Fahamu kwamba yanayovuma sana kwenye mitandao ya kijamii hayana ukweli

ndenjii handsome

JF-Expert Member
Apr 27, 2021
647
704
Nimekuwa mfuatiliaji sana wa mambo kwa uhalisia wake kwa kipindi kirefu nilichogundua zile taarifa muhimu zinapotolewa kwenye hatua moja na kupelekwa hatua nyingine zimekuwa na chumvi nyingi na sijui wahusika wanafanya haya kwa maana gani.

Siku moja nikiwa mkoa fulani likatokea tukio moja hivi ambalo lilipelekea vyombo vya habari kuja eneo la tukio lakini cha kushangaza nilipokuja kusikiliza kwa baadae kwenye hivyo nitofauti na nilichojionea basi nilichofanya nikapiga simu kwenye media moja wapo kujaribu kusahisha ile ishu lakini nilipoanza kuchangia kuhusu lile tukio kilichonikuta sasa.

Na sio huko tu hata humu ndani tabia hii ipo, watu wanafutiwa nyuzi bila sababu za msingi hasa ikigundulika hizo nyuzi zinagusa taarifa nyeti za watu fulani.

Sio hivyo tu hata ikitokea likapenya kwa uhalisia hill jambo huwa watajitokeza na kukutuhumu.

Kwenu wahusika wa haya mambo mnafanya haya kwa maslahi gani hamjui kama hili ni tatizo?

Ushauri wangu:

Kwa wafuatiliaji sio kila unachokiona kipo kama unavyodhani penda kujiuliza mwenyewe kwenye utawala wa kichwa chako. Tupo kwenye kizazi ambacho ni kigumu kushugulika nacho usije ukapotoka kirahis kwa jambo la kusikia sehemu mwisho wa siku madhara yake ni makubwa.

Nakaribisha michango yenu

Asanten

Sent from my VFD 200 using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom