Fahamu Kuhusu Sehemu ya Mtandao wa Intaneti Iliyofichwa (Deep web na Dark web)

gwankos

gwankos

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Messages
326
Points
500
gwankos

gwankos

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2017
326 500
Hakika ulimwengu huu una mambo mengi ambayo hatuyafahamu bado, kila siku tunaweza kujifunza jambo jipya hadi mwisho wa maisha yetu.

Intaneti ni kitu ambacho kwa ulimwengu huu wa sasa kila mtu anakitumia kwa njia moja au nyingine. Jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na kutumika huku kwa intaneti bado kuna mambo mengi ya kushangaza tusiyoyajua.

Je wajua kuwa ipo sehemu ya mtandao wa intaneti iliyofichwa? Sehemu hii inajulikana kama Deep web na Dark web.
Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe juu ya sehemu hii ya mtandao wa intaneti iliyofichwa (Deep web na Dark web)
Deep web ni nini?

Deep web ni sehemu ya intaneti ambayo haionekani kwenye injini pekuzi kama vile Google na Bing — moja kwa moja injini pekuzi haziwezi kuona sehemu hii kwa sababu imefichwa isionekane.

Deep web siyo kitu kilicho nje ya huu ulimwengu bali ni kitu ambacho umekuwa ukikitumia mara kwa mara — barua pepe yako, benki mtandao, meseji zako za Twitter, LinkedIn n.k Taarifa hizi haziwezi kuonekana kwenye injini pekuzi kwa kuwa zinalindwa kwa nywila (password) au kulipiwa ili kuziona.

“Vitu vyote visivyoweza kupatikana kwenye uso wa juu wa mtandao kwa kutumia injini pekuzi ni sehemu ya Deep web”
Ikizingatiwa kuwa tuna mabilioni ya watumiaji wa mtando wa intaneti duniani, hivyo inaelezwa kuwa kuna mamilioni ya taarifa au data zilizoko kwenye Deep web.

Hata hivyo inaminika kuwa Deep web inaunda sehemu kubwa ya mtandao; Deep web inaweza kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida kama vile Chrome na Firefox.

Dark web ni nini?

Dark web siyo sehemu tofauti na intaneti bali ni sehemu ya Deep web ambayo haiwezi kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida.

Kwa nini Dark web haiwezi kuonwa kwa kivinjari cha kawaida? Ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web ni haramu, si rahisi wahusika wake kuruhusu mambo haya kuonekana kwenye vivinjari vya kawaida.

Je kwenye Dark web kuna shughuli gani?

Uuzaji wa madawa ya kulevya
Uhalifu wa kila namna (uuzaji wa viungo vya binadamu, ajira za kutisha, ugaidi n.k)
Wadukuzi hatari wa kompyuta
Uuzaji wa taarifa na vitu vilivyoibiwa
Picha za unyanyasaji wa kingono hasa watoto
Uuzaji wa silaha
Mawasiliano ya wanaharakati na waandishi wa habari wanaotaka kuibua maswala mbalimbali. Hutumia njia hii kujificha wasije wakakamatwa na serikali au mahasimu wao. Mtandao wa wikileaks unapokea pia taarifa kupitia Dark web.
Je tovuti za Dark web zinaperuziwaje?

Tovuti za Dark web zinaishia na anwani mtandao (domain) zenye .onion, ambazo zinaweza kufunguliwa kwa kutumia kivinjari cha Tor pekee.

Tor ni kivinjari (browser) cha namna gani?

Tor ni kivinjari kilichotengenezwa na watu wakujitolea (voluntiers) kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambacho hufanya kazi kwa usiri wa hali ya juu wa kuficha mawasiliano pamoja na watumiaji wake.

Hivyo mtu anayetembelea tovuti fulani au kufanya chochote kwenye mtandao kwa kutumia kivinjari hiki siyo rahisi kubainika.

Kwa mfano unaweza ukawa unaperuzi mtandao kwa kutumia Tor ukiwa Tanzania lakini ukaonekana mara uko Japan, mara Uingereza au hata Marekani.T browser

Ikumbukwe kuwa kutembelea Dark web siyo kinyume cha sheria lakini kufanya vitu huko kunaweza kuwa kinyume cha sheria kutokana na tovuti nyingi kufanya vitu vinavyokiuka sheria.

Kwenye Dark web siyo mahali panapovutia kama sehemu ya kawaida ya mtandao wa intaneti tulio uzoea. Tovuti nyingi huku zimetengenezwa kwa makusudi maalumu au pengine ya siri, hivyo hazikujali wala kukulinda.

Ili kuperuzi kwenye Dark web ni lazima uwe na kiungo (link) cha tovuti unayotaka kutembelea kinachoishia na .onion kwa mfano http://zqktlwi4fecvo6ri.onion. Hii ndiyo Dark web, hakuna kugoogle hapa; mambo yanaenda kwa namna ya ajabu ajabu tu.

Je Dark web ni mbaya?

Hapa kuna majibu mawili ndiyo na hapana. Pamoja na kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web sio halali, bado kuna toleo lake la Facebook na ProPublica kwa anauani ya .onion.

Lakini ukumbuke kuwa wachambuzi wa mambo wanasema tovuti hizi zinaweza zisiwe za kweli, kwani si rahisi Fecebook kukubali watumiaji wake kutumia anwani za kujificha za .onion. Hivyo kuwa makini na taarifa zako za siri huku.

Uzuri wa Dark web ni kuwa inawawezesha waandishi wa habari, wanaharakati na wale wanaoibua taarifa za siri kuwasiliana na kubadilishana taarifa bila wao kujulikana.

Ni wazi kuwa hakuna kitu kibaya kwenye mtandao bali ni matumizi pekee ndiyo hukifanya kiwe kibaya.

Neno la mwisho

Naamini umejifunza mengi ambayo hukuwa unayafahamu kuhusu sehemu ya intaneti iliyofichwa. Lakini pamoja na hayo uliyojifunza ningependa kukushauri kuwa makini sana kama utaamua kutumia Dark web. Kumbuka pia kuzingatia sheria kwani uhalifu, maovu na ukatili wa kutisha umejaa kwenye Dark web.

Kwa mfano picha za video za watu wakichinjwa, ubakaji wa watoto, wizi, chuki na ubaguzi husambazwa bila woga wowote. Wadukuzi hatari pia wamejaa kwenye Dark web, hivyo epuka kutoa taarifa zako, kupakua kitu chochote au kufanya muamala wowote.
 
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined
Dec 18, 2018
Messages
493
Points
250
JESUIT MASTER

JESUIT MASTER

JF-Expert Member
Joined Dec 18, 2018
493 250

Kama unataka jua zaidi gusa hapa Vatican Inamiliki Dunia - JamiiForums
 
H sanny

H sanny

Senior Member
Joined
May 25, 2018
Messages
161
Points
250
H sanny

H sanny

Senior Member
Joined May 25, 2018
161 250
Hapana huko hakufahi kabisa, niliwahi kuingia na kila siku ilikuwa lazima nitembekee web yao, kuna MTU alinionya kuwa niachane na hii web ila nikawa mmbishi. Kuna siku nimeingia kwenye web yao simu ilizima hapo hapo jumla na mpaka Leo ilishindikana kutengeneza IPO ndani ile smartphone ni kopo nikanunua nyingine. NawaOmbeni achana na hiyo dark web kama huna kazi nao
Pole saana mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
sheremaya

sheremaya

JF-Expert Member
Joined
Mar 22, 2015
Messages
2,814
Points
2,000
sheremaya

sheremaya

JF-Expert Member
Joined Mar 22, 2015
2,814 2,000
Kunaogopesha sana, nimeingia usiku saa 10 simu ilizima gafla ndo imewaka saivi...hawa jamaa wanatumia kitu gani? Hata screenshot huwez kupiga,hata kudownload picha!!!!! TZ kumbe bado tupo gizani sana.....
Kwanini usitumie simu nyingine kuoiga picha au camera..kwani lazima uscreenshot?
 
Moe Szyslak

Moe Szyslak

Senior Member
Joined
Nov 6, 2016
Messages
175
Points
250
Moe Szyslak

Moe Szyslak

Senior Member
Joined Nov 6, 2016
175 250
Kunaogopesha sana, nimeingia usiku saa 10 simu ilizima gafla ndo imewaka saivi...hawa jamaa wanatumia kitu gani? Hata screenshot huwez kupiga,hata kudownload picha!!!!! TZ kumbe bado tupo gizani sana.....
Ni security measure kuhakikisha inaendelea kuwa secure
 
kingzard

kingzard

JF-Expert Member
Joined
Aug 15, 2017
Messages
404
Points
500
kingzard

kingzard

JF-Expert Member
Joined Aug 15, 2017
404 500
Nimetoka ukoo mda co mrefu ni pakawaidawa sana ila tyu uwez piga screen shoot but biashara iko waz waz kabsa
NOTE:kam unatumia tecno na ndugu zake ucende ukoo
 
Lord eyes

Lord eyes

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2018
Messages
5,535
Points
1,995
Lord eyes

Lord eyes

JF-Expert Member
Joined Aug 2, 2018
5,535 1,995
Sawa vipi kuhusu free masoni nawo wapo na wanafanya vitu gani na vipi kuhusu illuminat na nina fikiria huwenda kigogo 2014 atakuwa anaitumia kupata info za yanayo endelea tusio ya jua
 
Don Vito

Don Vito

JF-Expert Member
Joined
Jul 15, 2018
Messages
374
Points
500
Don Vito

Don Vito

JF-Expert Member
Joined Jul 15, 2018
374 500
Nimejaribu kuingia naona cm yangu inapiga picha za ghetto automatic haizim nimeiacha nje kwanza nawaza nikaiweke kwenye maji chakushangaza kila naipeleka nje naikuta ndan jaman plzz msiingie huko
Hahaaa . Muthengee kweli wewe
 
marcs

marcs

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2016
Messages
999
Points
1,000
marcs

marcs

JF-Expert Member
Joined Nov 2, 2016
999 1,000
Nauli yake bei gani na unalipa wapi nijiuzeni wakuu nataka kwenda huko soon imposible
Ushauri ukitaka kwenda huko download VPN ( nzuri ukanunua original) kisha download tor browser /,orbot ,kisha zama huko ukajionee
 
Chachasteven

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined
Jul 4, 2014
Messages
1,059
Points
2,000
Chachasteven

Chachasteven

JF-Expert Member
Joined Jul 4, 2014
1,059 2,000
Niliachana na hii kitu baada ya kujua wale jamaa wanaweza hack hata camera ya PC yako. Wakawa wanafwatilia nyendo zako.

Pia kuthibisha huko ni hatari kuna kiutani maarufu wanasema "nilivutiwa na stories za dark web hadi nilipofungua nikakuta (Mimi) ninauzwa."
 
Forum statistics

Threads 1,326,245
Members 509,448
Posts 32,215,659
Top