinai? Kwa mfano, nikivunja hicho kifungu cha mwisho yaani kama mtumiaji na nikatiwa hatiani nikalipa hiyo elfu 30 au kifungo cha siku 7 au vyote nakuwa nimetenda jinai? Nauliza hivi kwa sababu makosa ya jinai yana implications zake kwa maisha ya mhusika hapo baadaye tofauti na makosa mengine. Wajuvi nisaidieni.
 
Sio kweli watu wengi huwa wakimaliza kutumia mifuko huwa wanaitumia kuwashia moto au kuwekea uchafu so kama viwanda vingefungwa mifuko ingepitia taratibu

Hili tangazo limefanya watu waanze kuzitunza mifuko kwa matumizi ya muda mrefu hasa vijijini
Hata ufunge viwanda miaka kumi ijayo mifuko itakuwepo tu, ufumbuzi ni kila atayebeba mzigo apate adhabu.
 
Kwawale wanaoitumia kama kings ya ukimwi je? Bora kufungwa wiki lkn usiukwae ukwimi...Tunahangaika na mifuko tunaacha mambo muhiiimu watu hata maji hawana!! Ipi hatari kunywa maji machafu au tumifuko huko
 
... awali ya yote naomba kuuliza hivi kosa la uvunjaji wa hii sheria linaangukia katika kundi la makosa ya jinai au sio jinai? Kwa mfano, nikivunja hicho kifungu cha mwisho yaani kama mtumiaji na nikatiwa hatiani nikalipa hiyo elfu 30 au kifungo cha siku 7 au vyote nakuwa nimetenda jinai? Nauliza hivi kwa sababu makosa ya jinai yana implications zake kwa maisha ya mhusika hapo baadaye tofauti na makosa mengine. Wajuvi nisaidieni.
Makosa ya kuzalisha, kuhifadhi, kusambaza, kuuza na kutumia mifuko ya plastiki ni ya jinai.
Ingawa watu wengi tunaona udhaifu wa adhabu ndogo ya mtumiaji (Siku 7 jela, faini alfu 30) , lakini naamini wengi watapata kesi ya kuhifadhi mifuko hiyo ambayo adhabu yake iko juu.
Kujiandaa na sheria hii tuhakikishe tunaondoa mifuko ya plastiki kwenye maeneo ya nyumba zetu
 
IMG-20190521-WA0021.jpg
 
... duh! Hatari sana hii. Kwa hiyo nikitiwa hatiani na kupigwa faini ya elfu 30 automatically nakuwa nimekosa baadhi ya haki zangu za kiraia hapo baadaye. Mfano, sitaruhusiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia wa mtaa hadi urais hap baadaye! Kutakuwa na kesi nyingi sana za kubatilisha matokeo ya chaguzi na mapingamizi huko tuendako.
 
mifuko Hii ni miepesi, utaondoa eneo lako, upepo utaileta nawe utakuwa mtunzaji. Ukusanyaji endelevu ni muhimu, mingi imezagaa.
 
... duh! Hatari sana hii. Kwa hiyo nikitiwa hatiani na kupigwa faini ya elfu 30 automatically nakuwa nimekosa baadhi ya haki zangu za kiraia hapo baadaye. Mfano, sitaruhusiwa kugombea nafasi yoyote ya uongozi kuanzia wa mtaa hadi urais hap baadaye! Kutakuwa na kesi nyingi sana za kubatilisha matokeo ya chaguzi na mapingamizi huko tuendako.
Nalo neno. Kuna mifuko itarushwa uani kwa mgombea ili ashitakiwe, afungwe, ili asigombee.
 
Nishaanza kutoa mifuko yote iliyokuwa ndani na kuichoma,Hii serikali ilivyo na shida na hela na polisi nao wanasubiri kwa hamu kuanza kupata za kubrashia.
 
Kwawale wanaoitumia kama kings ya ukimwi je? Bora kufungwa wiki lkn usiukwae ukwimi...Tunahangaika na mifuko tunaacha mambo muhiiimu watu hata maji hawana!! Ipi hatari kunywa maji machafu au tumifuko huko
Huko Rukwa na Tabora wanaitumia kuzalishia akinamama!
 
Back
Top Bottom