Fahamu: Maeneo 10 usiyoruhusiwa kutembelea duniani

Sam Gidori

Senior Member
Sep 7, 2020
165
414
1. Mapango ya Lascaux, Ufaransa
Mapango ya Lascaux nchini Ufaransa yanajulikana kama duniani kwa kuwa na moja ya michoro ya kale zaidi, yakiwa na michoro ya zaidi ya miaka 17,300 iliyopita. Michoro hiyo inaonesha mwanadamu akifuga wanyama kama ng’ombe. Lakini mapango hayo yamefungwa tangu mwaka 1963, wanasayansi wakiamini kuwa uwepo wa binadamu unaweza kuharibu michoro hiyo.

106_deuxieme_taureau.jpg

Picha: SPL Lascaux international

2. Kisiwa cha Sentinel Kaskazini, India
Kisiwa hiki kilichopo katika mnyororo wa visiwa vya Andaman kinakaliwa na watu wa kabila la Sentinel. Wakazi wa kisiwa hiki wanajulikana kutumia njia yoyote, ikiwamo mishale yenye sumu kuwafukuza wageni wanaojaribu kuingia katika visiwa hivi. Wasentinel wameishi kisiwani hapo kwa zaidi ya miaka 50,000. Ni hatari kutembelea kisiwa hiki, na Serikali ya India imeweka marufuku kwa watu kuingiliana na wakazi wa kisiwa hicho.

north-sentinel-island_1.jpg


3. Kisiwa cha Surtsey, Iceland
Hiki ni kisiwa kinachotajwa kuwa moja ya visiwa vipya kabisa duniani. Kisiwa hiki kimetokana na mlipuko wa volcano uliodumu kwa miaka minne. Wanasayansi wachache na wanageolojia ndio wanaoruhusiwa kutembelea kisiwa hiki, lengo likiwa ni kutunza mabadiliko ya kiikolojia yanayojitokeza katika kisiwa hiki.

surtsey-volcano-island-iceland.jpg


4. Kisiwa cha North Brother, Marekani
Kisiwa hiki chenye ukubwa wa eka 13 kipo karibu na mji wa New York nchini Marekani na kiliwahi kutumika kama hifadhi kwa zaidi ya abiria 1,000 walionusurika katika ajali ya meli iliyotokea karibu na kisiwa hicho. Umaarufu wa kisiwa hicho ulitokea baada ya kutumika kama Karantini kwa mgonjwa wa kwanza wa Typhoid nchini Marekani, Mary Mallon aliyejulikana zaidi kama Tyohoid Mary mwanzoni mwa miaka ya 1900. Baadaye, kisiwa hicho kilitumika kama sehemu ya kubadilisha tabia kwa wahanga wa madawa ya kulevya (rehab). Kisiwa hicho kimetelekezwa tangu miaka ya 1960; kwa sasa ni makazi ya ndege na hakuna mtu anayeruhusiwa kukitembelea.

North-Brother-Island-15-Morgue-plant-from-dock.0.0.1450311800.0.jpg



5. Kisiwa cha Nyoka, Brazil
Kama jina lake lilivyo, kisiwa hiki ni makazi ya maelfu ya nyoka hatari na wenye sumu kali. Nyoka waliopo katika kisiwa hicho wanatajwa kuwa na sumu kali mara tatu hadi tano ya nyoka waliopo katika maeneo mengine. Hakuna mwanadamu mwenye uthubutu wa kutembelea kisiwa hicho na serikali ya Brazil imetunga sheria kuzuia watu kutembelea kisiwa hicho.

AAIlhaQueimadaAmazon_Clipper_Wilderness_animals_9.jpg


6. Area 51, Marekani
Eneo hili linalomilikiwa na Jeshi la Marekani lipo katika jangwa Kusini mwa Jimbo la Nevada. Uwepo wake umekuwa ukitawaliwa na nadharia nyingi kwa muda mrefu, ikiwamo nadharia maarufu kuwa eneo hilo linatumika kuhifadhi viumbe kutoka sayari nyingine (alliens). Jeshi la Marekani limekuwa likisisitiza kuwa eneo hilo linatumika katika majaribio ya ndege za kijeshi na silaha za kivita. Ni marufuku kutembelea au kupiga picha eneo hilo.

Screen-Shot-2017-09-21-at-11.38.58-PM.png


7. Kaburi la Qin Shi Huang, China
Qin Shi Huang anatajwa kuwa Mtawala wa Kwanza wa China, aliyetawala kati ya mwaka 247 hadi 221 KK, alizikwa katika kaburi maalum, lililokuja kugunduliwa zaidi ya miaka 2,000 baadaye, mwaka 1974. Kaburi la ‘mtemi’ huyo linatajwa kuwa na vitu atakavyovihitaji katika maisha yake baada ya kifo, ikiwamo 'wanajeshi' zaidi ya 8,000 watakaomlinda huko alipo. Baada ya kugunduliwa, serikali ilikataza watu kutembelea eneo hilo ili kuendelea kutunza eneo hilo la zamani.

muzej.jpg


8. Kisiwa na Niihau, Marekani
Hiki ni kisiwa kilichopo Magharibi mwa Visiwa vya Hawaii nchini Marekani, kikiwa na wakazi takriban 170 tu. Kisiwa hiki kilinunuliwa na mkulima na mfanyabiashara, Elizabeth Sinclair mwaka 1864, na tangu wakati huo, hakuna mtu mwingine anayeruhusiwa kutembelea kisiwa hicho zaidi ya ndugu wa karibu, wanajeshi wa Marekani, viongozi wa serikali na wageni waalikwa pekee.

niihau_1.jpg


9. Kisiwa cha Heard, Australia
Hiki ni moja kati ya visiwa visivyotembelewa zaidi na watu duniani. Kisiwa hiki ni eneo la nje la Australia na kipo katikati ya Kisiwa cha Madagaska na Bara la Antaktika. Ni kisiwa kilichoundwa kwa miamba ya volkano, kikiwa na volcano hai mbili, na kwa sehemu kubwa halina uoto wa asili. Serikali ya Australia iliweka marufuku ya kutembelea kisiwa hicho kutokana na kuwa na hali ya hewa isiyotabirika, uwepo wa volkano hai na umbali uliopo kati ya kisiwa hicho na eneo la karibu la nchi kavu. Huchukua takriban wiki mbili kufikia eneo la karibu la nchi kavu, hivyo kuongeza hatari ya kuwepo katika kisiwa hicho.

10723254-16x9-2150x1210.jpg


10. Doomsday Vault, Norway
Hii ni benki (ghala) ya mbegu iliyojengwa kwa lengo la kutunza aina tofauti za mbegu duniani ili kuhifadhi mimea hiyo isitoweke. Mamilioni ya mbegu hutumwa kutoka kila kona ya dunia ili kuhifadhiwa katika benki hii ya mbegu kwa ajili ya “Siku ya Kiama”. Ili kuhakikisha uhifadhi wa muda mrefu wa mbegu hizi, benki hii hufunguliwa kwa watu maalum na kwa siku maalum tu.

1200x773.jpg
 
Namba 2 hao jamaa wanaishije bila kuhusiana na watu wengine??.Kwa hiyo hata Serikali ya Australia imeshindwa??.
 
Kibongo bongo zipo,naifahamu ile ya Arusha na hata SUA Wana kitu km hicho.
Lakini mkuu sidhani kama hizi za kibongo zina ulinzi wa kutosha kama hii inayozungumziwa hapa. Isitoshe malengo ya kuwepo kwa hii benki ni ya kiama kwa maana nyingine ni kwamba hilo jengo litakuwa limejengwa ktk hali ya kuhimili majanga yoyote yale huku ulinzi ukiwa umeimarishwa maradufu
 
10 Reactions
Reply
Back
Top Bottom