Fahamu Kuhusu Sehemu ya Mtandao wa Intaneti Iliyofichwa (Deep web na Dark web)

gwankos

gwankos

JF-Expert Member
Joined
Dec 28, 2017
Messages
326
Points
500
gwankos

gwankos

JF-Expert Member
Joined Dec 28, 2017
326 500
Hakika ulimwengu huu una mambo mengi ambayo hatuyafahamu bado, kila siku tunaweza kujifunza jambo jipya hadi mwisho wa maisha yetu.

Intaneti ni kitu ambacho kwa ulimwengu huu wa sasa kila mtu anakitumia kwa njia moja au nyingine. Jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na kutumika huku kwa intaneti bado kuna mambo mengi ya kushangaza tusiyoyajua.

Je wajua kuwa ipo sehemu ya mtandao wa intaneti iliyofichwa? Sehemu hii inajulikana kama Deep web na Dark web.
Karibu ufuatilie makala hii ili nikufahamishe juu ya sehemu hii ya mtandao wa intaneti iliyofichwa (Deep web na Dark web)
Deep web ni nini?

Deep web ni sehemu ya intaneti ambayo haionekani kwenye injini pekuzi kama vile Google na Bing — moja kwa moja injini pekuzi haziwezi kuona sehemu hii kwa sababu imefichwa isionekane.

Deep web siyo kitu kilicho nje ya huu ulimwengu bali ni kitu ambacho umekuwa ukikitumia mara kwa mara — barua pepe yako, benki mtandao, meseji zako za Twitter, LinkedIn n.k Taarifa hizi haziwezi kuonekana kwenye injini pekuzi kwa kuwa zinalindwa kwa nywila (password) au kulipiwa ili kuziona.

“Vitu vyote visivyoweza kupatikana kwenye uso wa juu wa mtandao kwa kutumia injini pekuzi ni sehemu ya Deep web”
Ikizingatiwa kuwa tuna mabilioni ya watumiaji wa mtando wa intaneti duniani, hivyo inaelezwa kuwa kuna mamilioni ya taarifa au data zilizoko kwenye Deep web.

Hata hivyo inaminika kuwa Deep web inaunda sehemu kubwa ya mtandao; Deep web inaweza kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida kama vile Chrome na Firefox.

Dark web ni nini?

Dark web siyo sehemu tofauti na intaneti bali ni sehemu ya Deep web ambayo haiwezi kuonwa kwa kutumia kivinjari (browser) cha kawaida.

Kwa nini Dark web haiwezi kuonwa kwa kivinjari cha kawaida? Ikizingatiwa kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web ni haramu, si rahisi wahusika wake kuruhusu mambo haya kuonekana kwenye vivinjari vya kawaida.

Je kwenye Dark web kuna shughuli gani?

Uuzaji wa madawa ya kulevya
Uhalifu wa kila namna (uuzaji wa viungo vya binadamu, ajira za kutisha, ugaidi n.k)
Wadukuzi hatari wa kompyuta
Uuzaji wa taarifa na vitu vilivyoibiwa
Picha za unyanyasaji wa kingono hasa watoto
Uuzaji wa silaha
Mawasiliano ya wanaharakati na waandishi wa habari wanaotaka kuibua maswala mbalimbali. Hutumia njia hii kujificha wasije wakakamatwa na serikali au mahasimu wao. Mtandao wa wikileaks unapokea pia taarifa kupitia Dark web.
Je tovuti za Dark web zinaperuziwaje?

Tovuti za Dark web zinaishia na anwani mtandao (domain) zenye .onion, ambazo zinaweza kufunguliwa kwa kutumia kivinjari cha Tor pekee.

Tor ni kivinjari (browser) cha namna gani?

Tor ni kivinjari kilichotengenezwa na watu wakujitolea (voluntiers) kutoka sehemu mbalimbali duniani, ambacho hufanya kazi kwa usiri wa hali ya juu wa kuficha mawasiliano pamoja na watumiaji wake.

Hivyo mtu anayetembelea tovuti fulani au kufanya chochote kwenye mtandao kwa kutumia kivinjari hiki siyo rahisi kubainika.

Kwa mfano unaweza ukawa unaperuzi mtandao kwa kutumia Tor ukiwa Tanzania lakini ukaonekana mara uko Japan, mara Uingereza au hata Marekani.T browser

Ikumbukwe kuwa kutembelea Dark web siyo kinyume cha sheria lakini kufanya vitu huko kunaweza kuwa kinyume cha sheria kutokana na tovuti nyingi kufanya vitu vinavyokiuka sheria.

Kwenye Dark web siyo mahali panapovutia kama sehemu ya kawaida ya mtandao wa intaneti tulio uzoea. Tovuti nyingi huku zimetengenezwa kwa makusudi maalumu au pengine ya siri, hivyo hazikujali wala kukulinda.

Ili kuperuzi kwenye Dark web ni lazima uwe na kiungo (link) cha tovuti unayotaka kutembelea kinachoishia na .onion kwa mfano http://zqktlwi4fecvo6ri.onion. Hii ndiyo Dark web, hakuna kugoogle hapa; mambo yanaenda kwa namna ya ajabu ajabu tu.

Je Dark web ni mbaya?

Hapa kuna majibu mawili ndiyo na hapana. Pamoja na kuwa shughuli nyingi zinazofanyika kwenye Dark web sio halali, bado kuna toleo lake la Facebook na ProPublica kwa anauani ya .onion.

Lakini ukumbuke kuwa wachambuzi wa mambo wanasema tovuti hizi zinaweza zisiwe za kweli, kwani si rahisi Fecebook kukubali watumiaji wake kutumia anwani za kujificha za .onion. Hivyo kuwa makini na taarifa zako za siri huku.

Uzuri wa Dark web ni kuwa inawawezesha waandishi wa habari, wanaharakati na wale wanaoibua taarifa za siri kuwasiliana na kubadilishana taarifa bila wao kujulikana.

Ni wazi kuwa hakuna kitu kibaya kwenye mtandao bali ni matumizi pekee ndiyo hukifanya kiwe kibaya.

Neno la mwisho

Naamini umejifunza mengi ambayo hukuwa unayafahamu kuhusu sehemu ya intaneti iliyofichwa. Lakini pamoja na hayo uliyojifunza ningependa kukushauri kuwa makini sana kama utaamua kutumia Dark web. Kumbuka pia kuzingatia sheria kwani uhalifu, maovu na ukatili wa kutisha umejaa kwenye Dark web.

Kwa mfano picha za video za watu wakichinjwa, ubakaji wa watoto, wizi, chuki na ubaguzi husambazwa bila woga wowote. Wadukuzi hatari pia wamejaa kwenye Dark web, hivyo epuka kutoa taarifa zako, kupakua kitu chochote au kufanya muamala wowote.
 
GAS STATE

GAS STATE

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2017
Messages
1,637
Points
2,000
GAS STATE

GAS STATE

JF-Expert Member
Joined Mar 1, 2017
1,637 2,000
kwa hiyo kati ya google, mozila, bing etc ipi ni browser salama
 
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined
Apr 23, 2018
Messages
115
Points
250
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined Apr 23, 2018
115 250
Yaah huko kuna tisha sana unaweza kwenda na usirudi salama, yaani kule ni dunia nyingine, kuna jamaa anauza huko Nuclear Bomb anataka nimtumie advance billion 160, kwa njia ya Bitcoin, hapa nataka niende Nikaangalie mchakato bandarini nalipitisha hapo nione nitatoswa kodi how much na TRA.....
why unanunua nuclear bomb!
 
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined
Apr 23, 2018
Messages
115
Points
250
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined Apr 23, 2018
115 250
Msiogope kuthubu kuchunguliako, kwani mna nini!. Ni waharifu kwamba mkidukuliwa mtakamatwa! they don't waste time with nobody's unless uko interested na business zao
 
mtu chake

mtu chake

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Messages
15,297
Points
2,000
mtu chake

mtu chake

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2010
15,297 2,000
kwa hiyo kati ya google, mozila, bing etc ipi ni browser salama
Ukitaka kuingia huko uwe na VPN Strong ( au uwe mkali wa network security) nawatumia DDG ( Duck Duck Go ) iko km google ,website nyingi huko ni dot Onion ,na si dot com
 
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined
Apr 23, 2018
Messages
115
Points
250
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined Apr 23, 2018
115 250
Kwa upande wa simu unahitaji application mbili.
Orbot - ku-establish vpn au bridge connection
Orfox - ku-browse

For starters unaweza kutembelea deepweblinks.org kupata baadhi ya links zilizopangiliwa katika different categories

Search engine kama duckduck to go etc
Nikishadownload orbit nafanya nini ili kuestablish VPN?
 
mkaamweusi

mkaamweusi

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2013
Messages
428
Points
500
mkaamweusi

mkaamweusi

JF-Expert Member
Joined Feb 19, 2013
428 500
Nimesoma comment wee,mi ata sielewi mnazungumzia nini!!!,Ngoja nisepe zangu!
 
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined
Aug 6, 2018
Messages
2,687
Points
2,000
M

Marwa_J_Merengo

JF-Expert Member
Joined Aug 6, 2018
2,687 2,000
Hivi hizo .onion domains huwa zinahostiwa kwenye server gani
 
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined
Apr 23, 2018
Messages
115
Points
250
dramaqueen1

dramaqueen1

Senior Member
Joined Apr 23, 2018
115 250
Nami lazima nizame huko huu uthubut muhimu,wengine wanaweza sisi tunakalia woga tu,hela hatuna ,nyumba tunaishi za mbavu za mbwa ,liwalo na liwe , naomba maelekezo ya kina nizame huko walikojoficha na biashara zao
Yeah ni lazima kutoka out of your comfort zone ili ugrow kama binadamu

Ukikuta kuna nafasi za kazi nikumbuke na mimi mkuu
 
Moe Szyslak

Moe Szyslak

Senior Member
Joined
Nov 6, 2016
Messages
175
Points
250
Moe Szyslak

Moe Szyslak

Senior Member
Joined Nov 6, 2016
175 250
Yeah ni lazima kutoka out of your comfort zone ili ugrow kama binadamu

Ukikuta kuna nafasi za kazi nikumbuke na mimi mkuu
screenshot_20181016-171933-jpeg.900013

Muonekano wa Orbot na Orfox
screenshot_20181016-171556-jpeg.900014

Hicho kitunguu hapo mwanzoni kitakuwa kinasoma start. Uki-click ndio kinaanza ku-establish connection.
VPN mode na Bridges ni additional options endapo utapenda
screenshot_20181016-171505-jpeg.900015
screenshot_20181016-171544-jpeg.900016
 
Moe Szyslak

Moe Szyslak

Senior Member
Joined
Nov 6, 2016
Messages
175
Points
250
Moe Szyslak

Moe Szyslak

Senior Member
Joined Nov 6, 2016
175 250
mtu chake

mtu chake

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2010
Messages
15,297
Points
2,000
mtu chake

mtu chake

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2010
15,297 2,000
Mbn tunatishana kizembee... Mpk mkajua hayo siinamaana na nyie mmeshatembelea kweny maeneo yaoo ssa mbona hamjadhurikaa ?
Hahahaha, hebu kachungulie na wewe Mkuu ,utupe jibu
 
MSILOMBO

MSILOMBO

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2015
Messages
484
Points
500
MSILOMBO

MSILOMBO

JF-Expert Member
Joined Dec 3, 2015
484 500
kwa wale wapenzi wa Torrent and Movies hizi hapa links zitakazo kuwezesha kutembelea torrents na sites za kustream na ku download movies, documents, games na mengineyo

Aaah sasa mkuuu nimesikia hukoo nii hatariii mambo ya Ku download tenaa, Na umegusa kwenye ugonjwa wanguu aisee
 

Forum statistics

Threads 1,326,252
Members 509,458
Posts 32,215,859
Top