Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,196
- 25,516
Waungwana na wazalendo wa Tanzania mliopo JF nawasalimu,
Sasa ni Dhahiri kuwa Maalim Seif Sharrif Hamad amehama CUF na kuhamia ACT-Wazalendo. Kuanzia jana, kumekuwa na kuweweseka mno kwa makada wa CCM mitandaoni 'wakijikaza kisabuni' kwa kusema kuwa Maalim Seif ameikacha CHADEMA na kujiunga na ACT-Wazalendo iliyo chini ya Zitto Zuberi Kabwe Ruyagwa.
Mwaka 2015, CUF iliyokuwa ikiongozwa na Maalim Seif na Lipumba (kabla Lipumba hajajiweka mbali nao wakati wa uchaguzi) ilishirikiana na CHADEMA na vyama vingine vya NCCR-Mageuzi na NLD katika mwamvuli wa UKAWA. Makada wa CCM walipiga propaganda kuwa huo ulikuwa ni mwanzo wa CUF ya Maalim Seif kumezwa na CHADEMA ya Mbowe.
Ndiyo maana, ulipoibuka mgogoro mkubwa ndani ya CUF kufuatia Prof. Lipumba kurudi madarakani kama Mwenyekiti wake, makada wa CCM walikuwa wakimuunga mkono na kumpigia chapuo Prof. Lipumba. Ilikuwa ni njia ya 'kulipa kisasi kisiasa' kwakuwa tu Maalim Seif alishirikiana na CHADEMA hata kuwapa Mgombea Mwenza mwaka 2015 (Juma Duni Haji).
Propaganda ya kuwa CUF iliyokuwa ikiitwa ya Maalim kudhibitiwa na kumezwa na CHADEMA iling'ang'aniwa na hata kutangazwa vilivyo. Wakati huo, makada wengi wa CCM mitandaoni ikiwemo humu walikuwa upande wa CUF-ya-Lipumba. Maalim Seif alisemwa kuwa amedhibitiwa, anaendeshwa na kuamuliwa na CHADEMA ya Mbowe.
Hatimaye, jana Maalim Seif amejiunga na ACT-Wazalendo badala ya CHADEMA. Maalim Seif (yawezekana alikuwa akizifuatilia propaganda dhidi yake kwa umakini mkubwa) amefanikiwa kuruka kigingi cha propaganda hizo. Watungaji na wasambazaji wa propaganda hizo wamebaki wakiduwaa na kugosagosa wasijue la kufanya au kusema. Wanaweweseka!
Maalim Seif, kisiasa, anajitosheleza. Historia yake tangu akiwa masomoni inambeba ndani ya chama chochote kiwacho. Hakuna chama chochote cha siasa hapa Tanzania ambacho kinaweza kummeza Maalim Seif na kumfanya kuwa ni mwanasiasa wa 'kawaida' hasa kwenye siasa za Zanzibar. Ndiyo maana kuhama kwake kunafuatwa na kuhama kwa mamia ya wafuasi wake.
Kuhamia kwakeACT-Wazalendo badala ya CHADEMA ni pigo kwa makada wasio makini wa CCM. Ndiyo maana hawaachi kujipa Imani na kujikaza kisabuni kwa kubadili chenga hiyo kama kuikacha CHADEMA. Maalim ni mwanasiasa nguli na mbobezi. Anaweza 'kushaini' popote atakapojiunga. Kama kushirikiana kisiasa, alipo hapatakuwa ni kikwazo kwake.