kadoda11
JF-Expert Member
- Jan 6, 2011
- 21,453
- 20,712
Special presidential division(SPD) ni kikosi maalumu cha jeshi alichounda mzee Mobutu mwenyewe mwaka 1985 kwa jukumu la kumlinda yeye na familia yake pia kushughulikia maadui wote wa mzee kwa namna ambayo wao SPD waliona inafaa.
Wanajeshi wa SPD walikuwa wanapewa mafunzo maalum na washauri wa kijeshi toka jeshi la israel ambao kwa namna moja ama nyingine walikuwa na ushirika na mzee mobutu enzi za utawala wake.
Kamanda wa SPD alikuwa ni binamu yake na mzeee mobutu aliyefahamika kwa jina la Etienne Nzimbi Ngbale Kongo wa Basa ambaye pamoja majukumu mengine alihakikisha recruitee wote wa SPD wanatoka katika kabila la mzee Mobutu. ikumbukwe Mobutu alikuwa ni wa kabila la Ngbandi linalopatikana Kaskazini mwa DRC.
Mzee Mobutu aliitumia SPD kwa ufanisi mkubwa sana katika kukabiliana na maadui/washindani wake wa kisiasa.SPD ilitumika kuteka, kuua, kutesa, kuonea, kunyanyasa, kutisha na kupoteza watu kimyakimya, kuwaweka watu kizuizini, kufunga watu jela bila kesi, kutengeneza matukio ya kipropaganda nk. matukio yao yalikuwa ni zaidi ya matukio ya kikundi cha ''watu wasiojulikana''.
Hiki ndio kikosi ambacho moja ya makapteni wake alikuwa ni mtoto mtukutu wa mzee Mobutu na mtu wa kula bata aliyefahamika kwa jina la Kongulu Mobutu almaarufu Sadam Hussein(sadam sene). kwa wale wadau wa band ya wenge bcbg hili jina sio geni kwao maana jina lake limetajwa sana katika nyimbo za band hiyo zilitoka miaka ya tisini.
Miaka ya mwisho ambayo mzee Mobutu alikuwa anaelekea kupoteza ushawishi wa kuitawala Zaire, Kongulu alichukua jukumu la kuki-command kikosi cha SPD ambapo alihakikisha maadui wa baba yake ndani ya Zaire wanashughulikiwa barabara.
Kongulu alifariki mwaka 1998 jijini Monaco kwa maradhi ya ukimwi.
NB:
Nimeitafsiri kutoka nyanzo mbalimbali vya kwenye mtandao. karibuni kujazia nyama.