Fahamu kwa undani kuhusu Halmashauri ya Ilala kupandishwa hadhi na kuwa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam

MIMI BABA YENU

JF-Expert Member
Mar 1, 2019
200
500
Kiutawala Jiji lilikuwa limegawanyika katika Halmashauri sita za Serikali za mitaa ambazo ni:

Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam
Halmashauri ya Manispaa ya Temeke
Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni
Halmashauri ya Manispaa ya Ilala
Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo na
Halmashauri ya Manispaa ya Kigamboni

Sasa, ukiangalia hapo juu kulikuwa kuna chombo tu kinaitwa HALMASHAURI YA JIJI LA DAR ES SALAAM lakini chombo hicho hakikuwa na eneo rasmi la kiutawala kwa maana nyingine halmashuri ya jiji haina ARDHI inayoitawala, kwa maana hiyo inategemea vyanzo vya mapato kutoka halmashauri za manispaa.

Chombo hiki yaani Halmashauri ya Jiji ilikuwa ina meya wake na baraza lake huku halina vyanzo vya mapato, lakini walitenga bajeti.

Sasa swali, unapewaje bajeti huku miradi inaweza kuhudumiwa na manispaa zenyewe? Hivyo kulikuwa na matumizi mabaya ya pesa kwa kuwa ni kama unampa mtu pesa hana matumizi .

Sasa kilichofanyika nikuvua kofia ya Halmashauri ya Jiji na kuipa Ilala.

Na manispaa za Kigamboni, Kinondoni, Ubungo, Temeke zitabaki kama manispaa.
 
mweongo

Member
Aug 23, 2010
58
150
Swali je, huu ndio mpangilo unafaa kwa jiji letu pendwa la Dar. Na je hivi ndio wananci wa Dar wanavyotaka jiji lao liwe au ni kulazimishwa na wana siasa?

Majiji mengine duniani yana setup ya aina gani, je zina fanana na hii ya Dar?
 
Kitwa-Mulomoni

JF-Expert Member
Oct 25, 2016
1,709
2,000
Swali je huu ndio mpangilo unafaa kwa jiji letu pendwa la Dar. Na je hivi ndio wananci wa Dar wanavyotaka jiji lao liwe au ni kulazimishwa na wana siasa?
Ajiji mengine duniani yana setup ya aina gani, je zina fanana na hii ya Dar?
Setup ya majiji mengine kama haifanani na hii yetu, basi wao waige yetu! Siyo kila kitu kiwe ni sisi kuiga tu. Na wengine watuige sisi.
 
MIXOLOGIST

JF-Expert Member
Mar 1, 2016
4,958
2,000
Kwahivyo mimi mkazi wa Mbezi beach naishi nje ya Jiji alafu mkazi wa Chanika yuko ndani ya Jiji
 
bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
11,930
2,000
JIJI LETU JIPYA LA DAR ES SALAAM ILALA

Labda sasa Kariakoo itakuwa kama Dubai biashara masaa 24 , mwanga wa kutosha usiku wote lazima biashara zilizokufa Kariakoo ambazo wafanyabiashara kutoka Zimbabwe, Congo, Malawi , Zambia , Comoro n.k warudi na wasiwaze kwenda China wala Dubai kufuata mzigo.

Na machinga wote watasombwa kubwagwa huko manispaa mpya kimaeneo za Kinondoni, Ubungo, Temeke na Kigamboni.

Jiji la Dar es Salaam "mpya" yaani Ilala litaambaa na barabara ya Nyerere kuchukua ukanda wa Tazara Stesheni DSM, viwanda vote Ukanda wa "Pugu Road " hadi Airport ya Uwanja wa Kimataifa wa JNIA. Jiji hili jipya litaamba Kurasini mivinjeni mpaka bandari zote kavu na bandari yenyewe. Maeneo ya Mjini Kati Posta, Gerezani, Mnazi Mmoja , Upanga, Magomeni hadi Ukanda wa Morogoro road Ubungo Maji mpaka Stendi Mpya Mbezi Louis.

Bila kusahau maeneo ya Oysterbay , Masaki hadi Mawasiliano 2000 stendi yatakuwa ndani ya Jiji jipya la Ilala (Dar es Salaam) lenye miundo-mbinu ya flyover, madaraja , BRT mwendokasi, superfast internet, bila uchafu wa meza za wamachinga, bidhaa kupangwa barabarani sehemu za wenda-kwa-miguu.

Hii itasaidia Jiji jipya la Ilala Dar es Salaam kukusanya kodi kwa kusaidiana na TRA kwa ufanisi huku miundo-mbinu ikibaki wazi na safi kwa wenye shughuli zenye TIN Number TRA na Dar es Salaam jiji jipya kuwa ULAYA ndani ya Africa.

Hawa wamachinga "wametuchelewesha" sana Dar es Salaam yenye miundombinu na magorofa makubwa kuchangia kodi, kwani biashara zimekufa na wameharibu muonekano wa jiji kisa wamechangia Tshs. 20,000 kitambulusho cha mfanyabiashara mdogo wakati wanaharibu mazingira ya biashara kubwa, biashara za kimataifa na hata watu wanakimbiza ofisi zao toka mjini kati kuzipeleka maeneo ya Victoria, Makumbusho ili kuondokana na hawa "wakuja" machinga wasioelewa maana ya jiji.

Watendaji nao wa serikali madiwani, mameya, waDC , Mkuu wa Mkoa bila kusahau viongozi wa CCM ngazi zote Dar es Salaam nao wamekuwa waoga na kukosa ubunifu kulifanya jiji kuwa Dubai au Singapore ya Afrika huku serikali imewekeza matrilioni ya fedha kuinua hadhi ya mji wa Dar es Salaam uwe wa kisasa kufuatana na uwekezaji mkubwa wa Maendeleo ya Vitu uliowekwa jijini Dsm.

mhanila1

JF-Expert Member
Dec 15, 2017
1,018
2,000
Kwani hii serikali yenyewe mapato yake inatoa wapi kama siyo mikoani yenyewe ina ardhi kama siyo inategemea ardhi ya hiyo mikoa. Kwanini na yenyewe isibunjwe halafu jiji la Dodoma lipandiajwe hadhi na kuwa ndiyo serikali ya tanzania? Mambo mengi unasoma halafu unawazaa hivi tunakuwa tu nafikiria kweli kwa makini kabisa.

Huo Muundo uliokuwepo ndiyo muundo sahihi wa jiji sasa kusema Ilala imepemdoshwa hadhi sasa kwanini isiiywe jiji la Ilala kuna shida gani ili manispaa zingine zikipandishwa hadhi ziitwe majiji pia sasa sijui hilo vurugu ni kwa ajiri ya nini. Hivi hadi maniapaa ittwe jiji vigezo vyake ni vipi hasa na hiyo Ilala. Kwahiyo hiyo hilo jiji la ilala linaundwa na manispaa zipo za gondolamboto chanika na mongolandege sijui. Mambo mengine ndiyo Haya Nyerere alikataa ya mtu kumshauriana na mke wake na kuamuwa kutekeleza.

Ni vema tukaangalia sheria zetu na kuweka wigo kwa baadhi ya mambo kuna siku ataamka anasema jiji la dar es Salaam liitwe jiji la nani sijui sababu amefanya kazi nzuri. Ni shida sana hii awamu akija Rais mwengine atakuwa na kazi kama ile anayofanya Joe Biden baada ya vurugu za tramp
 
Dalmine

JF-Expert Member
Sep 8, 2016
5,071
2,000
Kwaiyo Ilala ni kubwa kwa Mikoa mikubwa ya Tanzania? Au wanachoangaria ni mijengo!

Morogoro
Shinyanga
Tabora
Singida
Geita
Kahama
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
82,133
2,000
Endeleeni kuupaka rangi uchafu

Instagram media - CLrsBdunl7R ( 640 X 640 ).jpg
 
Babati

JF-Expert Member
Aug 7, 2014
41,461
2,000
Kwani hii serikali yenyewe mapato yake inatoa wapi kama siyo mikoani yenyewe ina ardhi kama siyo inategemea ardhi ya hiyo mikoa. Kwanini na yenyewe isibunjwe halafu jiji la Dodoma lipandiajwe hadhi na kuwa ndiyo serikali ya tanzania? Mambo mengi unasoma halafu unawazaa hivi tunakuwa tu nafikiria kweli kwa makini kabisa.

Huo Muundo uliokuwepo ndiyo muundo sahihi wa jiji sasa kusema Ilala imepemdoshwa hadhi sasa kwanini isiiywe jiji la Ilala kuna shida gani ili manispaa zingine zikipandishwa hadhi ziitwe majiji pia sasa sijui hilo vurugu ni kwa ajiri ya nini. Hivi hadi maniapaa ittwe jiji vigezo vyake ni vipi hasa na hiyo Ilala. Kwahiyo hiyo hilo jiji la ilala linaundwa na manispaa zipo za gondolamboto chanika na mongolandege sijui. Mambo mengine ndiyo Haya Nyerere alikataa ya mtu kumshauriana na mke wake na kuamuwa kutekeleza.

Ni vema tukaangalia sheria zetu na kuweka wigo kwa baadhi ya mambo kuna siku ataamka anasema jiji la dar es Salaam liitwe jiji la nani sijui sababu amefanya kazi nzuri. Ni shida sana hii awamu akija Rais mwengine atakuwa na kazi kama ile anayofanya Joe Biden baada ya vurugu za tramp
Hakika umenena vyema
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom