Fahamu kwa ufupi kuhusu International Space Station (ISS); kituo cha anga cha kimataifa

I am Groot

JF-Expert Member
Jul 20, 2018
3,726
10,020
INTERNATIONAL SPACE STATION (ISS)

Ni kituo anga za juu cha kimataifa kinachojihusisha na maswala mbalimbali ya kisayansi juu ya tabia anga na mswala ya anga za juu kwa ujumla. Kituo hichi kipo katika mzunguko wa chini wa anga Dunia. Mara nyingine huweza kuonekana kwa macho kikiwa angani kutoka duniani lakini kiking'aa kama nyota itembeayo kwa mwendo wa wastani. Mwendo wake kikiwa angani hufikia mpaka zaidi ya 27,590km/h. Programu ya ISS ni mradi wa ushirikiano wa kitaifa kati ya wakala watano wa shirika zinazoshirikiana kama: NASA, Roscosmos, JAXA, ESA, na CSA.

MAISHA KATIKA ISS
. Wakati wa kukaa kwao kwenye Kituo cha Angani cha Kimataifa cha Space (ISS) lazima waendelee kuishi na kufanya kazi katika mazingira ambayo ni tofauti sana na ile hapa Duniani. ... Hii inamaanisha kuwa wanaanga wanapaswa kuhifadhi rasilimali kama vile maji na chakula na taka zinahitaji kutunzwa kwa kiwango kidogo.Aina hizo za vyakula ni pamoja na mboga zilizohifadhiwa na vyakula kavu kama biscuti, chakula cha jokofu, matunda na bidhaa za maziwa. Leo, orodha ya vyakula kwenye Kituo cha Nafasi cha Kimataifa inajumuisha vitu zaidi ya 100.

CHAKULA.
Wanaanga huchagua menyu yao ya kila siku kwa muda mrefu kabla ya kuruka kwenye nafasi. Kuna milo mitatu kwa siku, pamoja na vitafunio ambavyo vinaweza kuliwa wakati wowote.

SEX/KUJAMIIANA
"Hakuna ushahidi rasmi au usio rasmi kwamba kulikuwa na matukio ya kujamiiana au kufanya majaribio ya kijinsia katika nafasi anga."

MICHEZO
"Alikadhalika wanaanga wa kituo cha sayansi ya anga ya kimataifa (iss) hawawezi kuwa na chaguzo za michezo huko angani kutokana na tafiti zilizowapeleka, lakini ili wasiwe wakiwa, wanaweza kucheza michezo michache katika chumba maalum kati ya vyumba vilivyomo katika chombo hicho cha anga. Michezo hiyo ni kama basket ball isiyohusisha mivutano ya asili (gravitational force), kuendesha baiskeli na kurusha boomerangs pamoja na aina ya mchezo wa golf.

images%20(7).jpg
images%20(8).jpg
[/CENTER]
 
Kwamba hiyo siku hilo unaliona anga zetu Kama ndege vile?
Nafikiri unaongelea muonekano wa hicho kituo huko angani kati ya siku hizo itakapoonekana??
Jibu ni; Itaonekana kama nyota fulani kubwa kiasi kwa kuitazama kwa macho ila kwa kifaa maalumu itaonekana kama kilivyo.
 
Wenzetu wako mbali Sana, sisi tunakanyagana kwenye kukanyaga Mafuta kwa Mwamposa
Ni kweli kabisa. Wanatuacha mbali sana ila hata sisi tunaweza kufanya wafanyacho tukielekezwa namna ya kufanya.
 
Hiyo picha ya pili inayoonesha wakiwa ndani ndio wanaelea hivyo?
 
T
Ni kweli kabisa. Wanatuacha mbali sana ila hata sisi tunaweza kufanya wafanyacho tukielekezwa namna ya kufanya.
Thubutuuu nyie mnaishia kuitumia tako huru na tis kumzidishia mbowe umaskini kisa uchaguzi 2020
 
Sisi tunajua nyungu tu, budget yetu ya tafiti ni Kama hakuna, tunatenga fedha nyingi kudidimiza upinzani badala ya kuwekeza kwenye tafiti za kisayansi
Tujivunie vya nyumbani. Kuwa mzalendo mkuu 😀😀
 
Bill Gates aliwahi ku fund research ya namna/uwezekano wa kugeuza kinyesi cha binadamu kua Chakula ili wana anga wawe wanakigeuza msosi huko huko juu.,wasipate shida ya msosi.

Na niko serious kwenye hili kama kuna anayebisha aseme hapa niweke Link.
 
Sio kubisha weka tujifunze zaidi
 
Bill Gates aliwahi ku fund research ya namna/uwezekano wa kugeuza kinyesi cha binadamu kua Chakula ili wana anga wawe wanakigeuza msosi huko huko juu.,wasipate shida ya msosi.

Na niko serious kwenye hili kama kuna anayebisha aseme hapa niweke Link.
Haha mkuu hebu weka hiyo link hapa tushughudie. Ila jamaa anaonekana anaroho ngumu sana.
 
Hivi kuna nchi ya kiafrica yoyote ile yenye kituo chake huko kwenye anga za kimataifa?
 
CHAKULA.
Wanaanga huchagua menyu yao ya kila siku kwa muda mrefu kabla ya kuruka kwenye nafasi. Kuna milo mitatu kwa siku, pamoja na vitafunio ambavyo vinaweza kuliwa wakati wowote.

SEX/KUJAMIIANA
"Hakuna ushahidi rasmi au usio rasmi kwamba kulikuwa na matukio ya kujamiiana au kufanya majaribio ya kijinsia katika nafasi anga."

Mkuu, Shukrani kwa kutupatia elimu juu ya ISS, naomba niulize; kwakuwa jamaa huko huwa wanakula mara 3 je haja zao huwa wanazihifadhi vipi au wana zi dispose vipi??.

Juu ya sex, umesema kwamba hakuna ushahidi wa jambo hilo kufanyika, je kama ushahidi utapatikana kutatokea nini??
 
Back
Top Bottom