Fahamu kuhusu Uchaguzi wa Raisi USA kwa Mtanzania wa (kawaida)!

Barbarosa

JF-Expert Member
Apr 16, 2015
22,584
27,786
*Hii siyo mada ya international Forums!

Nafahamu kuna Watanzania wengi kama nilivyokuwa mimi hapo awali ambao hawafahamu jinsi Uchaguzi wa USA unavyofanyika, wengi wetu hufikiri kwamba Wamarekani huenda kuchagua Raisi kwa kupiga kura kama vile sisi tufanyavyo na kwamba Mgombea tunayempigia kura nyingi ndio huwa mshindi, siyo hivi Raisi wa USA hapatikani kwa kura za wananchi, bali Raisi wa USA huchaguliwa na watu 538 tu!

Wamarekani wakienda kwenye Uchaguzi mwezi Novemba mwaka huu hawaendi kumpigia kura Raisi wa USA kama ambavyo wengi wetu hufikiri bali huenda kuchagua watu waitwao electors ambao ni watu 538!

Kwa mfano mtu atakayaempigia kura D.Trump siyo kwamba amemchagua Trump bali amechagua electors na hili hufanyika nchi nzima, ktk Majimbo yote ya USA, sasa hawa electors 538 ndiyo hupiga kura kuchagua Raisi wa USA!

Hivyo basi uchaguzi wa USA hufanyika kwa Awamu Mbili, awamu ya kwanza ni ambayo ni mwezi Novemba na ndiyo hutangazwa Dunia nzima kama siku ya uchaguzi lkn siku hii Wamarekani hawachagui Raisi wa USA bali ni kuchagua electors ktk kila Jimbo!

Awamu ya Pili ya Uchaguzi hufanyika Mwezi Desemba na hii ndiyo huamua raisi wa USA, ambapo sasa hawa maelectors 538 waliopigiwa kura na Wananchi hupiga kura kuchagua Raisi wa USA, hivyo basi Raisi wa USA huchaguliwa na Watu 538 na siyo wapiga kura wote wa USA!

Kama kuna mtu ana ufahamu zaidi anaweza kuongezea au kurekebisha nilichoandika kwa manufaa ya Watanzania wote, hasa wale ambao kama mimi nilivyokuwa, hawafahamu jinsi Raisi wa USA anavyopatikana!
 
Back
Top Bottom