Fahamu kwanini jk kashinda sehemu kubwa zaidi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Fahamu kwanini jk kashinda sehemu kubwa zaidi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by PAS, Nov 4, 2010.

 1. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #1
  Nov 4, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Katika kipindi kilichopita cha kampeni za vyama, kila mgombea alijinadi kwa sera zake ikiwemo CCM ambao walitoa ahadi za kufa mtu ili mradi tu wapate kura za wananchi..
  CCM ili ishinde mbinu wanayotumia ni kudhoofisha sekta ya elimu ili wananchi wasijue kamwe au wasielewe vizuri kuhusu haki zao za kijamii,kiuchumi na kisiasa.
  Ukitaka kuona ilo katika elimu wao wanadanganya watu ktk kampeni kua shule zimeongezeka zaidi, lakini kiukweli hakuna walimu, vifaa,hata kama wapo walimu wachache basi mazingira ma malipo ya kazi ni mabaya.

  Mfano mzuri alipokua kule mkoa wa manyara JK aliahidi maji kutoka mto ruvu, kwa watu ambao hawajui jografia wataona ni kitu rahisi hivyo wakampa kura .. Je hayo maji yavuke mito yote mikubwa kama wami, mito ya tanga moshin na mbaya zaidi hata ile ya jirani yao Arusha???
  Loooh!!!! Kweli elimu wanayowapa ndugu zetu wasio wa mijini haitaweza kuwabadilisha hata ikifika 2015 mana ccm wamejiwekea mizizi ya UBINAFSI,TAMAA,Roho mbaya,Ukatili n.k.
  Hii ni ule utawala waliotumia wakoloni (indirect method) ktk kawagawanya waafrika enzi hizo, na hadi leo bado waafrika walio wengi wanawaona wazungu kama mungu wao(wakoloni walipokuja afrki waliangalia lugha ya wenyeji na kuongezea maneno yao PIA WAKIJIFANYA NI WAMISHONARI ili tuwasujudie mfano walisema wao wanaitwa MZUNGU na aliewatuma kazi ya umishonari ni MUNGU.
  Wito wangu kwa wanaJF hata kama kuna mtu wa chama gani tubadilike ili tuondokane na ilo janga mana nchi yetu ipo nyuma
  .
  .
  TAFAKARI CHUKUA HATUA....haki elimuuuuu:A S-danger::A S-danger:
   
 2. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #2
  Nov 4, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Watanzania hawadanganyiki kama wewe unavyodhani.
   
 3. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #3
  Nov 4, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  wewe upo eneo gani kwasasa tz???
  ebu angalia majimbo yaliyochukuliwa ya ccm ni yale ya kwenye majiji.. pia na sehemu zile za mipakani ambapo kuna fujo watu hawakubali haki zao kuibiwa lakini hapa katikati ya nchi watu hawajielewi kabisaaa mdau..
  mbona mayara wamekubali maji ya ruvu
   
 4. Bongolander

  Bongolander JF-Expert Member

  #4
  Nov 4, 2010
  Joined: Jul 10, 2007
  Messages: 4,882
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 135
  Mkuu unahakika na unachosema? Kama kweli mtu ana akili timamamu anaweza kuona wazi kuwa huu ni uongo. I can assure you kuwa kaa tukiendelea ufuatiliaji wa utekelezaji wa ahadi hizi naweza kukwambia kuwa unaweza kuwa wa kwanza kulia.

  Unajua inachukua muda gani kuufanya mji uwe wa viwanda? Can you beleieve that JK ana uwezo wa kufanya hata wilaya iwe ya viwanda?
  Can you believe that kuna uwezekano wa kujenga barabara hata moja? Miaka mitano iliyopita hawajenga barabara hata moja, sasa kuna uwezekano wa kujenga barabara kweli? Hizi ndio ahadi za JK, kama kweli unaakili unajua kabisa kuwa hii ilikuwa danganya toto.

  1. Kujenga reli mpya kutoka Dar es Salaam mpaka mikoa ya Kanda ya ziwa-Nzega, Tabora

  Mkoa wa Tanga kuwa Jiji la Viwanda- Tanga mjini
  Tabora kutumia maji ya Ziwa Victoria-Igunga
  Kulipa madeni ya chama cha Ushirika mkoa wa Shinyanga (SHIRECU)- Shinyanga
  Kumaliza migogoro ya Ardhi nchini- Dodoma
  Wakulima kuacha kutumia jembe la mkono-Dodoma mjini
  Kuwapatia trekta wakulima -Kata ya Mrijo, Dodoma
  Wananchi kutoondolewa kwenye Ranchi ya Misenyi-Kagera
  Kujenga Uwanja wa Ndege Misenyi-Kagera
  Kupanua Uwanja wa Ndege Bukoba-Bukoba Mjini
  Kujenga uwanja wa ndege mkubwa Kigoma - Kigoma Mjini
  Mtukula kupatiwa umeme kutoka Uganda- Kagera
  Mikoa ya Kagera, Kigoma, Lindi, Rukwa na Ruvuma kuunganishwa katika gridi ya taifa ya umeme- Kagera
  Kuimarisha Takukuru kwa miaka mitatu-Kagera
  Hukumu kwa waliopatikana na hati ya kuua albino- Mbeya
  Kununua meli kubwa kuliko MV Bukoba-Kagera
  Kuanzisha benki ndogondogo kwa ajili ya wajasiriamali
  Serikali kuvisaidia vyama vya ushirika-Mwanza
  Kuimarisha usalama Ziwa Victoria na Ziwa Tanganyika kwa kupeleka kikosi maalum chenye vifaa kupambana na wahalifu-Mwanza
  Wilaya ya Geita kuwa hadhi ya mkoa Januari mwakani- Geita
  Kulinda muungano kwa nguvu zote-Pemba
  Kuwajengea nyumba waathirika wa mafuriko Kilosa-Morogoro
  Kununua meli mpya kubwa Ziwa Nyasa-Mbeya mjini
  Kujenga bandari Kasanga –Rukwa
  Kumaliza tatizo la walimu miaka mitano ijayo - Songea
  Kufufua mgodi wa makaa ya mawe Kiwira -Mbeya
  Kuzuia hatari ya kisiwa cha Pangani kuzama- Tanga
  Kununua bajaji 400 kwa ajili ya kubeba wajawazito hasa vijijini- Iringa
  Kujenga barabara yenye kiwango cha lami kutoka Same mpaka Kisiwani –Kihurio na kuiunganisha na barabara kuu ya Moshi -Dar es salaam- Same mkoani Kilimanjaro
  Kumaliza tatizo la maji katika wilaya ya Same-Same Mjini
  Kuboresha barabara za Igunga -Tabora
  Kusambaza walimu 16,000 katika shule za sekondari zenye upungufu makubwa wa walimu- Kisesa Magu
  Kununua vyandarua viwili kwa kila kaya- Mbeya Mjini
  Kuzipandisha hadhi hospitali maalumu saba nchini kuwa za rufaa ili kuipunguzia mzigo Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MHN)-Hydom Manyara
  Kulinda amani nchini kwa kuzuia chokochoko za kidini, kikabila na kisiasa- Musoma
  Kulinda haki za walemavu- Makete
  Kujenga baabara ya Njombe- Makete kwa kiwango cha lami,urefu wa kilomita 109- Iringa mjini
  Kujenga barabara Musoma–Mto wa Mbu Arusha-Arusha
  Kuanzisha jimbo la Ulyankulu- Shinyanga Mjini
  Kujenga barabara ya lami Manyoni-Kigoma– Kaliua,Tabora
  Kukarabati barabara ya Arusha Moshi-Arusha Mjini
  Kuboresha barabara ya Handeni, Kondoa,mpaka Singida-Dodoma
  Kuwafidia wanakijiji ng’ombe waliopotea wakati wa ukame mwaka 2009- Longido 45.Vijiji vyote vilivyoko kilomita 15 kutoka kwenye bomba kuu la mradi mkuu wa maji wa Ziwa Victoria-Shinyanga-Kahama kuunganishiwa maji - Shinyanga
  Tatizo la umeme kufikia kikomo Novemba mwaka huu mkoani Arusha –Arusha mjini
  Kukopesha wavuvi zana za kilimo-Busekera, Wilaya ya Musoma, .
  Kuwapatia maji wakazi wa Wilaya ya Longido- Longido
  Kujenga barabara ya lami kupitia pembezoni mwa Hifadhi ya Taifa ya Seregenti – Ngorongoro
  Utekelezaji wa mpango wa maendeleo ya kilimo kuwasaidia wafugaji kuweza kupata na kutunza mifugo yao vizuri- Mbulu mkoani Manyara
  Kusambaza maji nchi nzima-Babati vijijini
  Kusambaza umeme, utoaji wa huduma za afya, na uboreshaji wa kilimo cha umwagiliaji na utoaji ruzuku kwa wakulima. mwaka 2010-2015-Babati vijijini Kuongeza mara tatu idadi ya wananchi wanaonufaika na ruzuku ya pembejeo za kilimo kwa mfumo wa vocha.-Iringa
  Kuhakikisha Isimani inapata maji ya uhakika- Iringa
  Kuiwekea lami barabara inayokwenda katika Hifadhi ya Taifa ya Ruaha, ambayo ndiyo hifadhi kubwa kuliko zote Tanzania-Iringa
  Kulinda usalama wa wananchi kwa ujumla ili kudumisha amani na sifa ya nchi-Ifunda
  kutokomeza malaria 2015-Bunda,mkoa wa Mara
  kuwapa wanawake nafasi zaidi-Kilolo ,Iringa
  ahadi kuisadia Zanzibar kuendeleza miradi mbalimbali ya kijamii-Kibandamaiti Mjini Zanzibar
  Kuipandisha hadhi hospitali ya Mnazi Mmoja Zanzibar kuwa ya rufaa-Kabandamaiti mjini Zanzibar
  Kuisaidia Zanzibar kila panapohitajika msaada-Kibandamaiti
  Serikali kujenga upya bandari ya Mbambabay-Ruvuma
  Ununuzi wa Meli mpya yenye uwezo wa kubeba tani 400-Mbambabay Ruvuma
  kufufua chama kikuu cha ushirika cha wakulima wa Mbinga(MBICU) –Ruvuma
  Ahadi Rais wa Marekani Barack Obama kuimwagia misaada Tanzania –Ruvuma
  Ahadi hakutakuwa na umwagaji wa damu baada ya uchaguzi-Dar es Salaam
  Mtwara kuwa mji wa Viwanda –Mtwara
  Ahadi ujenzi wa kwanda cha dawa ya kuua viluilui vya mbu-Kibaha
  Hospitali ya Tumbi kuwa ya mkoa-Kibaha
  Halmashauri ya manispaa ya Kibaha kutenga eneo maalumu la viwanda -Kibaha
   
 5. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #5
  Nov 4, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  sio kosa lake mana alikurupuka kujibu tu, wakati hapa tunachangia mada yeye analeta mipasho,
   
 6. doup

  doup JF-Expert Member

  #6
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 26, 2009
  Messages: 1,172
  Likes Received: 335
  Trophy Points: 180
  safiii
   
 7. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #7
  Nov 4, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,126
  Likes Received: 1,705
  Trophy Points: 280
  Umasikini wa kufikiri na ujinga ulokithiri wa watz wengi ndo mtaji wa mafisadi!
   
 8. L

  LUINASIA New Member

  #8
  Nov 4, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 4
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mfano mzuri alipokua kule mkoa wa manyara JK aliahidi maji kutoka mto ruvu, kwa watu ambao hawajui jografia wataona ni kitu rahisi hivyo wakampa kura .. Je hayo maji yavuke mito yote mikubwa kama wami, mito ya tanga moshin na mbaya zaidi hata ile ya jirani yao Arusha??:hippie:

  Mkuu Hapa utakuwa umejikanyaga. Mkoa wa Manyara kuna wilaya inaitwa Simanjiro na makao makuu ya wilaya ya Simanjiro ni Orkesumet. Kuna mto unaitwa Mto Ruvu ambao unapita umbali wa kilomita 36 kutoka mjini ambako ndiko kumependekezwa kiwe chanzo cha maji. Usanifu wa mradi unaendelea na unafadhiliwa na fedha za nje. Ni kitu ambacho kinajulikana na kipo kenye bajeti. Hata miradi mingine kama ya Same na Mwanga na Dar es salaam zote zipo kwenye pipeline
   
 9. PAS

  PAS JF-Expert Member

  #9
  Nov 4, 2010
  Joined: May 3, 2010
  Messages: 452
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  pamoja na hayo mkuu hivi huo mto umekuepo hapo leo???
  hadi asubiri wakati wa kampeni???
  je wewe unavozani hizo ahadi zake hapo juu atazitekeleza??
  be honest???
   
 10. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #10
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,576
  Likes Received: 4,690
  Trophy Points: 280
  Kataa kubali, mtaji wa CCM ni UJINGA NA UMASIKINI wa watanzania. Ndiyo maana wakidanganywa wanadanganyika, wakipewa fedha kidogo hata elfu 5 wanakubali kuuza haki yao, wakigeuzwa mabango ya JK kwa kupewa fulana ,kanga na kofia wanauza haki yao.Wangekuwa wameelimika vya kutosha na kuwa na hali nzuri ya uchumi wangezichana chana hizo kanga na fulana na kuwapiga mawe hao makuadi wa mafisadi wanaozileta.Na ndiyo maana wanapinga kwa nguvu zote kutoa elimu bure mpaka kidato cha sita kwani watu wakielimika ndiyo mwisho wa hawa majambazi wa CCM kuwa madarakani.
   
 11. sensa

  sensa JF-Expert Member

  #11
  Nov 4, 2010
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 398
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Kuna swala uelewa hapa,ahadi zao ni za kisanii.Afu pia DSM hapa kampeni zilivyoanza barabara karibu zote za mitaa hasa sinza na kinondoni zilichongwa,hivi walikuwa wapi mpaka uchaguzi ufike au ndo kiombea kura,ukiangalia idara fulan fulan za serekali zimeanza kujitangaza kwenye tv sana kwa waliyoyafanya,huo utaratibu ni wa siku zote au kipindi cha uchaguzi tu?kwa bajeti gani na mamlaka gani kutangaza shughuli za umma kama kutangaza biashara.Hiyo hela si ingewasaidia masikini wengi tu wakutupa tulio nao kama hela zipo>Haya sasa uchaguzi umeisha watafanya tena?
   
Loading...