Umeshasikia kuhusu 'DEEP WEB'?

View attachment 900013
Muonekano wa Orbot na Orfox
View attachment 900014
Hicho kitunguu hapo mwanzoni kitakuwa kinasoma start. Uki-click ndio kinaanza ku-establish connection.
VPN mode na Bridges ni additional options endapo utapendaView attachment 900015View attachment 900016
Screenshot_20181016-172751.jpeg

Mwonekano wa Orbot mwanzoni
Screenshot_20181016-173126.jpeg

Hapa ni chaguzi za wapi unapenda traffics ziwe routed ili kuficha location yako
Screenshot_20181016-172740.jpeg

VPN mode
Screenshot_20181016-172728.jpeg

Bridge mode (chagua servers za ku-route traffics)
 
kwa wale wapenzi wa Torrent and Movies hizi hapa links zitakazo kuwezesha kutembelea torrents na sites za kustream na ku download movies, documents, games na mengineyo

Aaah sasa mkuuu nimesikia hukoo nii hatariii mambo ya Ku download tenaa, Na umegusa kwenye ugonjwa wanguu aisee
 
wabongo tupunguze uwoga! hao wanaokuambia usiende huko panatisha wao wamejuaje kama hawakuingia? cha msingi fata maelekezo waliotoa wadau then nenda kajionee mwenyewe...
 
Hakika ulimwengu huu una mambo mengi ambayo hatuyafahamu bado, kila siku tunaweza kujifunza jambo jipya hadi mwisho wa maisha yetu.

Intaneti ni kitu ambacho kwa ulimwengu huu wa sasa kila mtu anakitumia kwa njia moja au nyingine. Jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na kutumika huku kwa intaneti bado kuna mambo mengi ya kushangaza tusiyoyajua.

Je wajua kuwa ipo sehemu ya mtandao wa intaneti iliyofichwa? Sehemu hii inajulikana kama Deep web na Dark web.
Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe juu ya sehemu hii ya mtandao wa intaneti iliyofichwa (Deep web na Dark web)
Deep web ni nini?

Deep web ni sehemu ya intaneti ambayo haionekani kwenye injini pekuzi kama vile Google na Bing — moja kwa moja injini pekuzi haziwezi kuona sehemu hii kwa sababu imefichwa isionekane.

Deep web siyo kitu kilicho nje ya huu ulimwengu bali ni kitu ambacho umekuwa ukikitumia mara kwa mara — barua pepe yako, benki mtandao, meseji zako za Twitter, LinkedIn n.k Taarifa hizi haziwezi kuonekana kwenye injini pekuzi kwa kuwa zinalindwa kwa nywila (password) au kulipiwa ili kuziona.

“Vitu vyote visivyoweza kupatikana kwenye uso wa juu wa mtandao kwa kutumia injini pekuzi ni sehemu ya Deep web”
Ikizingatiwa kuwa tuna mabilioni ya watumiaji wa mtando wa intaneti duniani, hivyo inaelezwa kuwa kuna mamilioni ya taarifa au data zilizoko kwenye Deep web.

Hata hivyo inaminika kuwa Deep web inaunda sehemu kubwa ya mtandao; Deep web inaweza kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida kama vile Chrome na Firefox.

Dark web ni nini?

Dark web siyo sehemu tofauti na intaneti bali ni sehemu ya Deep web ambayo haiwezi kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida.

Kwa nini Dark web haiwezi kuonwa kwa kivinjari cha kawaida? Ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web ni haramu, si rahisi wahusika wake kuruhusu mambo haya kuonekana kwenye vivinjari vya kawaida.

Je kwenye Dark web kuna shughuli gani?

Uuzaji wa madawa ya kulevya
Uhalifu wa kila namna (uuzaji wa viungo vya binadamu, ajira za kutisha, ugaidi n.k)
Wadukuzi hatari wa kompyuta
Uuzaji wa taarifa na vitu vilivyoibiwa
Picha za unyanyasaji wa kingono hasa watoto
Uuzaji wa silaha
Mawasiliano ya wanaharakati na waandishi wa habari wanaotaka kuibua maswala mbalimbali. Hutumia njia hii kujificha wasije wakakamatwa na serikali au mahasimu wao. Mtandao wa wikileaks unapokea pia taarifa kupitia Dark web.
Je tovuti za Dark web zinaperuziwaje?

Tovuti za Dark web zinaishia na anwani mtandao (domain) zenye .onion, ambazo zinaweza kufunguliwa kwa kutumia kivinjari cha Tor pekee.

Tor ni kivinjari (browser) cha namna gani?

Tor ni kivinjari kilichotengenezwa na watu wakujitolea (voluntiers) kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambacho hufanya kazi kwa usiri wa hali ya juu wa kuficha mawasiliano pamoja na watumiaji wake.

Hivyo mtu anayetembelea tovuti fulani au kufanya chochote kwenye mtandao kwa kutumia kivinjari hiki siyo rahisi kubainika.

Kwa mfano unaweza ukawa unaperuzi mtandao kwa kutumia Tor ukiwa Tanzania lakini ukaonekana mara uko Japan, mara Uingereza au hata Marekani.T browser

Ikumbukwe kuwa kutembelea Dark web siyo kinyume cha sheria lakini kufanya vitu huko kunaweza kuwa kinyume cha sheria kutokana na tovuti nyingi kufanya vitu vinavyokiuka sheria.

Kwenye Dark web siyo mahali panapovutia kama sehemu ya kawaida ya mtandao wa intaneti tulio uzoea. Tovuti nyingi huku zimetengenezwa kwa makusudi maalumu au pengine ya siri, hivyo hazikujali wala kukulinda.

Ili kuperuzi kwenye Dark web ni lazima uwe na kiungo (link) cha tovuti unayotaka kutembelea kinachoishia na .onion kwa mfano http://zqktlwi4fecvo6ri.onion. Hii ndiyo Dark web, hakuna kugoogle hapa; mambo yanaenda kwa namna ya ajabu ajabu tu.

Je Dark web ni mbaya?

Hapa kuna majibu mawili ndiyo na hapana. Pamoja na kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web sio halali, bado kuna toleo lake la Facebook na ProPublica kwa anauani ya .onion.

Lakini ukumbuke kuwa wachambuzi wa mambo wanasema tovuti hizi zinaweza zisiwe za kweli, kwani si rahisi Fecebook kukubali watumiaji wake kutumia anwani za kujificha za .onion. Hivyo kuwa makini na taarifa zako za siri huku.

Uzuri wa Dark web ni kuwa inawawezesha waandishi wa habari, wanaharakati na wale wanaoibua taarifa za siri kuwasiliana na kubadilishana taarifa bila wao kujulikana.

Ni wazi kuwa hakuna kitu kibaya kwenye mtandao bali ni matumizi pekee ndiyo hukifanya kiwe kibaya.

Neno la mwisho

Naamini umejifunza mengi ambayo hukuwa unayafahamu kuhusu sehemu ya intaneti iliyofichwa. Lakini pamoja na hayo uliyojifunza ningependa kukushauri kuwa makini sana kama utaamua kutumia Dark web. Kumbuka pia kuzingatia sheria kwani uhalifu, maovu na ukatili wa kutisha umejaa kwenye Dark web.

Kwa mfano picha za video za watu wakichinjwa, ubakaji wa watoto, wizi, chuki na ubaguzi husambazwa bila woga wowote. Wadukuzi hatari pia wamejaa kwenye Dark web, hivyo epuka kutoa taarifa zako, kupakua kitu chochote au kufanya muamala wowote.
Elimu maridhawa
 
ok kwa hiyo kumbe wanakuwa na server zao
Yes, asilimia kubwa. Ni risk sana kuwa na centralized server ktk known location. VirtualMachines na pia kama zitakuwa online muda mrefu ni risk kuwa tracked na kupatikan. Keep in mind kuwa asilimia kubwa ya vitu vinafanyika ktk dark web ni illegal na penalties zake sio za kitoto.
Kama upo interested cheki online kuhusu aliyeanzisha silk road moja ya sites zilizowahi kutikisa sana. Kuna mengi sana ambayo hatuyafahamu. Sio kila kitu ktk mitandao ni cha kuamini even in the dark web, you just have to know kile unakitafuta na wapi pa kukipata. Otherwise utakuwa umeingia ktk bwala la tope
 
Yes, asilimia kubwa. Ni risk sana kuwa na centralized server ktk known location. VirtualMachines na pia kama zitakuwa online muda mrefu ni risk kuwa tracked na kupatikan. Keep in mind kuwa asilimia kubwa ya vitu vinafanyika ktk dark web ni illegal na penalties zake sio za kitoto.
Kama upo interested cheki online kuhusu aliyeanzisha silk road moja ya sites zilizowahi kutikisa sana. Kuna mengi sana ambayo hatuyafahamu. Sio kila kitu ktk mitandao ni cha kuamini even in the dark web, you just have to know kile unakitafuta na wapi pa kukipata. Otherwise utakuwa umeingia ktk bwala la tope
Yap nimecheki naona Ross Ulbricht alifungwa jela maisha tena hawezi kutolewa hata kwa parole
 
Yap nimecheki naona Ross Ulbricht alifungwa jela maisha tena hawezi kutolewa hata kwa parole
But kama umesoma kwa kina upande wa ushahidi wake kuna facts nyingi sana sio yeye pekee aliyekuwa akiendesha silk road. Walikuwa 3 na hawafahamiani as insurance policy endapo mmoja atakamtwa wengine watakuwa huru. Amehukumiwa kwa circumstantial evidence kwa sababu ni ngumu sana kuthibitisha mashitaka yao na tayari walishatumia billions of money ktk kumtafuta mhusika only to find out walikuwa watatu. So kifungo chake somehow bado kina utata kama kweli walimpata mtu sahihi au walitaka ku-justify matumizi makubwa ya hela na muda
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom